Lema na Sugu kesho nendeni bungeni

Lema na Sugu kesho nendeni bungeni

Leo makamanda wa ukweli katika Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wamefukuzwa Bungeni.

Kwa hiyo nawasihi makamanda wengine kama Lema na Sugu, kesho waende bungeni wakaongeze nguvu iliyopungua.

Sisi wananchi tuliyo wengi tunaamini Lema, Sugu wakienda bungeni wakishirikiana na makamanda wengine kama vile Wenje, Halima Mdee, Moses Machali, James Mbatia na kamanda mkuu wa kikosi chote cha UKAWA Freman Mbowe akikisheni hi sera ya gesi na mafuta haipitishi Bungeni kwa manufaa ya nchi.

Sidhani kama unajua unachokiandika.
 
Tangazo Tangazo Tangazo kutokana na ccm kuwafikuza wapinzani bungeni sasa nn kifanyike huko dodoma moja wanasheria wote kufungua kesi haraka sana mahakamani pia wabunge wote walio majimboni na wao waende bungeni wakaibane serikali na wabunge wa ccm na wagombea wa ukawa huko majimbo sasa waongeze speed ya mikutano na kuwaambia wananchi wasiwachague wabunge kutoka ccm popote hapa nchini tanzania ili tuitoe ccm madarakani mwaka huu tusidanganyike tena na ahadi hewa
 
hii nchi inaelekea kuanguka.maccm yanaitafuna mpaka mifupa

Mkuu maccm sasa hivi yanafanya ubaya wa mwisho kwani yanajua kuwa baada ya octobee hayana chao
 

Attachments

  • 1436082319962.jpg
    1436082319962.jpg
    39.2 KB · Views: 294
Wakienda kuleta vurugu wembe ni ule ule...wanakatwa posho na mishahara +kusimamishwa kushiriki vikao bungeni!

Kwa hiyo washaurini wakawe wapole!

Kati ya watu mbulula ni wewe yaani upo tayari kuona nchi inauzwa kisa kuipenda ccm?
 
Wabunge aina hio ccm ndio kwao, Kessy, Mlata, Lusinde ....endekeza list utajaza makapu 12.

Jah people,profesa maji marefu,nkamiia,raage,murjii,.....mwingine aendeleze
 
Ccm tunatakiwa tuwashugulikie mwaka huu wasiludi kabisa bungeni
 
watanzania ndio akili zetu zilipoishia hapo.. Kwahiyo wote wakifukuzwa then miswada maccm wakiipitisha itakuaje?? Tunawaona wabunge wetu wakipambana kule ndani, vipi sie huku nje mbona hatuonyeshi kujali??

Yaani mitanzania tunashindwa hata kujikusanya jumatatu tutie timu wizara ya nishati au ikulu sie tumekalia majungu kwenye mitandao.. No wonder ccm ikishinda kwa kishindo tena uchaguzi mkuu huu. Sijui tumelaaniwa na nani sisi..

haya watanzania andamana ulipo. Wa dar tukutane ikulu kesho saa 2 asubuhi, wa dodoma tukutane lango la bunge saa 2 kamili, wa mwanza, arusha, mbeya, tanga na miji mingine yote tukutane ofisi za wakuu wa mikoa kama wawakilishi wa rais, vivyo hivyo vilayani ili ujumbe wetu ufike
 
sehemu-ya-wabunge-wa-upinzani-620x308.jpg

baadhi ya wabunge wa ukawa waliotimuliwa bungeni, walipokuwa kwenye mvutano na askari wa bunge

wabunge 10 ukawa watimuliwa bungeni

posted by: dany tibason 9 hours ago 562 views


wabunge 10 wa kambi rasmi ya upinzani wanaounda umoja wa katiba ya wananchi (ukawa), wametimuliwa bungeni kile kilichoelezwa utomvu wa nidhamu na kudharau kiti cha spika. anaandika dany tibason … (endelea).
wabunge hao wametimuliwa baada ya kutiwa hatihani na kamati ya maadili, haki na madaraka ya bunge inayoongozwa na brigedia jenerali mstaafu hassan ngwilizi kwa madai ya kukiuka kanuni za bunge kwa kudharau amri halali ya spika wa bunge anna makinda.
kwa mujibu wa ngwilizi aliyesoma hukumu hiyo bungeni, wabunge wanne wamepata adhabu ya kutohudhuria vikao vyote vilivyosalia katika mkutano huu wa 20, wawili vikao vikao viwili na wengine watapata hukumu yao leo baada ya kusikilizwa na kamati hiyo.
Amesema waliofungiwa vikao vyote vilivyosalia na kutopata fursa ya kumshuhudia rais jakaya kikwete akivunja bunge julai tisa mwaka huu, waligoma kutoa utetezi wao, wakitaka wapate fursa ya kuja na mawakili wao kujitetea.
Brigedia ngwilizi aliwataja waliofungiwa vikao vyote vya mkutano huu wa 20 ni john mnyika (ubungo), paulin gekul, (viti maalum), tundu lissu (singida mashariki) felix mkosamali (muhambwe) na moses machali (kasulu mjini).
Waliofungiwa kuhudhuria vikao viwili ni peter msingwa (iringa mjini), mbarouk mohamed mbarouk (ole). Mwenyekiti huyo aliwataja watakapata adhabu baada ya kuhojiwa leo ni pamoja na joseph selasini (rombo), khalifa suleman khalifa (gando), rashid ali abdallal (tumbi)

akichangia hoja ya kuwafungia wabunge hao, mbunge wa karatu, mchungaji israel natse ambaye ni mmoja wa wajumbe wa kamati ya maadili, amesema walikubaliana kuwaruhusu watuhumiwa waje na mawakili wao kama walivyoomba, lakini ameshangazwa na hukumu iliyosomwa na ngwilizi amesema wabunge hao hawakujitetea, hivyo hawakutendewa haki.

mbunge wa chake chake, mussa haji kombo alihoji kwanini kamati hiyo imeamua kutoa adhabu jana wakati bado kuna watuhumiwa wanaopaswa kuhojiwa leo.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa bunge, lissu amesema watu wenye hatia siku zote ni waoga na bunge hili ni la watu waoga.
Amesema wabunge walioitwa kwenye kamati hawakujitetea kwani waliomba kuja na mawikili wao na ndio utaratibu na kanuni za bunge.
“kwenye kamati wote tulitaka tuje na mawakili wetu, ndani ya bunge hatukupata fursa ya kujitetea. Mnakumbuka hivi karibuni mbunge wetu, joseph mbilinyi, alipelekwa kwenye kamati hii, akaomba kwenda na wakili wake. Leo sisi tumepata adhabu hiyo bila kujitetea.” amesema lissu.
Lissu alirejea hoja ya aliyekuwa mbunge wa chadema, zitto kabwe kwamba mwaka 2007 alihukumiwa na kamati hiyo, alipata muda wa kujitetea kwenye kamati na ndani ya bunge, hivyo alishangazwa na adhabu waliyopata.
Mbunge huyo amesema wamepata adhabu hiyo ili kuwapisha wabunge wa ccm kupitisha miswada ya kuliibia gesi taifa, dhambi ambayo amesema wao hawako tayari kushiriki.
Akizungumzia kilichotokea asubuhi, lissu amesema wote waliosimama asubuhi wakati waziri wa nishati na madini akilazimisha kusoma miswada hiyo, walitaka kuomba mwongozo, utaratibu na kutoa taarifa, lakini spika makinda alikataa na ndio chanzo cha vurugu.
Juzi spika aliahirisha kikao cha 41 cha bunge, baada ya wabunge wa kambi rasmi ya upinzani inayoundwa na umoja wa katiba ya wananchi (ukawa), kupinga serikali kuleta miswada mitatu nyeti kwa hati ya dharula kwa madai kuwa wabunge hawajaisoma na wadau hawajapata muda zaidi wa kuijadili.
Miswada hiyo ambayo ni mwiba mchungu bungeni ni pamoja na muswada wa sheria ya petroli, muswada wa usimamizi wa mapato ya mafuta na gesi wa mwaka 2015 na muswada wa sheria ya uwazi na uwajibikaji katika taasisi za uchimbaji tanzania wa mwaka 2015.

najiuliza hivi wabumge wa ukawa wakikataa kutoka ama kurudi wote kwa pamoja bungeni watafanywa nini. Wale askari wa bunge hawawezi zuia watu 40 wassingie. Wakija ffu tayari attensio yote itaelekezwa kwenye fujo na sio mjadala na lengo litakuwa limefanikiwa kutojadili hoja hadi next bunge ambayo mimi by any standard naona ina logic na mshiko sana
 
Naunga mkono hoja Wabunge wote wa UKAWA warudi bungeni na wagome kutoka kama wataitwa FFU kuja kuwatoa waache waitwe maana hawa wahuni na mafisadi sasa wanazidi kuvuka mipaka ya kutuheshimu Watanzania. Na hata FFU wakija wagome na kwa akili yao fupi wanaweza kabisa kutoa virungu na kutumia ubabe kuwatoa Wabunge wa UKAWA.

najiuliza hivi wabumge wa ukawa wakikataa kutoka ama kurudi wote kwa pamoja bungeni watafanywa nini. Wale askari wa bunge hawawezi zuia watu 40 wassingie. Wakija ffu tayari attensio yote itaelekezwa kwenye fujo na sio mjadala na lengo litakuwa limefanikiwa kutojadili hoja hadi next bunge ambayo mimi by any standard naona ina logic na mshiko sana
 
Kesho moto kwanza ndio unaanza
 
Rutta unatumika vibaya lakini cku si nyingi utakuja kujuta.
 
Back
Top Bottom