sirluta
JF-Expert Member
- Nov 28, 2012
- 6,325
- 2,486
Wapiga kura wa Arusha Lema asiwadanganye eti mbunge akiwa wa CHADEMA, Meya akiwa wa CHADEMA na Madiwani wakiwa wa CHADEMA, ndo mtapata maendeleo! Hizi ni huruma za kutafuta kura. Ilani inayotekelezwa ni ilani ya CCM na siyo ya Chadema.
Lema ameanza kuwadharau madiwani wake kuwa wameshinda kwa hisani yake, hataweza kukaa nao chini wapange mipango ya maendeleo. Lema hawezi kuishawishi wala kuishauri serikali kama mbunge ili Arusha ipige hatua kutoka hapa ilipo. Alishashindwa kwa miaka mitano hata aongezewe miaka 40 hawezi kitu chochote.
Lema anakiri mwenyewe ana sifa ya kutukana viongozi akiwemo rais. Sasa atashirikiana nao vipi viongozi wa kitaifa ama mkoa kuitetea Arusha?
Pia upotoshaji kutoka kwa mgombea Lema umezidi. CCM haijaongoza jimbo la Arusha kwa miaka 50. Changanyeni na za kwenu. CCM yenyewe ni ya 1977 hata miaka 40 bado. Arusha ya 1995 ni tofauti na Arusha ya 2015 kwa mipaka ya jimbo. Kwahiyo kama mbunge wa 1990 Arusha ilikuwa ni pamoja na Ngaramtoni, na kwasasa hiyo Ngaramtoni ipo jimbo lingine, huwezi kuisema Arusha ya wakati ule na ya leo. Najua wenye vichwa vya kupepesa hawatanielewa lakini jihadharini na maneno mepesi kama tishu.