Lengo la CCM kung'ang'ania umeya wa DSM ni nini , kuleta maendeleo au kulinda ufisadi ?

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
127,936
244,517
Wadau wengi wanajiuliza kisa cha wasomi wa nchi hii kujitoa akili na kufanya njama ili kuvuruga uchaguzi wa Meya ni nini ?

Hivi watu walioshindwa kuleta maendeleo kwa miaka 60 wataweza vipi katika kipindi kifupi cha miaka mitano ?

Ama lengo lao ni kuhakikisha ufisadi katika zabuni za jiji ( ikiwemo UDA ) vinalindwa na kufichwa kwa udi na uvumba ?

Kwa maoni yangu na hata kwa ukweli kutoka tume ya uchaguzi ccm ilishindwa vibaya sana uchaguzi jijini DSM , hivyo inalazimika ama ilazimishwe kukabidhi madaraka kwa washindi , vinginevyo itaabika vibaya sana !

wadau karibuni tujadili .
 
kura ni siri ya mtu, wingi wa wanachama siyo jibu la ushindi, cha msingi asimamishwe mgombea anayekubalika kwa wapiga kura, otherwise we will continue making noise .
 
kura ni siri ya mtu, wingi wa wanachama siyo jibu la ushindi, cha msingi asimamishwe mgombea anayekubalika kwa wapiga kura, otherwise we will continue making noise .

Sio kweli. Kila mara unapofanyika uchaguzi na ikaonekana ccm kushinda kwa mauzauza mlikuwa mkitumia kigezo cha wingi. Na mlipoona ni shida mliiamua kufanya kura za wazi, leo nini kimewasibu?
 
Watu waliokula hadi mishara ya mgambo ndio kuna kuleta maendeleo hapa kuna uchafu mwingi hapo ndio maana hawataki kupaachia ufisadi Wa jiji la dar utakuwa mkubwa sana
 
Maendeleo wameshindwa kuleta miaka 55 walete leo. Ni kulinda ufisadi.

Either Magufuli mwenyewe ni msanii au mawaziri wake ni wasanii maana sijaona mabadiliko yoyote serikali za mitaa
 
tatizo la ukawa munaishi kwa hofu, unyasi ukikugusa unahisi nyoka. uchaguzi wa umeya kwa taarifa yako wanachama wenu hawaoni cha kupoteza kwani wanaimani na chama tawala. Yeyote atakayechaguliwa ndiye mwakilishi wa kweli maana akienda tofauti na kasi hii atawajibishwa ifikapo 2020. Tunahitaji maendeleo sio maneno kwenye mabango
 
Watu waliokula hadi mishara ya mgambo ndio kuna kuleta maendeleo hapa kuna uchafu mwingi hapo ndio maana hawataki kupaachia ufisadi Wa jiji la dar utakuwa mkubwa sana
hii habari ya kutafuna mishahara ya mgambo lazima imtokee puani aliyekuwa meya wa ilala na timu yake , unajua nilikuwa nashangaa kwanini mgambo wote wa jiji wanaishi keko mwanga , shida ni hela .
 
Maendeleo wameshindwa kuleta miaka 55 walete leo. Ni kulinda ufisadi.

Either Magufuli mwenyewe ni msanii au mawaziri wake ni wasanii maana sijaona mabadiliko yoyote serikali za mitaa
dhuluma ya umeya wa jiji ina baraka za kila mwanaccm .
 
Back
Top Bottom