Lema: Lowassa, Sitta na Mwakyembe kuhamia CHADEMA

Lema: Lowassa, Sitta na Mwakyembe kuhamia CHADEMA

Huyo waziri mkuu wa zamani kama ni Edward Lowassa hapana kupokelewa! Lakini mbona JK 2005 aliomba kuingia Chadema kama angepigwa chini lakini Mungu akaisaidia Chadema kwa CCM kutompiga chini!!!
 
Watanzania tumekuwa vinara wa events na magwiji wa analysis, lakini upande wa ideas na execution (i.e job well done), am standing to be corrected but for sure we are real poor. Let us critically discuss for sure dhambi ya Lowasa isiyotakiwa toba ni ipi? Je, ni RICHMOND? kUJIUZULU UWAZIRI MKUU? UTAJIRI? Ama nini hasa? Tuongee kwa facts ni si hisia.

Mundali mimi nakubaliana sana na wewe kwamba hakuna dhambi isiyofaa kutubu, lakini mimi nawaona Watanzania hawako strategic kabisa kwasababu huenda Lowassa hakuhusika na hizi lawama na huenda anataka kuwataja wahusika kamili.

Kwanini asipewe mahali pa kuja kutolea hayo aliyonayo kama kweli anataka changes? Inatakiwa aseme wazi kwamba yeye hahusiki kwa lolote ila kilichotokea ni 1, 2, 3... Au akiri kwamba hatuwezi kujua anaweza kusema kuna aliyofanya lakini ameamua kubadili dini ili amtumikie Bwana kwa njia nyingine.

I believe He'll be of use in many ways ila haitakiwi yeye aimeze CDM, anatakiwa kumezwa na CDM na hilo mimi naamini linawezekana.
 
hizi PRO-PER- GANDA bwana, sasa kama mkutano ulikuwa wa hadhara mwandishi
ameshindwa nini kuweka Hayo majina hadharani wakati yalitamkwa Wazi??!!!

another upuuzi ndani ya JF!
 
Hbr nilizozinyaka kwa mtu wa karibu kbs na EL ni kwa hbr hii ni ya ukweli toka ndani ya nafsi yake EL.

Na anachotaka kufanya ni kutoa kutapika yote yaliyomfanya ajiuzuru uwaziri mkuu ile enzi yake na bila kusaha mambo ya epa & richmond ambayo imekuwa ikimgusa sana kwn karibu kila Mtanzania amekuwa akimwonyeshea kidole.
Mdau amesema kwmb ataweka wazi kila kitu wazi na ndipo atatua chama ajuae yeye na hajaweka wazi ni chama gani ataingia ila ataibwaga manyanga ccm muda wowote kuanzia mwezi ujao.

Tusubirie na tuangalie hii sinema itakavyokuwa kwani natarajia kuona hii kimbunga ikuchukua angalau kama siyo nyumba nzima lakini itachukua hata bati.
hizi hadithi tumezisikia sana kwamba lowassa ataeleza kila kitu miaka inasonga tuu ni ndoto za alinacha!!
 
Mundali mimi nakubaliana sana na wewe kwamba hakuna dhambi isiyofaa kutubu, lakini mimi nawaona Watanzania hawako strategic kabisa kwasababu huenda Lowassa hakuhusika na hizi lawama na huenda anataka kuwataja wahusika kamili. Kwanini asipewe mahali pa kuja kutolea hayo aliyonayo kama kweli anataka changes? Inatakiwa aseme wazi kwamba yeye hahusiki kwa lolote ila kilichotokea ni 1, 2, 3... Au akiri kwamba hatuwezi kujua anaweza kusema kuna aliyofanya lakini ameamua kubadili dini ili amtumikie Bwana kwa njia nyingine. I believe He'll be of use in many ways ila haitakiwi yeye aimeze CDM, anatakiwa kumezwa na CDM na hilo mimi naamini linawezekana.
Akiingia CDM pamoja na kueleza yote kwa ukweli na kutubu pale alipokosea kwa makovu aliyo nayo hatakiwi kupewa uongozi! sikumbuki vema kama kwenye ili list of shame ya mwembe yanga iliyotolewa na dr. slaa jina lake lipo au la!!kama lipo je litaondolewa kwenye hiyo list au itakuwaje??
 
Chonde chonde Kamanda Lema; hii spin sio nzuri, it is a bad joke, ungewaacha wafunguke wenyewe>
 
Ficha gamba, vaa gwanda.

Nduka umeona mbali. great mheshimiwa. naona sasa cdm tunakokwenda siko kuzuri. Lema usituambie vitu ambavyo havijatokea. visipotokea utapoteza utashi wa watu kukuamini na kukusikiliza. jembe tunakuamini sasa unapoanza ku pre empty stories ambazo hazijafanikiwa hatukuelewi. please stop this if at all you are the one threading us with the info. ache waje kwanza kisha ndo tuseme kitu. otherwise tuwe makini. M4C for ever
 
Siku zote kwenye vita silaha ya mwenzako ikiangukia mikononi mwako hauitupi ila unaificha ili adui yako asipate silaha ya kukuumiza nayo, la msingi sana ni wewe ujue namna ya kuitumia maana kama ni bomu ukiliweka vibaya litakulipukia. Ila kama unazifahamu silaha vyema una uwezo mkubwa wa kutumia hiyo hiyo silaha kumharibu mwenzako, usiitegemee sana silaha ya adui pia as it might fail on the way.

Akili mtindi !! ha ha ha ha!! very interesting name!
 
Mimi nadhani kama anataka kueleza yaliyo moyoni mwake kuhusu tuhuma dhidi yake ni bora akafanya hivyo mapema kuliko kuendelea kusubiri, haitakuwaja kuwa rahisi kutuaminisha hayo anayokusudia kuyasema ni bora akafanya hivyo sasa ili tujuwe kuwa yeye yupo upande wa wazalendo na siyo kwa sababu ccm wamemchoka ndiyo afanye visa. The earlier the better for him.

Vinginevyo utakuwa ulaghai na hoja zake hazitakuwa na nguvu.
 
Mpaka niskie kauli halisi toka kwao wenyewe
 
Tafadhari jf, tunakoelekea siko, tuwe makin na post zetu. Siku hizi jamii forum imekuwa kama kijiwe! Hiyo habar hiyo siyo ya kweli, lema hakutaja majina. Alichosema yeye ni waziri mkuu mstaafu+mawaziri, na waziri mkuu mstaafu sio lowasa peke yake, wapo na wengine. Pls mod ondoa hii thread.
 
Lema amewataja Ndg. Edward Ngoyai Lowassa, Ndg. Samweli Sitta na Ndg. Harisson George Mwakyembe kuwa ni kati ya vigogo walioomba kuhama kutoka CCM kuja CDM.

Source:
Nimehudhuiria mkutano wake wa jana!

Hii haiwezi kuwa reliable source. Kwa kuwa ulihudhuria na ulikuwa makini kufuatilia controversials zote ulitakiwa kurekodi kama alivyofanya yule aliyekuwa akifuatilia matusi ya LUSINDE ARumeru. Tunaomba video, na kama utakuwa hauna basi post hii ita qualify kuwa ni ya uzushi yenye lengo la kupunguzia watu credibility na hivyo post itaqualify kuitwa uzandiki na uchonganishi.

I am skeptical and stand by my words about the post until VIDEO evidence is provided.
 
Amewataja wapi? au sijaelewa kwa sababu kiswahili kinanisumbua kidogo?
 
Lowassa ni fisadi na ufisadi wake umeligharimu taifa kwa kiasi kikubwa. Hata akitema nyongo nyingi kiasi gani bado hasafishiki. Anahitaji kufungwa jela kwa ufisadi wake.

Labda akishatoka lupango akiwa hai akaja akatubu dhambi zake ndio ahamie CDM. Bila hivyo hafai kwa mbolea wala mbegu. Sitta naye ni fisadi sio kwa kiwango cha Lowassa lakini bado ni fisadi. Mwakyembe naye haeleweki wala haaminiki. Hamna yeyote kati ya hao watatu anayefaa.

Magamba yanayotakiwa kuvalishwa magwanda ni viongozi wa ngazi za chini - mabalozi, wenyeviti wa vijiji, madiwani nakuendelea. Hao ndio wataleta faida CDM.
 
Siri iliyopo katika majina hayo ni ipi au majina yalitajiwa ofisini kwa siri? Kama yalitajwa hadharani kwenye mkutano wa hadhara maana yake kila aliyehudhuria alisikia, siri hapa ni ipi?????????? Acha blaa blaa!!!!!!!!!!
 
Kumbe mtu yoyote akitaka kuamia Chadema lazima akaombe ruhusa kwa Lema?
 
Back
Top Bottom