Leila Khaled & 1970 Dawson's Field Hijackings: Komando wa kike kutoka PFLP (Marxist–Leninist Arab Movement) aliyehusika kuteka ndege El Al Flight 219

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Leila Khaled & 1970 Dawson's Field Hijackings: Komando wa kike kutoka PFLP (Marxist–Leninist Arab Revolutionary Movement) aliyehusika kuteka ndege El Al Flight 219

Ndege za abiria zikilipuka baada ya kupigwa mabomu na magaidi wa PFLP katika uwanja wa Dawson huko Jordan.

images (1).jpg


Serikali nyingi hapa duniani huwa zina kawaida ya kukataa kutilia maanani maombi/amri/mahitaji ya magaidi. Na katika kusisitiza jambo hilo, Uingereza iliahidi rasmi kutofanya mazungumzo na kikundi chochote cha magaidi/watekaji nyara katika Mkutano wa Kimataifa wa Tokyo juu ya Utekaji Nyara (Tokyo International Convention on Hijacking).

Lakini ilikuwa ahadi ambayo ilivunjika mnamo 1970. Mnamo tarehe 6 Septemba mwaka huo ndege nne zilitekwa nyara na kukamatwa na PLFP - The Popular Front for the Liberation of Palestine, kikundi chenye msimamo mkali cha Ukombozi cha Wapalestina.

Dada mrembo sana komando Leila akiwa amenyoosha vidole viwili juu kama ishara ya ushindi baada ya kuachiliwa huru kutoka katika mikono ya Uingereza.

images (19).jpg


Walidai kuachiliwa kwa Fedayeen (wanachama wa harakati za Wapalestina) waliofungwa huko Ujerumani, Uswizi na Israeli. Ndege mbili zilipelekwa katika uwanja wa ndege wa zamani wa RAF (Royal Air Force) katikati ya jangwa la Jordan, unaojulikana kama uwanja wa Dawson.

Mwana mama Leila Khaled enzi za ujana wake pamoja na muonekano wake wa sasa baada ya kuzeeka. Alikuwa komando mrembo kweli kweli.

images.jpg


Ndege ya tatu ililipuliwa huko Cairo baada ya abiria na wafanyakazi kuachiliwa. Utekaji nyara wa nne ulishindikana baada ya magaidi wote kuzidiwa nguvu kwenye ndege. Mmoja aliuawa na mwingine, mwanamke aliyeitwa Leila Khaled, alikamatwa. Ndege hiyo ilielekezwa Heathrow, uwanja wa ndege wa karibu.

Khaled, ambaye alikuwa kamanda anayesimamia operesheni hiyo, aliwekwa chini ya ulinzi wa Uingereza. Uwepo wake ulilazimisha Uingereza kuingia katika mgogoro mkubwa wa kimataifa.

PFLP ilidai kuachiliwa kwa Khaled - pamoja na wale wengine wenye msimamo mkali wa Palestina. Ili kusisitiza jambo hilo, siku chache baadaye kundi liliteka nyara ndege nyingine, BOAC - VC-10 ikiwa njiani kutoka Bombay hadi Beirut.

Mwana mama Leila akiwa na baba wa bara la Afrka mzee Madiba enzi za uhai wake.

images (17).jpg


Waasi hao sasa walikuwa wakishikilia mateka zaidi ya 300, 65 kati yao wakiwa Waingereza. Uingereza inapaswa kufanya nini? Hitimisho la Baraza la Mawaziri kutoka tarehe 9 Septemba lilihitimisha shida ilikuwa inakabiliwa na Serikali ya Uingereza. "Baraza la mawaziri linakabiliwa na uamuzi mgumu na wa kihistoria. Mwanamke anayeitwa Leila Khaled anashikiliwa nchini.

Kuachiliwa kwake ni jambo muhimu katika kujadiliana na viongozi wa PFLP." PFLP ilituma ombi la mwisho (Ultimatum) la masaa 72 kwa Serikali ya Uingereza, na kusababisha maafisa kutafakari faida na hasara za kumwachilia. Faida ilikuwa kwamba walipaswa kumtoa jambo ambalo ni hatari katika eneo lao la uwajibikaji na waonekane wametimiza mahitaji ya PFLP na hivyo kuokoa maisha ya Raia wa Uingereza.

Hasara ilikuwa kwamba Marubani na mashirika ya ndege yanamakubaliano na maono yanayofanana kwamba haipaswi kutii makubaliano ya magaidi kwa lengo la kusaliti. Walikuwa wanapaswa pia kutupilia mbali mtazamo wao walioutangaza hapo awali juu ya utekaji nyara na walipaswa kupoteza uaminifu wote katika nyanja za kimataifa za katika masuala ya anga.

images (13).jpg


Walipaswa pia kukiuka Mkataba wa Tokyo wa mwaka 1963. Shukrani kwa kazi nzito ya kidiplomasia kutoka huko Amman na msaada wa mpatanilikubali kuongezewa tarehe ya mwisho.

Serikali ya Edward Heath (huyu alikuwa ni Waziri mkuu wa Uingereza kuanzia mwaka 1970 mpaka mwaka 1974) huko London tayari ilikuwa imekwisha kuhitimisha ya kuwa kuokoa mateka haiwezekani, na nyuma ya pazia Uingereza ilianza kujadiliana na watekaji nyara, kupitia njia zake rasmi na zile za siri.

Mazungumzo hayo yalifanikiwa mapema wakati wa siku sita za mgogoro huo, baadhi ya mateka - haswa wanawake na watoto - waliachiliwa bila masharti. Lakini watekaji nyara hawakuwa na subira kwa matokeo. Mnamo Septemba 12 kama ishara ya onyo walilipua ndege hizo tatu.

images (2).jpg


Kitendo hicho, kilichoonekana ulimwenguni kote kwenye TV, kilituma ujumbe mzito kwa maafisa wa Uingereza huko Amman juu ya nia ya magaidi hawa - pia ilikuwa ni tishio na mkwara mzito kwa Mfalme Hussein wa Jordan.

Mawasiliano ya wasiwasi yaliyoanza kati ya Balozi wa Uingereza huko Amman na mabosi wake wa London yalikuwa yanasema kwamba baadhi ya magaidi wa PFLP wasiojitambua na wanaopenda vurugu wamepata wazo la uongo kwamba Uingereza haitamwachilia Leila Khaled.

Waliwaambia kupitia kwa mpatanishi kwamba ikiwa hawatatoa, ndani ya masaa machache, angalau hakikisho kwamba Uingereza imejiandaa kufanya hivyo, jambo kubwa sana lingetokea. Watu hawa walikuwa na uwezo wa kuua mateka wote.

images (12).jpg


Utamu huu utaendelea next time nikipata muda.......!!!!!!!

NDUGU YANGU USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.
 
Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.
Umasikini ni m-baya sana mkuu na kutokana na magumu hayo niliyoyapitia ndio nikaamua kujiita Infantry Soldier.
 
Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.
Mkuu, wanazengo watakuja kusema kuwa wewe pia ni ID yangu kwa sababu tu umeni-quote hayo maneno
 
Mimi Infantry Soldier sio askari jeshi wala mtumishi wa ofisi yoyote ya serikali bali ni raia mwema ninayeipenda sana Tanzania. Hili jina nilijpa tu kutokana na changamoto kadhaa nzito nilizowahi kuzipitia katika maisha yangu. Hakika umasikini ni m-baya.
Haya maneno yako kwenye uzi gani?
 
Back
Top Bottom