Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda Marekani, hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi. Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu, nitaleta mrejesho.

Wasalaam.
Mkuu,unajua kwamba kwa kuweka hii taarifa hapa tayari unaweza kupoteza au kupata max zaidi katika usahili huo?
 
Mleta mada lazima utakuwa unatokea kulee kwa wale jamaa wenye kupenda misifa
 
Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda Marekani, hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi. Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu, nitaleta mrejesho.

Wasalaam.
Utafanikiwa kaka naamini Mungu atakufanikisha, Amen.
 
msalimie Snoop, mwambie ndugu zake huku matimira wanamsalimia, usisahau pia kumjulisha Babu yake Dr Remmy Ongala alishafariki kitambo.

Otherwise, sisi tupo tupo hapa shamba la bibi tunaijenga Tanzania yetu na ukirudi utaikuta zaidi ya Newyork.
 
Na watu wa viza wa embassy lazima wakulazimishe waone umekata ticket, wakati hata bado hawajafanya maamuzi ya kukupa viza, maana walivyo Wajinga wanakulazimisha kukata ticket alafu kwenye viza wanakupa refusal tena!!!

Sent from my TECNO KC8 using JamiiForums mobile app
Ni SAwa na Uhamiaji wanataka admissions ya chuo ndipo wakupe pasipoti, na chuo nao awakupi admissions bila pasipoti.
 
Salamu kwenu nyote.

Awali ya yote napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha tangu naanza hizi harakati hadi leo nimefika mwisho wake na kufanikiwa.

Pili, nawashukuru wachangiaji wote hapa JF walionipa support (kwa njia ya ushauri) kuhusu jinsi gani naweza kufanikisha adhma yangu, Mungu awabariki sana (kwenu nyote mnaoamini uwepo wake na utendaji kazi wake).

Binafsi nina furaha ya pekee sana, nimefanya interview na visa yangu ime be approved, kesho saa nane kamili mchana nitakwenda kuchukua tayari kwa kuanza maandalizi ya safari hivi karibuni.

Mwisho kabisa, nawashukuruni nyote mlioniombea, mlionikejeri na kunikatisha tamaa, mmenipa nguvu kwa namna moja ama nyingine.

Nimelizie kwa kuwakaribisha nyote mlio na mlengo kama wangu, kwa ushauri namna gani mnaweza fanikiwa pia.

Wabillah tawfiq.
 
msalimie Snoop, mwambie ndugu zake huku matimira wanamsalimia, usisahau pia kumjulisha Babu yake Dr Remmy Ongala alishafariki kitambo.

Otherwise, sisi tupo tupo hapa shamba la bibi tunaijenga Tanzania yetu na ukirudi utaikuta zaidi ya Newyork.
Sawa ahsante.
 
Back
Top Bottom