Leo nafanya interview Ubalozi wa Marekani kwa ajili ya viza

Invigilator

JF-Expert Member
Aug 16, 2016
3,207
5,990
Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda Marekani, hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi. Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu, nitaleta mrejesho.

Wasalaam.

Salamu kwenu nyote.

Awali ya yote napenda kumshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha tangu naanza hizi harakati hadi leo nimefika mwisho wake na kufanikiwa.

Pili, nawashukuru wachangiaji wote hapa JF walionipa support (kwa njia ya ushauri) kuhusu jinsi gani naweza kufanikisha adhma yangu, Mungu awabariki sana (kwenu nyote mnaoamini uwepo wake na utendaji kazi wake).

Binafsi nina furaha ya pekee sana, nimefanya interview na visa yangu ime be approved, kesho saa nane kamili mchana nitakwenda kuchukua tayari kwa kuanza maandalizi ya safari hivi karibuni.

Mwisho kabisa, nawashukuruni nyote mlioniombea, mlionikejeri na kunikatisha tamaa, mmenipa nguvu kwa namna moja ama nyingine.

Nimelizie kwa kuwakaribisha nyote mlio na mlengo kama wangu, kwa ushauri namna gani mnaweza fanikiwa pia.

Wabillah tawfiq.
 
Salamu wakuu,

Baada ya kuwa kimya kwa muda mrefu, nikihangaikia suala la kutoka huku nchini kwetu kwenda masomoni Marekani. Hatimaye leo ndio siku yenyewe ya kujua mbivu na mbichi.

Nitakuwa ubalozini kwa ajili ya visa interview saa tatu na dakika 45 asubuhi hii.

Namuomba sana Mwenyezi Mungu anifanikishe katika jambo hili, niombeni pia rafiki zangu. Nitaleta mrejesho.

Wasalaam.
Saa sita tunasubiri mrejesho.
 
Zamani waafrika walichukuliwa kwa nguvu kwenda utumwani siku hizi waafrika wanagombea wenyewe huku wakililia kwenda utumwani. Kama walivyokufa baharini enzi ya slave trade ndivyo wanavyokufa hata leo baharini pindi boti za wazamiaji zinapozamishwa majini.
 
Back
Top Bottom