Lengo la Zitto ni kupata wafuasi toka UKAWA

Emc2

JF-Expert Member
Sep 26, 2011
16,808
16,873
Zitto anajaribu kuzichanga sana. Lakini wale wenye jicho la tatu tumeona.

Kwa kuwa UKAWA wapo na namna yao ya vipi wafanye siasa. Zitto anajifanya yupo pamoja nao na huku akijitahidi sana kupaza sauti kwa guvu ili aonekane yeye.

Ukiangalia kwa juu juu utadhani kuwa zitto anashindana na Rais lakini ukiangalia kwa jicho la tatu utagundua zitto anataka kujipatia wafuasi wa haraka kutoka Ukawa. Wapo wengi sana ambao bado hawajajua waende wapi. Kwa hiyo anatafuta kwa nguvu aaminike ili apate wafuasi wengi.

Kwa hiyo hapa ni kati ya Ukawa na Zitto nani mjanja.
anajitahidi sana ateke vijana kwenye mitandao ili apate mbegu na aweze kusonga mbele.

Na katika hili amefanikiwa kwa kiasi kikubwa. Yaani walipokuwa wanatoka dodoma alivyoandaa mapokezi wangekosea tu wakakubaliana naye basi ange kuwa amewaingiza kingi.

Zitto anawatafuta Ukawa waingie kingi na atawatumia wakija kushituka tayari amepata watu.

Ni juu yenu sasa kuamua kusuka au kunyoa.
 
Zitto yupo makini sana. Anajua anachokifanya. Mwaka 2025 chama chake kinaweza kuwa chama kikuu cha upinzani. Huku ukawa wakipoteana.
 
Zitto
Zitto yupo makini sana. Anajua anachokifanya. Mwaka 2025 chama chake kinaweza kuwa chama kikuu cha upinzani. Huku ukawa wakipoteana.
Zitto yupo makini sana ni mwanasiasa mbunifu hazuiliki zitto yuko juu level moja na kina raila odinga
 
Daaah!! Umeibuka na hii ID Leo kulikoni?

Mimi nakubaiana na wewe kabisa, na amekuwa wa kwanza kwa kila issue inayohusu upinzani, ila UKAWA wanatakiwa wawe makini kwani huyu jamaa sio wakuaminika hata kidogo, ni ndumilakuwili, na inawezekana anatumika kuzuia hoja za UKAWA, kwa mfano alikuwa wa kwanza kuandaa mikutano baada ya ukawa kufungiwa, na serikali ilipokataza ikajumuisha pamoja na ukawa. Hivyo inawezekana anatutangulia ili iwe rahisi kwa serikali kukataza jambo ambalo lingefanywa na UKAWA.
 
Anguko kuu la ukawa lazima, profesa kesha rudi cuf wanajitoa kwenye ukawa.chadema hawawezi kusimama peke yao, kuna mgogoro mkubwa wa madaraka unakuja... hivi vyama vitabaki na wafuasi wachache sana kwa upande mwingine mpinzani wa kweli act wazalendo ndio kitabaki katika kukidhi kiu ya watanzania wazalendo.
 
Mimi nakubaiana na wewe kabisa, na amekuwa wa kwanza kwa kila issue inayohusu upinzani, ila UKAWA wanatakiwa wawe makini kwani huyu jamaa sio wakuaminika hata kidogo, ni ndumilakuwili, na inawezekana anatumika kuzuia hoja za UKAWA, kwa mfano alikuwa wa kwanza kuandaa mikutano baada ya ukawa kufungiwa, na serikali ilipokataza ikajumuisha pamoja na ukawa. Hivyo inawezekana anatutangulia ili iwe rahisi kwa serikali kukataza jambo ambalo lingefanywa na UKAWA.
Umenifurahisha kamanda,badala ya kuwaambia ukawa kuwa makini na ccm,unawaambia wawe makini na zitto,kajimbo kamoja tu kanakutetemesha,mna safari ndefu sana kuipata ikulu
 
Umenifurahisha kamanda,badala ya kuwaambia ukawa kuwa makini na ccm,unawaambia wawe makini na zitto,kajimbo kamoja tu kanakutetemesha,mna safari ndefu sana kuipata ikulu
Umeshindwa kumtambu ccm mwenzako? Hatakama hamjuani huwezi kugundua huo uandishi wake wa kinafiki? Na nani wanaandika unafiki kama sio ccm wenzako?
 
Akikaa kimya anatumikq na ccm.

Akipambana na ccm aangaliwe atavuruga ukawa.

Akijitenga na ukawa msaliti.

Sasa ni lini mtaacha kumhofia Zitto?
Na kwa mantiki hiyo ni ngumu saana kujua nani anayeongea nini anasimamia kundi gani. Wapo wa CCM, CHADEMA, CUF na UKAWA na pengine ACT Wazalendo. Jiamini wewe na upande unaousimamia.
 
Mimi ni nonpartisan lakini obviously mleta mada ni mfuasi wa CCM. This is purely a classical propaganda !!
 
Kazi kubwa inayofa ywa Na wanaoanzisha thiredi ni kujitahidi kugawa ukawa ,,imeshindikana !! Anayeota kubaki Na chadema wabachama wachache hajui
 
Back
Top Bottom