Kwa hiyo "uki kejiliwa" tu utamaindi sana siyo na kuanzisha "vagi" kwa sbb ya "kejeli" toka kwa "mkejeli?"
Hujui kuwa wewe unaye maindi ndiye utakuwa na shida ktk judgement yako kuliko aliye kukejeli?
Kama wewe ni muumini wa dini ya kikristo i.e mkristo nishushauri uende ukasome kitabu kitakatifu cha Biblia (New Testament) kuhusu kiongozi shujaa na mfalme wa wafalme Yesu Kristo kuanzia kitabu cha Mathayo Mtakatifu hadi Ufunuo, utajifunza mengi sana juu ya kuzishinda kejeli.
Hakuna kiongozi yeyote mkubwa aliyewahi kuishi ktk dunia hii na kupokea kejeli za hali ya juu kama YESU KRISTO na kamwe hakuwahi kugombana wala kulipiza kisasi dhidi wakejeli wake ambao walifikia hatua mpaka ya kumtemea mate na yeye kamwe hakuwahi hujali zaidi ya kusema "baba wasamehe kwa kuwa hawajui walitendalo!"
Hawakuona hilo linatosha kwani huyu ndugu pamoja na kukejeliwa saaana, hakuwahi kuanzisha vurugu japo alikuwa na nguvu na mamlaka ya kuwaangamiza wote kufumba na kufumbua tu!!
Mwisho waliona huyu mtu dawa yake ni kumuua tu tena kwa kifo cha fadhaa na kutisha. Yet he went on loving all na leo hii bila yeye mimi na wewe si kitu!!
Ukimuona mtu "ana maindi" hata kejeli za mwendawazimu wakati yeye anajijua ni "timamu" jiulize mara mbili mbili kuhusu utimamu wake na pengine tambua mara moja kuwa yeye ndiye hasa mwendawazimu!!