Lema: Tutapokea kigogo wa CCM

Lema: Tutapokea kigogo wa CCM

Nimeamini siasa ni mchezo mchafu, Lowasa alipopigwa chini kwa tuhuma za richmond, nilifurahi sana na kumwona mwakyembe ni shujaa. Kwa ufaham wangu nilijua kitakacho fuata ni jamaa kushtakiwa, cha ajabu hili halikufanyika, nilijaribu kuuliza watu weng kwnn huyu mtu hastakiwi? Ndipo jamaa moja mwaka 2009 alinijibu, tuhuma za richmond si za kweli bali jamaa kapigwa jiwe la mbali ili kumharibia ndoto zake za urais; kadri siku zinaposogea nusu nasadiki kuwa kauli hii huenda ina ukweli.

Mtanzania bwana!
afikirii yeye analishwa maneno tu na kuaminishwa
 
kama ni Lowasa ule usemi wetu sisi kina gogo la shamba kwamba,ccm ndio mwisho wake utatimia
 
na wewe comred laki si pesa karibu (UKAWA) tujenge nchi, sisi tulisha amia mapema maana ccm ina wenyewe sio ile ya mwalimu nyerere,

karibuni:
lizabon
mzee tupa tupa
mussa alani
tanta madiba
faiza fox
simiyu yetu
rich pol
big show

nyote mna karibishwa (UKAWA)

Naam Prince
 
NAMI NAOMBA NIWAKARIBISHE PIA,KWANI HATA NANYI SI WATHAMANI KWAO ""MTAKATWA TU""
chama kimeshapokwa !!
hao akina kinana,mangula
wameshafungwa midomo na
WAPOKAJI!
 
masikini chadema inakwenda kutekwa hiviiiviiiihiiiiivi mchana kweupe.....

Wacha watekwe.... na ikibidi kifutike kabisa...!!!

Baba na mama yangu kule kijijini hawajui hivi vyama... wao wanataka mabadiliko ya hali zao za maisha....
Wameishi na CCM miaka yote hiyo wameshindwa kupata nafuu.... Waonee huruma ..... japo hata kwa miaka 5 waone mfumo mpya wa uongozi ndani ya nchi yao...!!!
 
"Rafiki wa adui yako nae ni adui yako. Adui wa adui yako huyo ni rafiki yako"

"Tunapokuwa vitani, unaweza kumshinda adui yako kwa kumtumia mateka uliyemshika. Mateka huyo anaweza kutoa siri zote za kumjua adui yako, hivyo ikawa rahisi sana kumpiga na kumshinda adui."
 
Kwenye siasa hamna falsafa kama hii ya kwako... Siasa si ndoa hivyo kujiunga, kujitoa na kurudi kundini ni halali kabisa... Ujasiri wako tu!!!

Siasa ni principles za jinsi ya kutumikia wananchi.
Kama jana mkiwatukana leo mnawakaribisha ni kielekezo tosha cha oppurtunism na ulemavu wa sera na fikra katika vyama vyenu.
Huko wanaoabudiwa ni watu kuliko principles,
CCM wembe wa principles umewanyoa, wachukueni mfaudike nao, au kwa lugha nyingine wawafaidi na wawatumie vizuri.
 
we unafikiri MTU aliyeingia kwenye vikao vya kamati ya ulinzi Wa nchi atakosa siri mnzito kawa waziri mkuu Wa nchi atakosa siri mzito mwanachama Wa ccm Wa muda mrefu atakosa siri za serikali acha ushabiki
Kuna siri nzito bila kiapo???!
Hebu kuweni na kiasi cha kuzungumza au ndio likizo sasa watoto wote uhuru wa manyani?????
 
"Chadema kama kanisa, hatubagui mtu unaingia unatubu, unasamehewa tunaendelea kupigania wokovu wa nchi yetu" Hon. Msigwa. M4C for ever
 
Siasa ni principles za jinsi ya kutumikia wananchi.
Kama jana mkiwatukana leo mnawakaribisha ni kielekezo tosha cha oppurtunism na ulemavu wa sera na fikra katika vyama vyenu.
Huko wanaoabudiwa ni watu kuliko principles,
CCM wembe wa principles umewanyoa, wachukueni mfaudike nao, au kwa lugha nyingine wawafaidi na wawatumie vizuri.

Maneno ya mkosaji hayo
 
"Rafiki wa adui yako nae ni adui yako. Adui wa adui yako huyo ni rafiki yako"

"Tunapokuwa vitani, unaweza kumshinda adui yako kwa kumtumia mateka uliyemshika. Mateka huyo anaweza kutoa siri zote za kumjua adui yako, hivyo ikawa rahisi sana kumpiga na kumshinda adui."

Mkuu hapo nimekukubali. Mwenye akili ataelewa. Sisi yetu macho na masikio.....
 
Kama chadema wamefika hatua ya kumwalika lowasa kwenye chama chao, basi ni hatari. Kwa lugha nyingine wanamualika chenge, rostam na wengine wa aina hiyo! Watakuwa ni wapumbavu, binafsi nakatishwa tamaa na siasa za bongo hasa ninaposikia kuwa sasa lowasa ni mbeba bendera wa chadema. Sasa baada ya uchaguzi watatuambia kuwa wanapinga ufisadi?

nyie magamba huwa mnashangaza sana mnaisuport ccm ikiwa na magamba hao hamjawahi kuisuport cdm pamoja na kupinga ufisadi lakini mmesikia lowasa anakwenda cdm chupi zimeanza kubana sasa nani kakwambia akija chadema ataendeleza ufisadi wake
 
Kuna siri nzito bila kiapo???!
Hebu kuweni na kiasi cha kuzungumza au ndio likizo sasa watoto wote uhuru wa manyani?????

nimemueleza kuwa siri mzito anazo aache ushabiki siri za kiapo zipo na zisizo za kiapo zipo siri nyingi wewe unadhani mipango ya ufisadi wanakula kiapo cha kutunza siri vipo vingi ni vya siri kwa chama havihusishi serikali kila chama kinamikakati yake ya ushindi ya siri ni ya chama na siyo ya serikali unadhani aijui kiapo cha serikali ni kulinda vya serikali na ndio maana wana kuwa na ulinzi wanao ufahamu na wasio ufahamu kwa vyeo vyake ana siri nyingi za chama cha mapinduzi
 
Back
Top Bottom