Lema athibitishwa kuwa mfalme wa Arusha leo mbele ya Rais Magufuli hadi Gambo kaona aibu kumtambulisha

Ukikaa na chuki kama zako unakuwa mchawi tu!! Sasa hapo mbona katambulishwa bila shida!!!!
 
Aisee hata mimi nilishuhudia mlipuko wa kelele pale Gambo aliposema anautambua uwepo wa rafiki yake Lema
 
Tatizo la Arusha ni moja tu,mbunge awamu 2 hua zinamtosha hawaongezi zaidi,big up Lema wapi Felix Mrema.
 
Screenshot_20180407-213450.jpg
 
Inawezekana wewe uwezo wa kutafsiri matukio ni mdogo.

Tukio lile kwa msomi mwenye upeo mpana anaweza kutoka na tafsiri nyingi. Kwa hiyo yawezekana matukio mengine yote ni ya kawaida ila lile halikuwa la kawaida.

Wananchi kumshangilia sana Lema, kuna kitu wanataka kumweleza Rais japo hawakupewa nafasi ya kuongea. Nafasi ndogo waliyopewa, waliamua kumfikisha ujumbe Rais. Na Rais kama ni mtu anayependa kusoma hisia za watu, ujumbe wao atakuwa ameupata ila wewe kwa bahati mbaya umeshindwa kuelewa uzito wa ujumbe wa wananchi kwa Rais.
Walichoshangilia ni ile lugha iliyotumika kumtambulisha Lema sio kwamba walimshangilia lema
 
Awamu ya Tano badala ya viwanda wamejikita kudidimiza Demokrasia wanajua Vyama vya upinzani vikiwa imara vitawazui kupiga Dili za 10% kwenye miladi na manunuzi mbali ya kitaifa kupitia pesa za walipa kodi kule Hazina, pesa inayotumika kudhoofisha upinzani ni pesa nyingi sana ni pesa ambazo zingeweza kujenga Hosptal za rufaa kila mkoa na kuajiri madaktari toka India na wagonjwa wote wakatibiwa nchini pasipo kupelekwa nje, pia Nchi Jiran wangekuja kutibiwa Tanzania na kuingiza pesa za kigeni kuongeza pato la Taifa.
Viwanda havihitaji siasa za majitaka za upinzani za kupinga kila kitu.
 
Gambo nakumbuka aliwahi kumwambia Rais kuwa tumeimaliza CHADEMA Arusha.
Salamu ya Jana kanisani imewaonyesha kuwa Lema ni Arusha na Arusha ni Lema


Kwa uchaguzi huru na haki, ccm hawana hata diwani moja Arusha.
 
Yaan nna uhakika ya laiti watu wa Lumumba ndiyo wangekuwa wana fursa ya kurecord lile tukio wao peke yao lazima kipande cha Lema wangekidelete
 
Back
Top Bottom