Lema: Tutakwenda Mtwara kuwasha Moto!

Lema: Tutakwenda Mtwara kuwasha Moto!

Eeeh huyu mchagga kilaza anasema atahakikisha gesi haitoki mtwara! hii kaitoa wapi mbona mawazo yake yako tofauti na ya wana mtwara! mpelekeni elimu ya watu wazima huyu mchagga aache kuropoka na kudandia mambo asiyoyajua au albda anazungungumzia gesi ya wana arusha kama wanayo
Patamu hapo, akilii ni nywele kila moja ana zake ila inaonyesha wewe una upara
 
kweli siasa ni kazi duh...tusije kuwa kama kwa gadaffi
 
kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika Zito kabwe yuko jimboni mwake wakati wabunge wenzake wakiwa dodoma,na kuna taarifa kuwa anajiandaa kwa maamuzi magumu,ambayo yanahusishwa na mkutano wa cdm uliyomalizika juzi diamond jubilee

Maamuzi magumu ni kwa faida yake
 
Mshaachia magamba,kitu ndani ndo mnashtuka!!!
 
Hahahaha,UWONGO MWINGINE BAKIZA AKIBA,USIUMALIZE WOTE,KAZI NI KWAKO GODBLESS LEMA.
 
Gesi wacha isafirishwe kuja Dar na kutumika kwa maslahi ya taifa zima. Ila yapasa mchakato mzima uwe wazi kuanzia ujenzi wa bomba la kusafiria,ulipaji wa fidia kwa maeneo linamopita, fidia kwa wamiliki wa maeneo ambapo gesi itatoka na iwekwe wazi faida ya ziada kwa wakazi wanaozunguka mradi huu huko Mtwara na Lindi.
 
Huyu jamaa anapenda sana vurugu!!! Kwanini asiende kuwasha moto kwenye kiwanja cha kujenga hospitali alichokiandikisha jina lake?
 
Haya mabadiliko na kuamka kwa wana Mtwara hakujatokea kama mvua,CDM na vyama vingine vya kisiasa vimefanya kazi kubwa sana kuwaelimisha wananchi katika umiliki wa rasilimali zao.

Chadema haijawahi kuchochea vurugu hata siku moja,hatujawahi kuskia kiongozi wa CDM akiwa na silaha lkn tumeshawahi kuskia wabunge na viongozi wa Chama tawala wana silaha tena kwenye mikutano ya hadhara.

NI WAKATI WA MABADILIKO.
 
MBUNGE wa Arusha Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Godbless Lema amesema kuwa Chama hicho kitakwenda kuwasha moto katika Mkoa wa Mtwara ili kuhakikisha gesi haitoki mkoani humo.

Katika hatua nyingine Lema alidai kuwa alivuliwa Ubunge kwa ajili ya kukataa dili la Rais Jakaya Kikwete la kumtaka kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mkutano huo ulihudhuriwa na watu wachache kutokana na kuzuiwa na Jeshi la Polisi huku wananchi waliofika kumsikiliza wakiwa wamekaa mbali na uwanja wakihofia huenda askari Polisi wangefika uwanjani hapo.

Watu walianza kusogea katikati ya uwanja baada ya Lema kuwasili uwanjani hapo ambapo wengi waliohudhuria mkutano huo walikuwa ni vijana.

Akihutubia katika mkutano huo katika Viwanja vya Barafu, Lema alisema kuwa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma hana mamlaka ya kuzuia mikutano ya kisiasa kufanyika kipindi cha Bunge.

Alisema kuwa Watanzania wanasema gesi ya Mtwara haitoki na Chadema watahakikisha kuwa wanahamasisha wananchi kuhakikisha gesi haitoki mkoani humo.

Alisema kuwa, sasa amerudi tena bungeni mpaka Mungu atakapopenda na si binadamu.

Alisema kuwa hata Rais Jakaya Kikwete akiendelea kuzimua watahakikisha kuwa wanamtoa madarakani kabla ya mwaka 2015. Alisema kuwa sasa wataanza kuiamsha Dodoma na watahakikisha katika kipindi cha Bunge wanatembelea karibu kata zote za Mkoa wa Dodoma.

"Nitaanza kuamsha Dodoma kwenye matawi niliyofungua ikiwemo Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo cha Mipango na Chuo cha Madini na kila moja ana wajibu wa kutafuta ukombozi wake" alisema.


Hii ni kwa mujibu wa HabariLeo

Kwa nini bado polisi wanawatisha wakazi wananchi kusikiliza mikutano ya vyama vya upinzani? Na pia hao wakuu wa mikoa na wilaya wanadharaulika na jamii kila kukicha kutokana na maamuzi yao yasiyo na mbele wala nyuma kwa jamii tunaomba muelewe mnaongoza wananchi wa vyama vingi sio ccm pekee.

Kuhusu gesi naomba chadema hilo suala muwaelimishe tu wananchi na sio kwenda kuchochea vurugu tumieni busara ya hali ya juu tena kusubiri kwanza kama muafaka utashindikana ndipo mjitokeze.
kwenye gesi hawana influence yoyote watu wa magwanda. siko zote wamepinga magwanda hayakuwepo itakuwa sasa.
 
Eeeh huyu mchagga kilaza anasema atahakikisha gesi haitoki mtwara! hii kaitoa wapi mbona mawazo yake yako tofauti na ya wana mtwara! mpelekeni elimu ya watu wazima huyu mchagga aache kuropoka na kudandia mambo asiyoyajua au albda anazungungumzia gesi ya wana arusha kama wanayo
Ustadhi Karibu kwenye pilau la hitma hapa mbagala hakikisha unavaa lile Tineti lako na shanga za kuhesabu
 
Mbona TANZANITE iliyopo kwake inaibiwa miaka hadi miaka na yeye kakaa kama MBURULA tu, leo ndo ajifanye akawashe moto Mtwara? Hana lolote.
 
kwa hiyo hata wana mtwara wakijadiliana na serikali (jalia) wanamtwara wamekubali kwa hiyari yao kwamba gesi iende dar, ninyi (CHADEMA) Mtahakikisha mnatatoka Arusha hadi mtwara kuhakikisha mnavuruga maridhiano hayo? (sisemi gesi ni lazma iende dar lakn).

Betlehem nadhani suala hapa si CHADEMA, CCM, CUF wala chama chochote cha siasa. suala hapa ni maisha duni na yanayozidi kuwa duni ya watanzania. labda kama wewe ni mkaaji wa mjini tu, lakini kwa siye tunaokwenda vijijini mara kwa mara hoja za wanaMTWARA ni akisi ya wananchi wa maeneo mengi katika nchi yetu. watu wana malalamiko lukuki, bahati mbaya ni ya chini chini.

BTW hebu nikuulize. Je, Umesoma tamko la SHURA YA MAIMAMU MTWARA? Je Umesoma tamko la UMOJA WA MAKANISA YA KIPENTEKOSTE MTWARA? Je, Umesoma ujumbe katika MABANGO ya waandamanaji wa MTWARA? hivi tunajadili nini hapa? Mi nadhani suluhu ya mgogoro huu na mingine ni kwa SERIKALI kuweka wazi kila MKATABA inaoingia ili wananchi wajue tangu awali kama kuna maslahi kwa nchi au la. Tabia ya kuweka mikataba kuwa siri ya wachache nadhani ndiyo inayochochea kwa kiasi kikubwa KUKUA KWA UFISADI NCHINI. Nadhani tunahitaji busara beyond limit kurudisha nchi yetu kwenye umoja uliojengwa waasisi wa Taifa hili. Propaganda za kisiasa zimepitwa na wakati katika nyakati hizi za utandawazi.
 
Wewe ni mbulula, serkali hii haina kiwango cha kupewa naafasi ya maridhiano. Maslahi ya taifa yapi unazungumzia chini ya chama kilichojaa ufisadi..! Moto utawashwa kama kawaida, hakuna gesi kutoka Mtwara..! Acha nikupasulie yai, mradi huu wa gesi ni deal la kupata hela za uchaguzi 2015..!
i
Si sahihi kumuita mtu mbulula kwa kutoa maoni yake binafsi na ambayo wengine pia twayaunga mkono. Kamwe mgogoro hauwezi kutatua mgogoro mwingine kuna kila haja ya kutatua mambo kwa mijadala. Kauli hizi za cdm zinatufanya watu tuogope hiki chama.
 
i
si sahihi kumuita mtu mbulula kwa kutoa maoni yake binafsi na ambayo wengine pia twayaunga mkono. Kamwe mgogoro hauwezi kutatua mgogoro mwingine kuna kila haja ya kutatua mambo kwa mijadala. Kauli hizi za cdm zinatufanya watu tuogope hiki chama.

ukiogope we na nai au una nafsi 2
 
Naomba kufahamu Lema anamipango gani na jimbo lake na ni viipi ataitekeleza? Ni vizuri kama akiendelea na jitihada za kuliendeleza jimbo kwasasa baada ya kuwa nje kwa muda mrefu vinginevyo atahatarisha kiti chake 2015. Upinzani sio vurugu,
 
i
Si sahihi kumuita mtu mbulula kwa kutoa maoni yake binafsi na ambayo wengine pia twayaunga mkono. Kamwe mgogoro hauwezi kutatua mgogoro mwingine kuna kila haja ya kutatua mambo kwa mijadala. Kauli hizi za cdm zinatufanya watu tuogope hiki chama.
Kauli hizi zinamaanisha kuwa haki haiombwi bali inachukuliwa na enzi za ubabaishaji zimeisha, wametufanya kitu mbaya for over 50 years, enough is enough. It is a moment of making things happen at reasonable cost and it is today not tomoro. Ikiwa wewe umejaaliwa uoga endelea kuogopa, wana wa Ntwara tumesema gesi kwanza uhai baadaye
 
Back
Top Bottom