Leo Ndiyo Siku Yako

Leo Ndiyo Siku Yako

MSHUAH

Member
Joined
Nov 8, 2023
Posts
17
Reaction score
126
"Kifo chako kitakuja siku ya kawaida, katikati ya mipango ambayo haijakamilika, na dunia itaendelea bila wewe. Hivyo basi, ishi kidogo."

Kifo chako hakitakuja kwa tangazo au maandalizi maalum. Kitakuja siku ya kawaida kabisa, ukiwa katikati ya mipango ambayo bado hujakamilisha, ndoto ambazo bado hujazifikia, na mambo ambayo uliahirisha ukisema, “nitafanya baadaye.” Na ukweli mchungu ni huu: dunia haitaacha kuzunguka kwa sababu umeondoka. Watu wataendelea na maisha yao, siku zitaendelea kupita, na kila kitu kitaendelea kana kwamba hakuna kilichotokea.

Hii ndiyo sababu unapaswa kuishi kweli. Acha kuahirisha furaha yako, acha kuishi kwa hofu ya maoni ya watu, acha kusubiri muda “sahihi” ambao hauji. Fanya unachotaka, sema unachojisikia, chukua hatua hata kama unaogopa. Maisha hayakusubiri ujiandae kikamilifu. Ukiendelea kuchelewa, utapoteza nafasi ya kuyaishi kabisa.
 
na wala hakuna ajuae saa wala muda, mwana wa Adam atakapomjia.

Ishi na watu vizuri sasa bila kuahirisha unayoyaahirisha daily 🐒
 
Kwenye haya maisha usipokua makini unaweza kujikuta muda wako wote wa uhai uliutumia kukimbizana na hela tu na ukasahau kuishi,

Don't forget to enjoy your life while chasing your dreams.
Life is a gift,don't forget to live it.
 
Sahihi 📌
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom