Leo natimiza miaka minne ya bila kuhonga

Tajiri Mapesa

JF-Expert Member
Feb 26, 2020
707
698
Habarini za leo wakuu, natumai mko salama.

Wakuu leo nimeamua kuwafichulia siri ya maisha yangu tangia 2017 mpaka leo 2020.

Leo hii wakuu nimetimiza miaka minne tangu nisitishe biashara ya kuhonga. Mwanzoni haikuwa rahisi sana wapenzi wangu kwenda na huu mfumo wangu wakupata penzi bila kuhonga. Ili nibidi niende nao taratibu mwisho walizoea.

Mbinu nilizo tumia. Moja nilianza kupunguza hela ya kuhonga kuanzia asilimia 90 mpaka asilimia 30 kwa kila mwezi. Taratibu nilifanya hivyo mpaka mwanzoni mwa mwaka 2018 nilikua nimeshapunguza mpaka asilimia Sufuri. Pili nilianza kupunguza kutoa ahadi mpaka mwisho nikaacha kabisa.

Tangia nisitishe hii biashara nimepata mafanikio yafuatayo.
1. Akili yangu imetulia marudufu

2. Nimefanikiwa kufanya uwekezaji ambao utaniletea faida baadaye.

3. Mwili umerudi, nimenenepa, navutia navaa vizuri na napendeza tofauti na mwanzo hili limepelekea watoto wengi mtaani kuvutiwa na mimi.

4. Nimekuwa na amani na furaha kuliko mwanzo ambapo mwanzo ilikuwa nikiwasha simu tu baby naomba hela ya saluni.

5. Wapenzi wangu wananyoa nywele zao na kupendeza vizuri ambapo wanaonekana ni wazuri zaidi kuliko kipindi walicho kuwa wanasuka marasta ya makatani na manywele ya uzi.

6. Nimefanikiwa kuwabadirisha wapenzi wangu wote waende na mfumo wangu wa ubahiri. Kwa hiyo huwa hawaniombi pesa na kila kitu wanajitegemea wenyewe.

6. Nimefanikiwa kugundua kuwa wanawake wanaweza kujitegemea wenyewe bila ya sisi maana nao wana mikono na miguu. Hawakuumbwa ili waje kuchoma tunavyo vitafuta.

7. Nimefanikiwa kugundua kuwa sisi ndio tuna waharibu wanawake kwa kuwazoesha vipesa ambapo wao hawana shida na pesa zetu. Wao wanachotaka ni upendo wa kweli sio pesa.

Wakuu kiukweli mafanikio ni mengi niliyo yapata. Sasa naishi raha msitarehe na papuchi zinaliwa kama kawaida.

Mwisho:
Ukikuta mwanamke anapenda kuhongwa hela ujue mwanamme wake wa kwanza alikuwa domo zege alimtongozea pesa.

Karibuni kwa maoni wakuu, sasa uwanja ni wenu.

Ushauri wenu wakina Jonah, Financial service na dada yetu cute love. Nini maoni yenu juu ya hili.
 
Umezungumzia kuhonga as if ni kitu cha lazima sana na hakikwepeki. Kuhonga ni uoga, kuhonga ni utumwa, kuhonga ni kununua mapenzi. Mtu anajiingiza kuhonga kwa kutojiamini. Kama kweli umetoka huko hongera sana!
 
Back
Top Bottom