Lema atabiri machafuko tena Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lema atabiri machafuko tena Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Molemo, Dec 30, 2011.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Asema atakufa kulinda haki za wananchi

  MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA), ameonya juu ya uwezekano wa kuzuka kwa ghasia nyingine kubwa ikiwa uongozi wa halmashauri ya jiji hili unaoundwa kwa sasa na watendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) utawahamisha kwa nguvu wakazi zaidi ya 24,000 wa eneo la Kaloleni kupisha ujenzi wa mji wa kisasa.

  Lema akizungumza na Tanzania Daima juu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa mji wa kisasa wa kibiashara katika eneo la Kaloleni jijini Arusha, unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitano ambapo jumla ya wakazi 24,000 watalazimika kuhama, alisema hawezi kukubaliana na mpango huo mbovu wa kutaka kuwahamisha wakazi wa eneo hilo kabla ya kufikiwa kwa mambo ya msingi na pande zote zinazohusika.
  Mbunge huyo alisema kinachotaka kufanywa na uongozi wa jiji ni cha hatari na yeye kama mwakilishi wa wananchi wote hatakubaliana na mpango huo, badala yake ataungana na wananchi kuchukua hatua nzito na madhubuti za kuzuia jaribio lolote la kuwahamisha wananchi hao wa Kaloleni.
  Aliutuhumu uongozi wa jiji chini ya meya mwenye mgogoro, Gaudence Lyimo, kwa kutumia mabavu kuamua mambo yanayohusiana na uhai na utu wa mtu kwa sababu ya fedha za wawekezaji.
  Akifafanua juu ya jambo hilo, Lema alisema madiwani na uongozi wa jiji wamefikia uamuzi huo kutokana na kiwewe baada ya kupewa ufadhili wa kwenda Dubai na kulipiwa mamilioni ya fedha na mwekezaji huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kujifunza namna miji ya wengine ilivyojengwa kibiashara.
  “Mimi siko tayari kupokea fedha hizo chafu ili kuwasaliti wananchi wangu. Nitasimama imara na masikini wenzangu kutetea haki, utu na heshima yetu kama wanadamu katika ardhi aliyotupatia Mwenyezi Mungu,” alisema.
  Hata hivyo, mbunge huyo alisema kimsingi hapingi kuwapo kwa shughuli za maendeleo katika jiji hilo, lakini akadai kutokubaliana na taratibu zote zilizofikiwa kumpata mwekezaji huyo, ikiwa ni pamoja na kutowashirikisha wawekezaji wazawa katika mchakato mzima wa zabuni.
  “Nieleweke tangu awali kuwa mimi sipingi kuanzishwa kwa eneo la mji wa kisasa, wala shughuli za maendeleo kwa watu wa arusha. Nikifanya hivyo nitakuwa mbunge wa ajabu sana na hata chama changu kitanishangaa. Ninachokataa ni ukikukwaji wa mambo mengi ya msingi, ikiwa ni pamoja na kutowashirikisha wananchi watakaohama kupisha mradi huu.
  “Kwanza huyo meya wao aseme lini tenda hii ilitangazwa na ni Watanzania wakazi wa Arusha wangapi walishirikishwa. Kama hilo halikufanyika, siwezi kukubaliana na mpango mzima na lazima tuanze upya,” alisema Lema.
  Aliongeza kuwa ni jambo la kushangaza kwa chama kinachodai kujali wananchi wake kwenda kuwabeba wawekezaji wa kigeni na kuwaacha Watanzania wenye uwezo mkubwa wa kujiendeleza na kuendeleza nchi yao.
  “Mji huu umejengwa na kuendelezwa na wananchi wenyewe, na hata ule wa Moshi. Sasa imekuwaje hata katika mradi huu wasihusishwe na wadharaulike?
  Lema alidai kuwa mapema wiki hii, kuliitishwa kikao maalumu cha madiwani na viongozi wa halmashauri na kuhudhuriwa na mwekezaji huyo kikiwa na nia ya kupanga mikakati ya kuanza kwa ujenzi huo.
  “Nimepokea taarifa kwamba baadhi ya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi, wakiongozwa na mtu anayejiita meya pamoja na wakurugenzi wa kampuni hiyo wamekubaliana kuanza ujenzi katika eneo la Kaloleni haraka iwezekanavyo.’
  “Huu ni usaliti kwa wananchi kwa sababu, hakuna maandalizi yoyote makini yaliyofanywa, wala mimi kama mbunge sijashirikishwa na wananchi wangu hawajakubaliana na mamlaka hiyo katika mambo mengi ya msingi,” alisema Lema.
  Aliongeza kuwa suala la kuwahamisha watu si la mzaha na linahitaji maandalizi makini, ya haki, yenye masilahi na yaliyokubaliwa na kila upande unaohusika.
  “Haiwezekani kuhamisha watu bila kwanza kukaa na kukubaliana nao wapi wanakoenda, wanakwenda kwa utaratibu gani na wanalipwa kiasi gani, lini na kwa njia gani fidia ya nyumba na mali zao,” alisema.

  SOURCE:TANZANIA DAIMA
   
 2. T

  Tanzaniaist Senior Member

  #2
  Dec 30, 2011
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 162
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Saaaafi sana Mbunge! Ndio Maana nilishawahi kusema Tanzania Hakuna Mbunge Kama Godbless Lema...,Ambaye ameamua kuweka mbele maslahi ya wananchi kwanza na pia kuuliza kwanini wawekezaji Tanzania hawajahusishwa? kwani Tanzania hakuna wawekezaji ...,huyu anaweza kuwa raisi ajaye Tanzania
   
 3. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #3
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Mh. Lema kubali maendeleo yaje kwa faida ya wengi; hizo guest house za Kaloleni zina tija kidogo sana kwa uchumi wa jiji letu la Arusha
   
 4. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #4
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  mkuu huyu mwekezaji anatoka nchi gani?ni kwa nini haya mambo yafanyike kwa siri na yanatuhusu sana sisi?hilo ni tatizo
   
 5. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #5
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Madai ya mbunge yanapoints.
   
 6. Bhbm

  Bhbm JF-Expert Member

  #6
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 716
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35

  Nashauri ungejaribu kurudia tena kusoma vizuri maelezo ya mbunge Lema ili umuelewe vizuri anachomaanisha, haifai kupinga kila kitu kwa kukurupuka na kusukumwa na ushabiki wa kichama.
   
 7. N

  NDOFU JF-Expert Member

  #7
  Dec 30, 2011
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 656
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kama kingamboni kama Arusha!
   
 8. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #8
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  NI UKWELI KWAMBA TUNATAKA MAENDELEO TATAKAYOWANUFAISHA WATZ NA SI MA-BAAZAZI WACHACHE TOKA NJE!
  TANGU TUANZE KUWEKEZWA,TUMEFIKIA WAPI?
  UPO SAWA MH LEMA,WIN-WIN situation has to be met!
   
 9. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #9
  Dec 30, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Kushirikishwa kwa wananchi ni jambo la muhimu sana katika miradi mikubwa kama hiyo,kwa hiyo hoja ya mbunge ina mashiko,isidharauriwe.Tusipokuwa makini yanaweza kutokea mauaji kama ya mbeya!
   
 10. Myakubanga

  Myakubanga JF-Expert Member

  #10
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 5,816
  Likes Received: 329
  Trophy Points: 180
  kWELI KABISA!
  UVIVU WA KUSOMA UNAPONZA WENGI!
   
 11. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #11
  Dec 30, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,671
  Trophy Points: 280
  Juzi nilileta thread humu JF kuhusu huo mradi nakauliza Lema, naye anahusika sikupata jibu sahihi..

  Leo ndio nimepata jibu, hivi huo mradi ni wa Chadema au CCM? huo mradi ni kwa manufaa ya wana Arusha.

  Nashangaa Lema kujipa majukumu ya Shekh Yahaya utabiri
   
 12. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #12
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Hoja nzuri sana hii.

  Ina maana wanainchi wanaoishi pale Kaloleni hawajashirikishwaga? Kweli kuna kazi ya ziada kuwaelimisha viongozi wabovu waliopo madarakani hasa ktk uongozi mbovu wa sisiem. MB Lema tupo pamoja A to Z! Aluta Continue!! Acha kama inakuwa mbaya na iwe mbaya tu. Mpaka wanainchi wa sehemu husika wakubaliane na kauli tajwa.

  Ama wanafikiri pale wanaishi watoto wao. Na hata kama ni watoto wao ni lazima ungemhabarisha ya kwmb siku fulani hapa utahama na utaenda sehemu fulani kwn hapa nafanya ukarabati na utasikia majibu ya mwanao kama atafurahia ama atalalama.

  Lakini nafikiri hakuna mtu anayeichukia maendeleo,kinachoshangaza ni wanainchi hawajaambia tu kwa ustaarabu ya kwmb hili linakuja.

  Ngoja tusubirie na tutaona yajirio!
   
 13. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #13
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Wewe ritz!

  Hata kama ni kwa faida ya wanainchi wenyewe,lakini lazima maelewano yawepo tena mazuri tu siyo unawajia watu waishio pale kama watoto wadogo haiwezekani hata kidogo.

  MB uko sahihi sana na endelea kuwasimamia wanainchi wako kama ilivyoada yako.
   
 14. Mvaa Tai

  Mvaa Tai JF-Expert Member

  #14
  Dec 30, 2011
  Joined: Aug 11, 2009
  Messages: 6,174
  Likes Received: 2,175
  Trophy Points: 280
  Hajakataa maendeleo, tatizo ni utaratibu wa kupata hayo maendeleo, huwezi ukakiuka taratibu kwa kisingizio cha maendeleo. Mimi nilijua wahusika wametaarifiwa kwamba watahama na watahamishwa vipi, pia nilijua tenda zilitangazwa hakuna Mbongo wala mtu kutoka Taifa lolote duniani aliyeweza kukidhi vigezo na hatimaye Huyo mwekezaji kutoka Dubai akashinda. Wewe nakufananisha na watu wanaobariki hata wakiona dada yao anajiuza ilimradi tuu anapata maendeleo.
   
 15. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #15
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,010
  Likes Received: 1,816
  Trophy Points: 280
  Jamani si nilisikia ya kwamba mzee 6 amewapatanisha Lema na Lyimo sasa mbona Lema anamwita Lyimo ati "anayejiita Meya"!

  Lema naye hatabiriki yupo kama hali ya hewa!
   
 16. Watunduru

  Watunduru Senior Member

  #16
  Dec 30, 2011
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 163
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  big up mh Lema,mfano wa kuigwa kwa wabunge goigoi waganga njaa.kama maendeleo ni kwa ajili ya watu kwa nini kusiwe na taratibu nzuri na kushirikisha walengwa ili kupata muafaka wa pamoja?hivi serikali bado haiamini kwamba Arusha kuna tatizo eh???na hao madiwani wanaoendekeza bahasha siku zao zinahesabika.
   
 17. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #17
  Dec 30, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wewe ndiye utabiriki kwani Lema aligombana na Lyimo? naswala la mgogoro wa arusha Lema hawezi kupatanishwa na Lyimo kwani hawa gombana kwa maslahi yao kwamba mtoto wa Lema amenda kuowa kwa Lyimo useme watoto waligombana hivyo Lema ahitaji kukaa na Lyimo wawapatanishe watoto pia wapatane Lema Lyimo hilo la mzee 6 siyo unalo fikiri wewe kwani hawa kupatanishwa bali waliambiwa wasalimiane
   
 18. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #18
  Dec 30, 2011
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,529
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Usifike huko Mh. Lema ni mjumbe halali wa Baraza la madiwani, anayofursa ya kwenda kuhoji huko kwenye vikao vyao
   
 19. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #19
  Dec 30, 2011
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160
  Kimbunga!

  Wewe ndiyo hautabiri kama unavyosomeka jina lako.
   
 20. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #20
  Dec 30, 2011
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,496
  Likes Received: 2,740
  Trophy Points: 280

  There you go again!!!!!

   
Loading...