Lema kwa hili umetu disappoint wakazi wa Arusha

Hivi kwanini baadh ya wanacdm mmeanza tabia za kimagamba ya kutokukubali kukubaliana,mwandika thread ana deserve kujibiwa na lema,kwa nn wengine mnabeza hiyo ni tabia ya kimagamba mnataka kila siku kusifiwa tu?sidhan kma kweli tunaitakia mema cdm hii tabia inajenga!wabunge wetu sio malaika na wanaitaji kukosolewa,kma kuna upupu achaneni nao najua kuna point kwenye alichoandika achaneni na habari za zidumu fikra.
You are right mkuu, Arusha haina Mbunge wa kuwatetea.
Lema amekaa kimagwanda zaidi, maandamano kwa kwenda mbele.Vita haijawahi kujenga-maafikianao ndo unampata maendeleo.
This is a warning shot, Lema asipowaridhisha wana Arusha kwa kile walichomchagua kuwatetea ili maendeleo yapatikane -this will be his last position.
Watu wanapenda u-ONE MAN SHOW,mbunge na madiwani wakiwa na umoja ndio mikakati ya maendeleo ya wananchi at grass roots yanapatikana.
Mtu ukiamua kupambana na serikali ya magamba, hukosi wapambe, lakini grassroots hizo hizo ndo zinaumia.
Lema ni kimagwanda zaidi-maandamano kwa kwenda mbele.
BREAKING NEWS : mpambe wa Lema mbaroni kwa ujambazi Arusha!!
 
Nafikiri Lema inambidi ajitambue kuwa yeye ni mjunge wa Arusha town na hivyo inampasa kupeleka malalamiko ya wanchi wake bungeni. Asifikirie kuwa yeye ni mbunge wa taifa zima.
 
Kwa hilo la umeme umechemka, sioni kwanini usifikirie kuwa wabunge walikaa akiwemo Lema unayemshutumu wakaamua kumtumia Wenje kuwakilisha kilio chao.

Si kweli kwamba walimtumia Wenje na kama amefanya hivyo ni sawa na kukwepa majukumu ya familia kwa kuomba baba mwingine kushughulikia matatizo ya familia. Kwa nini asingesimama kama yeye?
 
mnh.............mkuuu kwakweeeli huajeleweka,sijaona nguvu ya hoja.

Huwezi iona kwa sababu umepofushwa na ushabiki kuliko ukweli. Sometime inabidi tuwe wakweli kuepuka ushabiki na ndicho ninachofanya hapa. Lema anatakiwa ajue role yake kwetu sisi tuliomchagua
 
Mimi niko Arusha town na najaribu kufuatilia hali ya mji hizo hoja zako sioni kama zinaendana na hali halisi. Suala la umeme linasumbua nchi nzima hoja iliyotolewa na Wenje ilipangwa na cdm kama chama Wenje alitumika kuwasilisha wabunge wote wa cdm. Mh Lema anajitahidi kutatua matatizo yana Arusha. hivi unategemea mabadiliko gani makubwa ndani ya miezi 10, kijana ndo ameingia hebu tumpe mda kidogo.

Hivi ni kitu gani au tatizo gani ambalo umemwona Lema amejaribu kuli address angalau kwa kuliongelea tu? Yeye hakai kitako jimboni asikilize matatizo ya watu wake. Kama anaweza kwenda Singida kuhamasisha inakuwaje anakosa muda wa kutembelea hata kata moja za jimbo la Arusha ili kusikiliza matatizo ya watu wake.
 
Mimi nilimchagua Lema na hata sasa mimi ninampa supporti kubwa ila sioni kwamba yeye ni malaika asighafilike ktk utendaji wake. Kuna mambo ya msingi ktk hoja iliyotolewa kwani pamoja na umeme kuwa janga la taifa ,hapa Arusha Meneja wa TANESCO ana tabia ya kusababisha internal mgao bila sababu za msingi na hamna ufuatiliaji. Kwa mfano utakuta watu wa Kimandolu wanastahili kupata umeme kuanzia saa 2 asubuhi lakini utwashwa saa 2 ila baada ya I hour unakatwa na kuja kuwashwa saa 11 na utazimwa saa 12 na hapo zamu inahesabiwa imeisha. Suala kama hili anatakiwa mbunge kufanya follow up na si kila mwananchi kukimbilia tanesco kwani tumepiga simu tumechoka na sababu zinazotolewa kwa kiasi kikubwa zinaashiria ni uzembe wa TANESCO mkoa na si suala la upungufu wa umeme kitaifa.
 
Unajua Lema anaweza akasema hilo swala bungeni. Lakini yeye co mtekelezaji. Kibaya zaidi msemaji na mtekelezaji ni maadui,ingawa tatizo lenyewe ni la kitaifa,lkn pia tunafahamu kila mtu na machungu yake. Unajua tulikoxea wapi.. Pale juu,2015 tumtoe yule anayeongoza nchi sasa na tumpe mwenye itikadi xawa na Lema.. Mambo yataenda. Tuliharibu paleeee,tulipoamua kumpa kuku mayai ya khanga..
 
Unajua Lema anaweza akasema hilo swala bungeni. Lakini yeye co mtekelezaji. Kibaya zaidi msemaji na mtekelezaji ni maadui,ingawa tatizo lenyewe ni la kitaifa,lkn pia tunafahamu kila mtu na machungu yake. Unajua tulikoxea wapi.. Pale juu,2015 tumtoe yule anayeongoza nchi sasa na tumpe mwenye itikadi xawa na Lema.. Mambo yataenda. Tuliharibu paleeee,tulipoamua kumpa kuku mayai ya khanga..



Hatukati tamaa kwani tuko focused 2015 maana tunataka kizazi cha ukweli kuongoza nchi na 2015 ni option yetu ya mwisho kuifanya nchi irudi katika mstari wa ukweli. Ila pia tuliowachagua wanatakiwa waonyeshe ktk kipindi hiki cha miaka 5 kwamba "YES WE CAN" la sivyo wananchi watafanya uamuzi in favour ya watakaoweza ku address matatizo yao.
 
Hivi kwanini baadh ya wanacdm mmeanza tabia za kimagamba ya kutokukubali kukubaliana,mwandika thread ana deserve kujibiwa na lema,kwa nn wengine mnabeza hiyo ni tabia ya kimagamba mnataka kila siku kusifiwa tu?sidhan kma kweli tunaitakia mema cdm hii tabia inajenga!wabunge wetu sio malaika na wanaitaji kukosolewa,kma kuna upupu achaneni nao najua kuna point kwenye alichoandika achaneni na habari za zidumu fikra.

Ndugu yangu hakuna cha maana katika post hii zaidi ya pumba, anasema Lema haongelei kabisa matatizo ya Arusha badala yake anakomalia issue ya UMEYA na WAZIRI MKUU KUSEMA UONGO.... Sasa mtu kama huyu utamjibu nini maana inaonekana hana anachojua juu ya siasa za TZ. Lema ataletaje maendeleo wakati hakuna meya wa kuchaguliwa? Ataletaje maendeleo wakati wananchi wanauwawa na serikali iliyopo madarakani ili hali waziri mkuu anasema uongo juu ya mauwaji hayo? maendeleo ni Amani na utulivu pasipo utulivu hakuna maendeleo, watu wamepigiana simu kufanya uchaguzi wa umeya bila wengine kujua halafu unataka Lema akae kimya? waziri mkuu anasema uongo halafu unataka Lema akae kimya? kukaa kimya kwa Lema maana yake amekubali Meya ni halali na waziri mkuu ni mkweli.

Vilevile umeme ni tatizo la nchi nzima haliwezi kutatuliwa na Lema pekee yake bila serikali kuu.
 
1. Kuhusu kuwa mkazi wa Arusha au la ni ngumu kusema lakini hali hii--- mbunge wangu- wangu- wangu( fuatilia bold italics hizo) ................. hata mtu anayepretend anakuwa hivyo mara nyingi. Kuna maneno yenye red yanaonyesha kama unalazimisha hivi, kwamba si mtu wa hapo hivyo unatumia nguvu kuaminisha. Kama sivyo unatakiwa kuicheki hali hiyo muda mwingine

2. Ukosoaji ; Ukosoaji umekuwa mkubwa sana nikilinganisha na mategemeo uliyoyataja. Kwa mawazo yangu, kwa mategemeo unayoyataja ambayo ulikuwa nayo kwake na kama kweli ulimpigia kura- sitegemei disappointment ya kiasi hiki hivi sasa, zaidi nimetegemea kwamba ni muda ambao ilikuwa ndio mnapanga na kiongozi wako kwamba- bwana unajua hapa Arusha TANESCO wanazima umeme makusudi ili muone anachukua hatua kiasi gani, akishindwa uzungumze vingine.
3. Lakini pia aina za kauli, kauli zako zimekuwa na criticism zenye makali (mfano -tulimwona kama mkombozi nazo bado zinapingana na unachokisema) ; Ujumbe huu ulikuwa unaweza kufikishwa kwamba 'Mh. Lema, matatizo haya bado yanatusumbua hapa Arusha ----yataje1,2,3,4,5....... Ingawa katika umeme Wakati mwingine mgao huu unafanywa aidha kwa uzembe au kwa upendeleo na usanii wa hali ya juu na TANESCO mkoa kwa kisingizio cha overloading. Tafadhali liangalie hili kwa makini/ lifuatilie haraka'
Naamini ujumbe huu utaupata na utaufanyia kazi na I stand to be corrected!!!!

Au vingenevyo inavyofanana tofauti na ulivyoweka. Kama kweli ulikuwa na nia nzuri kama unavyodai.

Ingawa kitu kingine ambacho kinanitia shaka ni kwamba wana Arusha hasa jimbo hili wanafahamu maendeleo yao na matatizo kwa ujumla, kuna mwamko mkubwa ukilinganisha na maeneo mengine hapa nchini, hivyo nimetegemea kuyaona unayoyasema kwa wengi zaidi kama ndiyo mawazo ya wengi, na kama umetokea kuwaza wewe mwenyewe, basi ujumbe huu unakuhusu sana.

Ingawa wadau wa JF, unajua mwisho wa siku watu wanataka kazi, majibu ya kuridhisha ya maswali yao- la msingi kama yanatokea ni vema akaambiwa- atafanya kazi na watu watampenda zaidi na zaidi.

Ninavyoamini mpaka sasa,
wabunge wa chama cha Lema wamekuwa wawajibikaji kwa ujumla hasa kwenye suala la ufuatiliaji, sijadhani kama wanangoja kusukumwa, hii ni sifa yao- mpime Mbunge mmoja mmoja kutoka chama hiki na uwafananishe na wa vyama vingine, nategemea utapata zaidi ya asilimia 80 wazuri hawa hasa kwa kigezo hicho cha ufuatiliaji mambo.

Nimekuwa nikifuatilia bunge linaloendelea kwa karibu sana ili nione jinsi ambavyo mbunge wangu Mh. G. Lema atakavyo peleka kero za wapiga kura wake wa hapa Arusha mjini. Kwa bahati mbaya sana kimtizamo wangu ninapata shida na mbunge wangu kama hakika anajua matarajio ya wapiga kura wake walipomchagua.

Tulipomchagua Lema tukaacha wengine tulimwona kama mkombozi, mtu asiyeweza kuvumilia kuona wananchi wakinyanyasika na matatizo ambayo serikali ina uwezo wa kuya- address. Kwa bahati mbaya sana kama hali itaendelea ilivyo matarajio yangu yanaanza kuyeyuka kwani kwa muda mfupi tu wa uongozi wake ktk jimbo letu hapa Arusha kuna matatizo madogo sana lakini ambayo ni kero lakini sijamsikia hata siku moja Lema akijaribu kufanya follow up.

Nataka nimweleze tu Mh. Lema kuwa tatizo la umeme hapa Arusha lilianza mara tu baada ya yeye kutangazwa kushinda ubunge hapo November 2010. Sisemi kwamba yeye alisababisha tatizo la umeme ila inawezekana kuwa ni hujuma iliyopangwa ili kuingiza upuuzi ktk akili za tuliokupigia kura kwamba bila Magamba huduma nyeti za kijamii zitadorora jambo ambalo ni obvious si kweli.

Tangu November Mwaka jana sisi wapiga kura wako tumekumbwa na tatizo la mgao wa umeme lillilokuja kuunganishwa na mgao wa kitaifa na hadi sasa hivi bado tunaendelea kuumia. Wakati mwingi mgao huu unafanywa aidha kwa uzembe au kwa upendeleo na usanii wa hali ya juu na TANESCO mkoa kwa kisingizio cha overloading na hivyo kusababisha hasara kubwa kwa wajasiriamali wadogo na wakubwa.

Cha kushangaza ni kwamba kwa kipindi chote hiki sijakusikia popote ukizungumzia tatizo hili zaidi ya UMEYA na WAZIRI MKUU KUDANGANYA BUNGE. Kwa namna hii nakuona uko OUT OF TOUCH na concern zetu wakazi wa Arusha na badala yake unajishughulisha na mambo ambayo nafikiri yanakupa satisfaction kama individual zaidi.

Mbaya zaidi juzi hili tatizo lilipofika Mwanza mbunge jirani yako pale mjengoni Mh. Wenje wa Nyamagana aliweza kuinuka na kupeleka kilio si tu cha wapiga kura wake kwa wahusika lakini pia akakusaidia wewe kufikisha kilio cha watu wa Arusha bungeni. Mimi binafsi sikujisikia vizuri pale mbunge wa jimbo lingine anapokusaidia kufikisha kilio cha wapiga kura wako serikali ili hali wewe umejikalia tu bila kufanya juhudi zozote.

Hivi ina maana haya matatizo ulikuwa huyajui au frequencies zako zinashika UMEYA NA WAZIRI MKUU KUDANGANYA BUNGE ZAIDI kuliko immediate problems za watu wako ? Tunapata irregular,biased na unnecessary mgao si kwa sababu umeme ni wa shida hivyo bali kwa sababu meneja aliyeko yuko kisiasa zaidi kuliko ki professional na matokeo yake anaona kama Dar kuna mgao kwa nini Ar usiwepo hata kama si lazima.

Ninaamini ktk hili eneo hujafanya follow up kwa huyu meneja wa Arusha vya kutosha na sidhani kama hiyo iko kwenye ajenda zako kwani hata mikutano yako sijasikia ukigusia hili tatizo. Kama meneja anakuwa arrogant kwa nini usitu mobilize tukapige kambi pale ofisini kwake mpaka jioni ile ajue kama wananchi wamechoka.

Mh. Lema naomba uwe at per na matatizo ya watu wako na active kuyashughulikia kwani ndicho tunachotegemea kwani kesi yako na Pinda haitasaidia kuondoa tatizo la mgao usio na usawa au matatizo mengine. Hatutajisikia vizuri kabisa mtu mwingine kukusaidia kuongelea matatizo ya nyumbani au chumbani kwako kama alivyokusaidia Wenje kwani hiyo ni sign mojawapo ya FAILURE na kuwa IRRESPONSIBLE Leader.

Tuna matatizo chungu nzima ambayo mengine hayahitaji budget kupitishwa bali inahitajika kiongozi kama wewe kupiga kelele kama alivyokusaidia Wenje. Mh. sina lengo la ku disapprove role yake bali kukumbushana na kushtuana ni muhimu kwani inawezekana ume concentrate kwenye masuala ya kitaifa zaidi ukasahau ya wananchi tuliokuchagua katika jimbo lako. Ni vema ukamaliza ya jimbo lako kabla hujakomaa ktk masuala ya kitaifa.

Naamini ujumbe huu utaupata na utaufanyia kazi na I stand to be corrected!!!!

Peoples!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! Power!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mtoa mada umechemsha
Wenje ni cdm so aliwakilisha
C cdm wamoko akiongea m1 ni kwajili ya wote upo n abt ume2 we mwenyewe ni shahidi 2wkz b4 bajet kupita ume2 ulikuwa furuu baada ya hpo,,don blame mr. Lema 4dat coz ni janga la taifa
Na uongoz ukiwa poa maendeleo yanakuwa powah sakm mayor kimeo unataka lema acheke 2 ili badae ula2mike kinafki
1mor bajet ndo imepita so wait ze reaction afu ndo uje utoe lawama
Kwasa2 letz join 2gezer 2wasupport viongoz we2 wa cdm na 2cwe wanafki km magamba au co?
Get dt

Mmmm.... hii nini tena? uandishi kama huu niliwahi kuuona kwenye simu ya mtoto wangu yuko Secondary School, yaani huwa sielewagi kabisa. ila atapita hapa ofisini kwangu nitamuomba anisomee.
 
Mimi sio mnazi wa CDM kivile. lakini mlota hoja amekurupukuka ama anachuki binafsi.
Sioni anajaribu kusema nini hasa?
 
nami naona mtoa mada ujawasilsha kwa usanifu,.iko hvy 2natakiwa2achane na ushabik wa uchaguz uliopita tayari uwezi ukategemea kila m1ja wenu personal fealings bungen kuweni wavumilv chama lazmakijipange kimbinu na c wewe unataka nn wakati ukipata shda znazokutia ww uvivu wakuzita2a binafsi
 
changamoto aliyoleta mtoa mada ni ya kinafiki!yapo matatizo mengi ya msingi yanayoikabili arusha lakini kubwa linaanzia kwenye umeya wa halmashauri na kwa hili mb lema alilipa kipaumbele,huwezi kuoengelea matatizo au maendeleo ya arusha iwapo uongozi wa halmashauri haujapatanishwa.umeme ni tatizo la kitaifa ni vyema likafanyiwa kazi na wabunge wote sio lema pekee.



Mkuu pana ukweli hapo.
 
Lema alihaidi hospital 3,machinga complex 1 na barabara za lami kilometa 10 badala ya maendeleo tunaambulia mabomu,maandamano,mdororo wa uchumi ie mikutano mikubwa imehamishiwa Dar kukwepa maandamano ya CDM
 
Back
Top Bottom