Lema aanika meseji ya Ben Saanane

Lema aanika meseji ya Ben Saanane

Hotuba iliyosimama,...nilitamani aendelee kutoa nondo..
 
Kuna mwalimu shule ya msingi alikua anasema " ukiamua kuniloga, hakikisha nnakufa, ukinikosakosa hautabaki salama"..the return of GL.
Umesomea Kigoma eti? Huyo Mwalimu alikua Mhaya? Namkumbuka saaaanaaa
 
Sasa hizo meseji za Ben ziko wapi, jamani mbona povu? Hili sakata la kijana Ben inabidi wamkamate Mbowe na kumuuliza, ni yeye ndiye atakuwa anajuwa ukweli si CCM.
 
Ndio akina Lema wachukue Nchi? Ridiculous!
Ungependa watoke mbinguni mkuu??!! WaTz ni hawa hawa na bora kina Lema wana ujasiri wa kukemea kuliko kulamba vyatu vya watawala hata kama wanawadhulumu wananchi
 
Kamanda anajitambua sana, hekima na busara tele.

Hapo ndipo huwa namkubali Lema.

Anaweza kuwa na kasoro na madhaifu mengine lakini Lema sio mwoga na huwa anasema jinsi inavyotakiwa kusemwa. Na sio kusema tu bali kuishi na kutembea kwenye hayo maneno.
 
Hayo ndio matatizo ya wapiga kura wa arusha mjini waliyomtuma akaongee bungeni?
Huo ujumbe muhimu wa mtu mwenye kuangalia Taifa.Mbunge lazima uwe maono siyo ya jimbo tu,bali na upeo wa kitaifa.Wewe unauliza mambo ya kijinga,huna tofauti na Waziri anaepindisha sheria na kusema uongo kwa manufaa ya kulinda mtu mmoja Bashite.Waziri anajuwa kabisa katiba inazungumzia wabunge kuwa ndiyo wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika lakini wabunge walio wengi wa CCM,wamenyamaza kimyaaaa.Kimya maana yake nini,HOFU,WOGA,UJINGA,AU KUKUBALI YAWE HIVYO HIVYO POTELEA MBALI, kamandivyo kwa manufaa ya nani?TANZANIA MASKINI TANZANIA UNAKWENDA WAPI.Nawahi kuaga watoto wapendwa.
 
"Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Buffet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga"

Ikitokea siku hao MBWA wa CCM wakaelewa haya maneno itakua too late.
 
Siku hizi Ukawa wana CD mbili tu!

Moja ya Bashite nyingine ya Ben saanane, ya Kinana kila wakijaribu kuicheza Ina scratch
Yule muuza "unga"pale dukani amekamatwa nini ?
 
Utakuwa unaishi chini ya jiwe wewe! Hujasikia kuhusu bajeti hewa ya 29 trilioni lakini kutolewa 34% tu? Hujasikia kuhusu terrible teens na uongo wa Siri kali kwamba ile ni ndege mpya inatengenezwa? Hujasikia kuhusu kuanguka uchumi wa nchi kuanguka kwa sera za kukurupuka za uchwara? Kudharau katiba, kulidharau Bunge etc. Fungua akili yako achana na kujitoa ufahamu.
Kumbe uhuru wa habari upo sasa mnalilia nini?
 
Huo ujumbe muhimu wa mtu mwenye kuangalia Taifa.Mbunge lazima uwe maono siyo ya jimbo tu,bali na upeo wa kitaifa.Wewe unauliza mambo ya kijinga,huna tofauti na Waziri anaepindisha sheria na kusema uongo kwa manufaa ya kulinda mtu mmoja Bashite.Waziri anajuwa kabisa katiba inazungumzia wabunge kuwa ndiyo wenye sifa ya kujua kusoma na kuandika lakini wabunge walio wengi wa CCM,wamenyamaza kimyaaaa.Kimya maana yake nini,HOFU,WOGA,UJINGA,AU KUKUBALI YAWE HIVYO HIVYO POTELEA MBALI, kamandivyo kwa manufaa ya nani?TANZANIA MASKINI TANZANIA UNAKWENDA WAPI.Nawahi kuaga watoto wapendwa.
Ndio matatizo ya Jimbo la Arusha?
 
Ipo haja ya kukusanya hotuba zote za lema na kuziunganisha kwa ajili ya kufundishia kizazi kijacho.Kwani jamaa ana maneno yenye adili na mafunzo
 
Kungekua na bunge live haki ya nani ningependa kumuona Simbachawene alikua anaonekanaje baada ya kutajiwa kazi yake ya zamani. Lema ni noumer, haopi mtu. By the way hata hao wanao ua wenzao na wenyewe siku moja watakufa tu; ndio uzuri wa Mungu, unamtanguliza mwenzio na we siku yako ipo. Aliuawa Gadafi itakuja kua na hawa wa mikocheni?
 
Ni comment ila napenda kukumbusha kuwa tunaishi kwenye tufe ili tufe
 
Angalia paragraph ya kwanza Mkuu.

Mkuu huyu bwana mkubwa Simba cha wene alikua kondakta? napenda kujua alikua kondakta wa kitu gani, kwakua mchungaji msigwa yeye najua alikua chinga muuza mitumba pale iringa, na huyo Godbless mambo yake ya Mwanza pale kilimahewa kwa lema bado yanafahamika.
 
hiz
Lema aanika meseji ya Ben Saanane
www.ippmedia.com/sw/habari/lema-aanika-meseji-ya-ben-saanane

Akichangia mjadala wa makadirio ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Lema alisema: “Kama itanyesha mvua ya radi basi itaambatana na mwanga na cheche zitazowamulika walaghai, watesaji na watetezi wa haki watapata mwanga katikati ya giza totoro la unyanyasaji.”

Mbunge huyo alisema maneno hayo ni ujumbe wa mwisho ya Ben Saanane ambaye hajui kama ni marehemu ama yupo hai.

“Lakini hata kumjadili humu haturuhusiwi. Nje mikutano ya hadhara hatufanyi. Kama kijana wa miaka 16 katika Taifa ambalo halina uhuru wa vyombo vya habari, halina chama cha siasa aliandika maneno machache tu “Assad must go, Assad will be next, leo Syria haina amani,”alisema.

“Uhuru wa habari ni altenative (mbadala) ya amani, si kikwazo cha amani. Watu wanapoongea wanatema nyongo, ‘wanarealise tension’. Leo tunapotaka kujadili mambo ya msingi, mnatumia nguvu na uwezo mlio nao, mtashinda,” alisema Lema.

Alisema kila jambo wanalotaka kulipitisha kwa wingi wao watashinda.

“Katika mchango wangu uliopita, nilisema Mungu hadhihakiwi, apandacho mtu ndicho avunacho,”alisema

Alifunguka kuwa alipokuwa gerezani, vijana waliokamatwa kwa makosa ya mtandaoni ni wengi na walikamatwa kimya kimya.

“Wanapelekwa mahakamani wanasomewa mashitaka bila ndugu zao kuwapo. Vijana wamejaa magerezani kwa sababu ya ukosoaji,” alisema na kuongeza kuwa haiwezekani kuwa na taifa lenye amani bila kuwa na uhuru wa habari.

“Msifikiri mnatunga sheria kutukomoa sisi. Mna watoto wanakua, wajukuu wanakua…Tunapopigania uhuru wa habari hatupiganii Chadema, CCM tunapigania taifa bora na huru,” alisema.

“Leo ndani ya bunge hatusemi, kwenye mitandao hawaongei, vyombo vya habari havitasema huko mitaani mikutano ya hadhara imezuiwa. Iko siku watu wataingia mitaani kudai uhuru mnaowanyima.

Alisema watu hao watakuwa hawajatumwa na Chadema wala CUF na siku hiyo kila mtu atatafuta nyumba ya kujificha.

“Unapozuia haki, unapozuia uhuru, unapozuia kweli unatengeneza balaa katika taifa hili. Tunalalamika kwa sababu familia zetu zinaishi hapa, tungekuwa na mpango wa kuondoka tungeenda kulalamikia Marekani.

“Tukisema miongozo ni mingi na sijui hata hotuba yangu itakuwaje. Kama hotuba ya Waziri wa habari na michezo mmeifanya hivi, hotuba ya waziri wa mambo ya ndani na uzoefu wa Lijualikani alipokuwa magereza na uzoefu wangu nilipokuwa magereza mtaanza kuizuia kwenye salamu.

“Wabunge mko wengi tusaidieni, mawaziri tusaidieni tukishamalizwa sisi, msumeno utakaofuata utakuwa kwenu. Ni nini mnakipigania waheshimiwa wabunge, kita kitu kinakuwa hovyo. Ni fedha?,” alihoji.

Lema alisema utu wa mtu haupimwi kwa ghorofa, cheo, bali unapimwa kwa kazi na wajibu alioufanya duniani.

“Mimi nilikamatwa nje hapo getini nikapelekwa Kondoa nikaweka ‘lock up’ (rumande) saa 4:00 hadi saa 8 usiku nikapelekwa Arusha nikatengwa chumba peke yangu, nikakaa jela nikatoka baada ya miezi minne. Mnaweza kufanya hivi leo,” alisema.

Lema aliongeza kuwa: “Mimi mkitaka kuniua niueni leo, kesho ni mbali. Mkitaka kumuua yeyote hapa muueni leo, kesho ni mbali. Haya mambo mnayotuzuia kuyasema mnafikiri tunasema tunapenda uwanaharakati.”

Alieleza kuwa ana mtoto wa kwanza ana miaka 11 na wa mwisho ana miaka minne na angependa kuona ndoa na harusi na elimu za watoto wake kwa macho yake.

“Lakini ikibidi nisione hiyo harusi kwa sababu ya kupigania ya ninachokipigania watakumbuka maisha yetu bungeni kupigania property (mali). Yalipigania haki na msingi wa taifa hili ambayo mmeishindwa,” alisema.

Alisema ni muhimu wanaokalia Kiti cha Spika wakaacha faraja, baraka na kuacha kutumia wingi wa wabunge wa CCM.

“Hapo alikaa Mzee Sitta leo ni marehemu, kila mtu atapita kwa wakati wake. Ni muhimu mkapita mkaacha faraja nyuma, baraka acheni kutumia wingi wenu vibaya. Simbachawene wewe una historia. Ulikuwa kondakta Mungu amekuweka mpaka umekuwa hapo, tulitarajia kukuona wewe unapigania nchi hii.

“Leo unaishi utafikiri umezaliwa katika familia ya Warren Bafet. Mtu akisimama kuongea ukweli unapinga.
o

wanatoa povu kupigania haki za kiliberali. haki ya kujipatia mali kilaghai, uhuri wa kutoa na kupokea rushwa. uhuru wa mahakama usiyodhibitiwa, uhuru wa habari usio na mpaka. ndio maana hawawezi kua bayana wanatoa povu kupigania haki gani. wanataka uhuru wa wenyenacho kuwakandamiza na kuwanyonya wasionacho. huo ndio uliberali wa akina lema.
 
Back
Top Bottom