Lengo langu si kukuchezea....

lizzy hasira za nini tena,siko peke yangu wako wengi wanaofanya hivyo mimi nimeamua ku-share tu.tatizo lenu mnapenda kuuliza, Una mpango gani na mimi?sasa jamaa kashakuzimia badala kumkubalia na kumpa mapenzi matamu yatakayomfanya a-stay wewe unarukia kwenye conclusion oo utanioa au unataka kunchezea?
Alafu we lizzy na ukali wako huo ntakukomesha kwa kutumia mashangazi lazima uachie tu!!!(kama hujaolewa lakini)

mnawafanya mafungu ya nyanya, mkifunua mnafunika, mnawaumiza mtima
 
mnajua? mtu ajionavyo yuko, anadhani na wengine wapo kama yeye na wao wanaona sawa tu kwao kuwa na tabia za kishen*i. na hawajali kama haya yanaweza kuwatokea hata wao ndani ya familia zao. inachukiza sana kuharibiwa waliotulia.

nyie kina mkwaruzo ndio hatari zaidi 'silent kilazz'mnajidai wapoole kumbe ni balaa kubwa.
 
Ndivyo kwa mabinti wengi, lakini hapo utatafuta laana tu, kwanini uibue mapenzi kwa mtu unaejua huna mpango nae. kanunue wanao jiuza.
 
hahaaaaaaaaaa umenikumbusha mbali kuna siku moja nikakutana na mwanaume mwenyewe acha amwage sifa huyo nyingine unagundua kabisa unauziwa mbuzi kwenye gunia.

ushauri wangu kama huna nia na mtu usicheze hisia zake kuna watu wengi tu wanatoa huduma bure bila vigezo na masharti
 
KWeli we ni kipindupindua!!Kwahiyo mtu akikuuliza una malengo gani nae unashindwa nini kumwambia mwenyewe hujui unachotaka na huko mbeleni kila mmoja akipendezwa na mwenzake mnaweza kua zaidi ya wapenzi!?Acha kupinduapindua watoto wa watu!Alafu mashangazi zangu tu wamenishindwa hao unaowatuma wa kazi gani?
 
Nimefanya kautafiti kadogo na kugundua ukitaka 'kumlamba' binti mrembo aliyeshika dini basi mwambie ''lengo langu si kukuchezea na mungu akipenda tuta....halafu hapa unaanzisha kikohozi cha ghafla basi utaona mtoto kainuka na kukushika bega huku akikupa pole nyiiingi,ukiona hivyo ujue kimeshaeleweka hapo.

Hii imekaaje ?

tushawastukia.
Maujanja yenu yote tunayajua.
 
lakini kama kweli aisee... Hawa watu bila uongo utaishia kula kwa macho.
 
Na ole wao siku ikifika watalia na kusaga meno!
watu kama nyie ndio ambao mnaomghathibisha Mungu!! baada ya kumtia mtu moyo asonge mbele shetani anawatumia kuwarudisha nyuma!! imeandikwa kipimo upimiacho ndicho utakachopiwa!!

ole wako!!!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom