Leo hii Marekani yajaribu kuteka meli ya mafuta ya Iran, Iran yaichukua meli yao kwa kutumia kikosi maalum cha Makomando katika pwani ya Oman

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,568
Kikosi cha IRGC cha Iran chazima uharamia wa jeshi la Marekani katika Bahari ya Oman

Nov 03, 2021 11:25 UTC
Kikosi cha IRGC cha Iran chazima uharamia wa jeshi la Marekani katika Bahari ya Oman

Operesheni makinii na iliyochukiwa wakati mwafaka na wanajeshi shupavu wa kikosi cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) imefanikiwa kuzima jaribio la uharamia na wizi wa mafuta uliosimamiwa na manuwari ya kijeshi ya Marekani katika maji ya Bahari ya Oman.

Televisheni ya al Alam imeripoti kuwa, mashujaa wa kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu wamezima jaribio la operesheni ya manuwari ya jeshi la Marekani iliyojaribu kuiba mafuta yaliyokuwa yamepakiwa katika meli ya mafuta ya Iran.

Manuwari hiyo ya jeshi la Marekani ilipora na kuchukua meli iliyokuwa imesheheni mafuta ya Iran katika Bahari ya Oman na kupakua mafuta yake na kisha kuyapakia katika meli nyingine na kuielekeza kusikojulikana.

Hata hivyo, kikosi cha anga cha Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) kilitekeleza operesheni kinzani na kushusha wapiganaji wa kikosi hicho juu ya meli hiyo na kuitwaa na baadaye kuilekeza kwenye maji ya Iran.

Jeshi la Marekani viliifuata meli hiyo kwa kutumia helikopta na meli kadhaa za kivita, lakini limeshindwa kutokana na kuingia nguvu kubwa zaidi ya vikosi vya IRGC.

Baada ya hapo, jeshi la Marekani liliifuata meli hiyo ya mafuta kwa kutumia helikopta kadhaa na meli za kivita, lakini jaribio hili pia lilishindwa kutokana na azma kubwa ya la Walinzi wa Mapinduzi.

Jitihada kubwa za askari wa Marekani za kujaribu kusimamisha na kuzuia meli hiyo zimefeli na kwa sasa shehena ya mafuta iiliyokuwa imeporwa na askari wa Marekani iko katika maji ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

IMG_20211103_162554.jpg
IMG_20211103_161847.jpg
IMG_20211103_162621.jpg
IMG_20211103_161826.jpg
IMG_20211103_161759.jpg
 
Siwaelewi hawa watu....wataanza kukimbilia marekani..wakilia lia viwanja vya ndege wapelekwe marekani... Sijaona mantiki unachoshangilia
 
Unacheza na waajemi wa namtumbo...! Hapo anamaniisha kitu kingine kabisa. Maana yake jeshi lake la Iran ya mtogoro lina uwezo kuliko la marekani
Umechangia kama beki 3 na sio great thinker,umechangia kishabiki utafikiri upo New york,kumbe upo kwenu huko Namtumbo unapiga miayo tu na kuumwa na Mbu wa malaria.
 
Umechangia kama beki 3 na sio great thinker,umechangia kishabiki utafikiri upo New york,kumbe upo kwenu huko Namtumbo unapiga miayo tu na kuumwa na Mbu wa malaria.
Sawa black-mwaajemi wa kwa mtogole. Umefuga na ndevu ujifananishe na wao. Nilijua utakuwa wa kwanza kwanza pale juu. Vipi vikitokea vipigo huko kwenu wenyewe kwa wenyewe,mnaanza tena kung'ang'aniana ndege kwenda U.S.A?
 
Back
Top Bottom