273
Member
- Sep 12, 2017
- 63
- 82
Salam zenu wakuu,
Kama kichwa kinavyojieleza,
Ndugu zangu nimefikia uamuzi huu kutokana na ushauri mfupi na mzito kutoka kwa kaka yangu na pia kwa kuwa naona nafsi inamsuta sana.
Niseme tu nimeamua kuchana na pombe kutokana na sababu zifuatazo;
1. Ni kinyume na mafundisho ya kiimani.
2. Tangu nianze kunywa huu ni mwaka wa 5 sioni faida yoyote zaidi ya hasara kama za kupoteza simu, kupoteza pesa, kupoteza heshima, kupoteza baadhi wa watu wa msingi na sana sana kupoteza utu wangu.
3. Natokea familia ya kimasikini sana hivyo naona kuendelea kunywa pombe na kama naisaliti familia yangu.
4. Nimetathmini kuwa kuendelea kunywa pombe ni kuisaliti nafsi yangu, kumsaliti "my future wife" na pia kuwasaliti wanangu ambao bado wapo kiunoni mwangu (nitapoteza sifa mojawapo ya kuwa baba bora)
Kiufupi sioni faida za kuendelea kunywa pombe, naacha kunywa pombe rasmi hivyo ndgu zngu naomba mnikumbuke ktk sala.
Zaidi zaidi nipo mbioni kuachana na anasa nyingine ya kupenda wanawake, changamoto kubwa ktk hili ni kuwa sijawahi kukutana na mwanamke aliye commited(naweza kumpenda kwa dhati ila akaja kunitenda baadae) hivyo nakua sipo commited to a girl i be with, ila naamini yupo mmoja nilieandaliwa na Mungu na nitakutana nae tu naamini katika kipindi kifupi kijacho tujenge maisha.
Kwaheri pombe niilikupenda sana sana tena sana lakini mahala salama pamenipenda zaidi.