Tazama hapo kwenye red: mradi wenye manufaa kwa wana Arusha! Ni manufaa gani? Hivi kwa akili yako unaweza kusema kuwa ni jambo la maendeleo kwa mfano; mwekezaji anapopewa ardhi ambayo ilikuwa yako bila wewe kuulizwa na mwisho wa yote mwekezaji ajitafutie faida yake? Kuna mwekezaji gani kutoka wa kigeni aliyekuja kuwekeza hapa TZ na mwisho tukafaidika Watanzania?
Hii nchi kama tunategemea kuijenga kwa nguvu za uwekezaji kutoka nje, je, yatakuwa maendeleo kweli ya Watanzania? Chukua mfano mdogo, mwekezaji anawekeza kijiji kwako katika mradi unaozalisha faida ya Bilioni moja kwa mwaka. Katika kijiji hicho pato la wananchi wake ni miioni 50 kwa mwaka. Jumlisha pato la mwekezaji na wanakijiji unapaata bilioni moja na milioni hamsini kwa mwaka. Pato la kijiji hicho kwa mwaka (ukijumlisha na la mwekezaji) kwa mwaka litakuwa juu kuliko la baadhi ya mikoa katika nchi hii. Je, kiwango cha maisha ya wananchi yataendana na pato hilo?
Usidanganyike na uwekezaji ambao hauzingatii kuinua maisha ya wananchi kama ambavyo sasa hivi unafanyika Tanzania. Hakuna nchi inayofanana na Tanzania katika dunia hii kwa kufanya mamvo yake kiholela. Kitu cha ajabu zaidi ni kuwa, pamoja na kuona jinsi viongozi wa serikali wanavyotupeleka jehanamu, bado kuna wananchi kama ritz wanaendelea kuunga mkono upuuzi kama huu. Pole ritz kwa sababu unapenda uwekezaji huu wa Kitanzania. Ila tunajua kuwa "ukipenda chongo huita kengeza". Sii furaha ya Watanzania kuona kuwa mji umejengeka vizuri na hivyo kuwa kama mapambo kwao wakati wao wanashindwa kumudu maisha na wao wakiutazama kutoka pembeni kule ambako watakuwa wamehamishwa bila hata fidia ya maana.
Watanzania tupiganie haki zetu na wala tusikatishwe tamaa na kina ritz ambao wamekubali kula makombo na matapishi ya Wawekezaji.