Lengai Ole Sabaya kachukua tabia ya Baba yake

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
10,840
2,000
Maandiko yanasema muuaji na mtesaji kwa watu wasio na hatia damu hizo zitawalilia mpaka kizazi cha nne, Sabaya ni kizazi cha kwanza cha utesaji akirithi kwa Baba yake.

Ole Sabaya kakulia Serengeti kwetu wakati Baba yake Thomas Ole Sabaya akiwa DC wa Serengeti. DC mkatili kuwahi kutoea .

Babake aliumiza Watu wengi sana, Mtoto kafuata nyayo za babake. Baba yake aliwahi kuchoma Nyumba za Wananchi wa Kijiji cha Nyamuma akidai wamejenga hifadhini na ni Raia wa Kenya.

Baada ya kuzichoma huku wengine wakifia humo aliwasomba na magari kuwapeleka mpakani na kuwabwaga huko akidai si watanzania! Serikali ya Kenya ikawakataa na kuwapa masaa waondoke upande wa Kenya maana haiwatambui.

Alifikishwa Tume ya Haki za Binadamu ambapo alitiwa "hatiani" na kuamriwa Serikali iwalipe fidia Milioni 800 na kuwarejesha maeneo yao.

Tume ya Haki za Binadamu ikamfungulia mashtaka Mahakama Kuu lakini mpaka leo Jaji wa kusikiliza kesi hiyo hajapangwa! Imagine tangu utawala wa Mkapa mpaka leo?

Akahamishiwa Songea akampiga makofi Katibu Tarafa kwa kushindwa kusimamia ujenzi wa Sekondari za Kata, Katibu Tarafa akamkaba zikapigwa hadi OCD alipoamulia ugomvi.

Akafikishwa Kamati ya Maadili ya CCM akatiwa hatiani kwa kosa la kupigana hadharani, baadae Jakaya Kikwete katika badilisha badilisha ya Ma-DC akamtupia virago.

Ikumbukwe kabla ya kuwa DC Serengeti alikuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Arumeru ambako Wananchi walimkataa wakaandamana wakachoma Nyumba yake kwa kupandisha kodi ya maendeleo ( kichwa) kutoka 3000 mpaka 5000 bila kushirikisha mtu.

Akajiuzulu, Fredrick Sumaye akiwa Waziri Mkuu akampa pande la U-DC ( Yeye na Sumaye wameoa Mji mmoja)
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
5,815
2,000
Sabaya pale Ikizu sekondar alikuwa na kikundi cha wanyanyua vyuma , aisee majamaa walikuwa wa mwisho kuingia dinning na hamruhusiwi Kula mpak hcho kikundi kiingie dining , alishawah mgeuza taya jamaa yangu wakifanya mazoezi ya ku-nfu uwanja wa Mpira shule usku , kundi la Sabaya bila Shaka ndo walikuwa architecture wa shule ya Ikizu kuchomwa Moto mwaka 2006 mi nikiwa form one jamaa akiwa form four .....

Baada ya shule kuchomwa Baba yake akiwa mkuu wa wilaya ya Serengeti alitia timu Kesho yake na defender za kutosha na kutimua wanafunzi wote with in 24 hrs ...
Sabaya alikuwa mbabe zaidi ya maelezo .... Ila ana dada yake mzur kinyama daaah 😋
 

mama D

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
13,488
2,000
"...nawapatiliza wana uovu wa baba zao; hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao" - Torati

Sio kwa Sabaya pekee ni kwa kila afanyae machukizo.... imagine wewe unafanya malipizi ya uovu wa babu yake baba yako, unalipia ya babu yako, ya baba yako halafu bado na wewe unaongeza yako😅😅😅
 

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
5,233
2,000
Kwenye Katiba Kuwe Na Kipengele Kuwa Kiongozi Yoyote Anapotolewa/Kusimamishwa Madarakani Kutokana Na Mapungufu/Makosa Fulani Fulani,Basi Katiba Iseme Hatakiwi/Hastahili Kuwa Kiongozi Tena For The Rest Of His/Her Life, Au Hata Kwa Kipindi Cha 30-50yrs. Awe Tu Mwananchi Wa kawaida.
 

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
34,025
2,000
Baba yake alikuwa mtu bomba sana labda useme babu mzaa mama kwani amekulia Hai kuliko huko serengeti.
 

Nyamatare1987

JF-Expert Member
Mar 29, 2021
268
500
Sabaya pale Ikizu sekondar alikuwa na kikundi cha wanyanyua vyuma , aisee majamaa walikuwa wa mwisho kuingia dinning na hamruhusiwi Kula mpak hcho kikundi kiingie dining , alishawah mgeuza taya jamaa yangu wakifanya mazoezi ya ku-nfu uwanja wa Mpira shule usku , kundi la Sabaya bila Shaka ndo walikuwa architecture wa shule ya Ikizu kuchomwa Moto mwaka 2006 mi nikiwa form one jamaa akiwa form four .....

Baada ya shule kuchomwa Baba yake akiwa mkuu wa wilaya ya Serengeti alitia timu Kesho yake na defender za kutosha na kutimua wanafunzi wote with in 24 hrs ...
Sabaya alikuwa mbabe zaidi ya maelezo .... Ila ana dada yake mzur kinyama daaah 😋
Baba yake alikuwa mkuu wa wilaya ya Serengeti akaja mission bukama Ikizu wilaya ya Bunda,mbona kama umeongeza chumvi
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom