Lema: Lowassa, Sitta na Mwakyembe kuhamia CHADEMA

Siasa ni mchezo wa ajabu sana, na inahitaji uelewa wa tofauti kuucheza. Kimaadili Lowassa hafai kabisa kuhamia CDM maana anajulikana sana kwa mambo mengi mabaya aliyohusishwa nayo, hata hivyo nitawauliza swali moja la msingi; mkiwa vitani Kamanda wa upande wa pili akijisalimisha kwenu mnamfanyaje? Mnamrudisha alikotoka au Mnamteka? Kwanini? Hili likitokea mara nyingi waliofanikiwa hutangaza sana kwenye media, kwanini?
 
Waanzilishi na wafadhili wa CCJ, Sitta na Mwakyembe. Wanaotaka kuhamia CDM, Sitta na Mwakyembe. CCM fukuza hawa wanafiki before it is too late.

...Katu haitawezekana Lowassa na Sita+Mwakyembe wote wakajiunga kwenye timu moja tena ili eti wawe 100% chini ya udhibiti wa Mbowe+Slaa kwa kila watakachokifanya kama anavyopelekeshwa leo Ndugu Magale Shibuda, hawa sio watu wa kumnyenyekea mtu, na hawataweza kunyenyekezwa ndani ya Chadema ambayo bado haina demokrasia pana....

...Pindi unapoona kundi la Lowassa limeanza kukikimbia CCM na kuelekea Chadema, hiyo ni dalili ya wazi kuwa Sitta na Mwakyembe wapo CCM to stay, na watakuwa waaminifu zaidi sasa kwa CCM kwa sababu hiyo...
 
CDM wanawinda ndege kwa kuwapigia kelele! Watafanikiwa kiasi gani?

Kwa mfano kuna potential person/politician (msafi tu kwa standard za Tz) anataka kujiunga na M4C, then zinakuja habari za watu kama hao waliotajwa kuwa na nia ya kujiunga na CDM il-hali wana tofautiana nao (3 gambas)....itakuwaje?

Kwanini CDM wasisubiri muda ufike na tukio lifanyike kisha ndio waanzie hapo? Unless it's a form of mind games, then this is avoidable blunder in making by CDM

.
 
Ben wewe unapinga EL asiingie CDM au unapinga wanaokubali aingie? Mimi nafikiri EL akija CDM atekwe kisha aseme kilichomtoa CCM akahamia CDM, kama kweli amegeuka ataweka kwenye public mambo ambayo hamkuyatarajia hata kidogo. Hilo litawaumiza sana CCM na nakuhakikishia watahangaika sana hili lisitokee kwa gharama yeyote, hakuna mtu yeyote duniani atakayeamini mambo ni shwari iwapo taarifa zitasambaa kwamba EL kahamia CDM hata kama hana cheo chochote. Maana yake duniani ni kwamba CCM inaenda kaburini ikiwa hai.
 
Hii ni kutoka Tanzania Daima

Lema ataja ‘wazito' wanaoenda CHADEMA
YUMO WAZIRI MKUU WA ZAMANI
na Stella Ibengwe, Sengerema
WAZIRI mkuu mmoja wa zamani na mawaziri wawili walioko madarakani, wametajwa kuwa miongoni mwa wazito walioko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioomba kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Aidha, mawaziri hao wanasubiri muda muafaka ufike waweze kutangaza rasmi kujiunga na chama hicho, kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa na mwenendo mzima wa uongozi na utendaji wa mambo unavyokwenda serikalini na ndani ya CCM, hususan suala la kuwalinda watu wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu.
Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbelss Lema aliwataja ‘wazito' hao, kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini Sengerema juzi, ambapo alisema hatua hiyo ni ishara wazi ya kuanguka kwa chama hicho.
Katika mkutano huo, uliofanyika katika viwanja vya Mnadani vilivyobatizwa jina la Uwanja wa Wenje, Lema pamoja na mbunge wa Nyamagana, Wenje walisema wananchi wengi wakiwemo baadhi ya viongozi wenye uchungu na taifa hili ndani ya CCM, hawafurahishwi na ubadhilifu wa mali za nchi, na kwamba hatua hiyo imewadidimiza Watanzania katika lindi kubwa la umasikini, kutokana na kubariki madini, wanyama, misitu, samaki na rasilimali nyinginezo kuuzwa nje ya nchi kwa maslahi ya vigogo wachache.
Katika mkutano huo ambao zaidi ya wanachama 100 wa CCM walijiunga na CHADEMA, wabunge hao waliishambulia serikali wakidai imekuwa kinara wa ombaomba duniani, wakati taifa lina rasilimali nyingi zinazotumiwa na wachache kufanya ziara za mara kwa mara ughaibuni.
Lema aliuambia umati huo wa watu kuwa kama walivyoamua kuchukua maamuzi mawaziri hao, nao wanatakiwa kuihukumu sasa CCM na serikali yake kwa kujiunga na CHADEMA, kwani kufanya hivyo ni kujiandaa na kile alichokisema ukombozi wa taifa mwaka 2015.
"CHADEMA tumejiandaa kuingia madarakani kwa kutumia nguvu ya umma. Ndiyo maana (akawataja mawaziri) wameomba kujiunga na CHADEMA ili tulisongeshe pamoja kwenda kuingia madarakani mwaka 2015.
"Lakini (akamtaja waziri mwingine) tumemkataa. Tunataka wachapa kazi na wenye mioyo ya kweli katika mapambano ya kupigania haki na kuondoa dhuluma kwa Watanzania," alisema Lema.
Awali, aliyekuwa Diwani wa CCM Kata ya Nyampulukano, Hamisi Mwagao Tabasamu, ambaye hivi karibuni alihamia CHADEMA, aliwaambia wananchi hao wa Sengerema kwamba, halmashauri ya wilaya hiyo imegubikwa na tuhuma za ufisadi, hivyo viongozi wawili waandamizi wanastahili kushtakiwa mahakamani.
"Halmashauri hii ya Sengerema kuna ufisadi mkubwa. Kuna fedha nyingi sana za miradi zimeliwa na ushahidi ninao, TAKUKURU kama mpo hapa na Usalama wa Taifa njooni mnikamate Jumatatu kama mnadhani ni uongo," alisema Tabasamu ambaye anadaiwa kuivuruga kabisa CCM wilayani Sengerema.
Alisema, anao ushahidi wa mamilioni ya fedha za miradi katika eneo la Bukala, zinazodaiwa kutafunwa kwa mgongo wa mafunzo jijini Mwanza, na kwamba wananchi wa Sengerema waanze kubadilika na kuikataa CCM kwani viongozi wake hawawasaidii katika kutatua kero zao za maji, afya, barabara na miradi ya maendeleo.
Kwa upande wake, Wenje aliwataka wananchi wa Sengerema kuhakikisha wanaanza kuikataa CCM mapema, kwani bila kufanya hivyo miaka michache watakuwa watumwa wa kupelekwa Ughaibuni kulima mashamba ya wakoloni.
"Wananchi wa Sengerema nawaambieni leo kwamba, viongozi wenu wa serikali wanauza kila kitu sasa. Twiga wanauzwa, tembo wanauzwa, misitu, madini navyo vinapigwa mnada kwa Wazungu," alisema.
Alisema, ufisadi, kukumbatia wawekezaji wa nje pamoja na mikataba mibovu ndiyo inayoiweka Tanzania katika hali ya umasikini kiasi kikubwa, huku akimtaja mbunge mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa), kwamba amepata utajiri mkubwa kuliko wa marais wawili wa zamani, Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.
Aliwaomba wananchi hao kushinikiza katiba mpya ijayo Tanzania iongozwe kwa mfumo wa majimbo kama ilivyo huko Bara la Ulaya, kwa madai kuwa utarudisha mamlaka na utawala kwa wananchi, kuliko ilivyo sasa ambapo viongozi wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wanawajibika kwa rais.
 
Pia nadhani ni muda muafaka CDM wawe na wasemaji rasmi kwa mambo rasmi.

Mimi sioni potentiality yoyote kwa hao magamba 3 kujiunga CDM. Kwa sababu tofauti, watatu hawa ni wahanga wa CCM-Kikwete. Inawezekana wanahamishia vita yao uwanja tofauti tu. Inawezekana sio kwamba ni wazalendo au wameamua kuachana na udhalimu wa CCM bali wana-explore new ventures in political spheres justs as Shibuda.
 
kwani tatizo liko wapi,Lowasa akisema ukweli wa siri zote za richmond kwanini asipokelewe

Huyu Mh. ana madoa mengi mno hata kama akisafishika na richmond bado ataendelea kua mchafu. Hatuwezi tukapuuza kauli za baba wa taifa kwa sababu ya pesa. Baba wa taifa hili amewahi kutamka waziwazi kua huyu mtu hafai na kama mkifanya kosa kumpkea mtaona matokeo yake.
 
Hivi ina maana siku zote watu wa Chadema mnasema EL ni fisadi kwa kuwa tu yuko CCM? Mnamaanisha EL akihamia Chadema basi ufisadi manaomtuhumu unabaki CCM?

Ndio maana sipendi siasa na kazi za kisiasa.

he he tengeneza hela peleka watoto shule nzuri..hizi siasa hazina maana kama wewe hauko ndani yake au haufaidiki nazo
 
Mbona mleta mada hajamtaja huyo mtu (Kigogo) ambaye kakataliwa na CHADEMA?
 
Pia nadhani ni muda muafaka CDM wawe na wasemaji rasmi kwa mambo rasmi.

Mimi sioni potentiality yoyote kwa hao magamba 3 kujiunga CDM. Kwa sababu tofauti, watatu hawa ni wahanga wa CCM-Kikwete. Inawezekana wanahamishia vita yao uwanja tofauti tu. Inawezekana sio kwamba ni wazalendo au wameamua kuachana na udhalimu wa CCM bali wana-explore new ventures in political spheres justs as Shibuda.

Siku zote kwenye vita silaha ya mwenzako ikiangukia mikononi mwako hauitupi ila unaificha ili adui yako asipate silaha ya kukuumiza nayo, la msingi sana ni wewe ujue namna ya kuitumia maana kama ni bomu ukiliweka vibaya litakulipukia. Ila kama unazifahamu silaha vyema una uwezo mkubwa wa kutumia hiyo hiyo silaha kumharibu mwenzako, usiitegemee sana silaha ya adui pia as it might fail on the way.
 
Lema amewataja Ndg. Edward Ngoyai Lowassa, Ndg. Samweli Sitta na Ndg. Harisson George Mwakyembe kuwa ni kati ya vigogo walioomba kuhama kutoka CCM kuja CDM.

Source:
Nimehudhuiria mkutano wake wa jana!

hii kama ni kweli ni sita, Dr mwaky basi waziri mkuu mstaafu atakua ni Fred S. na siyo EL
 
Hivi ina maana siku zote watu wa Chadema mnasema EL ni fisadi kwa kuwa tu yuko CCM? Mnamaanisha EL akihamia Chadema basi ufisadi manaomtuhumu unabaki CCM?

Ndio maana sipendi siasa na kazi za kisiasa.
watu mnavichwa vigumu sana humu tunakuambia ufisadi ndani ya ccm ni mfumo,
wakibadili mfumo ccm kitakuwa safi!
 
• YUMO WAZIRI MKUU WA ZAMANI

na Stella Ibengwe, Sengerema
WAZIRI mkuu mmoja wa zamani na mawaziri wawili walioko madarakani, wametajwa kuwa miongoni mwa wazito walioko ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) walioomba kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Aidha, mawaziri hao wanasubiri muda muafaka ufike waweze kutangaza rasmi kujiunga na chama hicho, kutokana na kile kilichodaiwa kuchoshwa na mwenendo mzima wa uongozi na utendaji wa mambo unavyokwenda serikalini na ndani ya CCM, hususan suala la kuwalinda watu wanaotuhumiwa kwa ubadhilifu.

Mbunge wa zamani wa Arusha Mjini, Godbelss Lema aliwataja ‘wazito' hao, kwenye mkutano mkubwa wa hadhara uliofanyika mjini Sengerema juzi, ambapo alisema hatua hiyo ni ishara wazi ya kuanguka kwa chama hicho.

Katika mkutano huo, uliofanyika katika viwanja vya Mnadani vilivyobatizwa jina la Uwanja wa Wenje, Lema pamoja na mbunge wa Nyamagana, Wenje walisema wananchi wengi wakiwemo baadhi ya viongozi wenye uchungu na taifa hili ndani ya CCM, hawafurahishwi na ubadhilifu wa mali za nchi, na kwamba hatua hiyo imewadidimiza Watanzania katika lindi kubwa la umasikini, kutokana na kubariki madini, wanyama, misitu, samaki na rasilimali nyinginezo kuuzwa nje ya nchi kwa maslahi ya vigogo wachache.

Katika mkutano huo ambao zaidi ya wanachama 100 wa CCM walijiunga na CHADEMA, wabunge hao waliishambulia serikali wakidai imekuwa kinara wa ombaomba duniani, wakati taifa lina rasilimali nyingi zinazotumiwa na wachache kufanya ziara za mara kwa mara ughaibuni.

Lema aliuambia umati huo wa watu kuwa kama walivyoamua kuchukua maamuzi mawaziri hao, nao wanatakiwa kuihukumu sasa CCM na serikali yake kwa kujiunga na CHADEMA, kwani kufanya hivyo ni kujiandaa na kile alichokisema ukombozi wa taifa mwaka 2015.

"CHADEMA tumejiandaa kuingia madarakani kwa kutumia nguvu ya umma. Ndiyo maana (akawataja mawaziri) wameomba kujiunga na CHADEMA ili tulisongeshe pamoja kwenda kuingia madarakani mwaka 2015.

"Lakini (akamtaja waziri mwingine) tumemkataa. Tunataka wachapa kazi na wenye mioyo ya kweli katika mapambano ya kupigania haki na kuondoa dhuluma kwa Watanzania," alisema Lema.

Awali, aliyekuwa Diwani wa CCM Kata ya Nyampulukano, Hamisi Mwagao Tabasamu, ambaye hivi karibuni alihamia CHADEMA, aliwaambia wananchi hao wa Sengerema kwamba, halmashauri ya wilaya hiyo imegubikwa na tuhuma za ufisadi, hivyo viongozi wawili waandamizi wanastahili kushtakiwa mahakamani.

"Halmashauri hii ya Sengerema kuna ufisadi mkubwa. Kuna fedha nyingi sana za miradi zimeliwa na ushahidi ninao, TAKUKURU kama mpo hapa na Usalama wa Taifa njooni mnikamate Jumatatu kama mnadhani ni uongo," alisema Tabasamu ambaye anadaiwa kuivuruga kabisa CCM wilayani Sengerema.

Alisema, anao ushahidi wa mamilioni ya fedha za miradi katika eneo la Bukala, zinazodaiwa kutafunwa kwa mgongo wa mafunzo jijini Mwanza, na kwamba wananchi wa Sengerema waanze kubadilika na kuikataa CCM kwani viongozi wake hawawasaidii katika kutatua kero zao za maji, afya, barabara na miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Wenje aliwataka wananchi wa Sengerema kuhakikisha wanaanza kuikataa CCM mapema, kwani bila kufanya hivyo miaka michache watakuwa watumwa wa kupelekwa Ughaibuni kulima mashamba ya wakoloni.

"Wananchi wa Sengerema nawaambieni leo kwamba, viongozi wenu wa serikali wanauza kila kitu sasa. Twiga wanauzwa, tembo wanauzwa, misitu, madini navyo vinapigwa mnada kwa Wazungu," alisema.

Alisema, ufisadi, kukumbatia wawekezaji wa nje pamoja na mikataba mibovu ndiyo inayoiweka Tanzania katika hali ya umasikini kiasi kikubwa, huku akimtaja mbunge mmoja wa CCM (jina linahifadhiwa), kwamba amepata utajiri mkubwa kuliko wa marais wawili wa zamani, Baba wa Taifa, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi.

Aliwaomba wananchi hao kushinikiza katiba mpya ijayo Tanzania iongozwe kwa mfumo wa majimbo kama ilivyo huko Bara la Ulaya, kwa madai kuwa utarudisha mamlaka na utawala kwa wananchi, kuliko ilivyo sasa ambapo viongozi wakiwemo mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya wanawajibika kwa rais.

Hivi huu mkutano ndio uliomfanya Ngeleja asiende Jimboni kwake kupokelewa na Wananchi wake?

Sababu ni Mabango tu yalionekana...
 
Back
Top Bottom