babalao 2
JF-Expert Member
- Apr 6, 2012
- 5,425
- 3,300
MBUNGE wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema amesema kuwa Chama hicho kitakwenda kuwasha moto katika Mkoa wa Mtwara ili kuhakikisha gesi haitoki mkoani humo.
Katika hatua nyingine Lema alidai kuwa alivuliwa Ubunge kwa ajili ya kukataa dili la Rais Jakaya Kikwete la kumtaka kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache kutokana na kuzuiwa na Jeshi la Polisi huku wananchi waliofika kumsikiliza wakiwa wamekaa mbali na uwanja wakihofia huenda askari Polisi wangefika uwanjani hapo.
Watu walianza kusogea katikati ya uwanja baada ya Lema kuwasili uwanjani hapo ambapo wengi waliohudhuria mkutano huo walikuwa ni vijana.
Akihutubia katika mkutano huo katika Viwanja vya Barafu, Lema alisema kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hana mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa kufanyika kipindi cha Bunge.
Alisema kuwa Watanzania wanasema gesi ya Mtwara haitoki na Chadema watahakikisha kuwa wanahamasisha wananchi kuhakikisha gesi haitoki mkoani humo.
Alisema kuwa, sasa amerudi tena bungeni mpaka Mungu atakapopenda na si binadamu.
Alisema kuwa hata Rais Jakaya Kikwete akiendelea kuzimua watahakikisha kuwa wanamtoa madarakani kabla ya mwaka 2015. Alisema kuwa sasa wataanza kuiamsha Dodoma na watahakikisha katika kipindi cha Bunge wanatembelea karibu kata zote za Mkoa wa Dodoma.
"Nitaanza kuamsha Dodoma kwenye matawi niliyofungua ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Mipango na Chuo cha Madini na kila moja ana wajibu wa kutafuta ukombozi wake" alisema.
Hii ni kwa mujibu wa HabariLeo
Kwa nini bado polisi wanawatisha wakazi wananchi kusikiliza mikutano ya vyama vya upinzani? Na pia hao wakuu wa mikoa na wilaya wanadharaulika na jamii kila kukicha kutokana na maamuzi yao yasiyo na mbele wala nyuma kwa jamii tunaomba muelewe mnaongoza wananchi wa vyama vingi sio ccm pekee.
Kuhusu gesi naomba chadema hilo suala muwaelimishe tu wananchi na sio kwenda kuchochea vurugu tumieni busara ya hali ya juu tena kusubiri kwanza kama muafaka utashindikana ndipo mjitokeze.