Lecturer part 3

miss strong

JF-Expert Member
Jul 4, 2012
7,012
3,694
Poleni wana JF na majukumu ya kila siku.

Nimerudi tena kwa muendelezo wa ile kesi,nisiwachoshe sana lakin hali iliyofikia ni kutishiwa aman kabisa kwa ujumbe mfupi wa maaandishi kupitia simu yangu ya mkononi.
Kama nilivyotoa maelezo katika thread ile ya pili juu ya hatua zangu nilizochukua .........hatimaye ss uongozi katika ngazi ya mkurugenzi wa mafunzo alimuandikia barua huyo lecturer juu ya mimi kutojaziwa course work na kumuamuru nijaziwe course work yangu ndani ya masaa 12.
Lecturer huyo alifanya hivyo lakin hakuipeleka kwa mkuu huyo na badala yake akaipeleka kwa mkuu wa idara yangu........!

Kilichotokea sasa ametoa excuse kuwa alikuwa anaona majina mawili kwahyo ndo yalimchanganya.......mfano;TINA JOEL NA TINA KIMARO(majina haya si rasmi) wakati ukweli mtu huyo anatumia TINA JOEL KIMARO,hiyo ni sababu iliyomfanya acheleweshwe course work yangu.
Tukumbuke mtu huyo alishawahi niifundisha semister iliyokwisha somo jingine na haijawahi tokea tatizo hilo.Lakini leo hii anatoa hiyo sababu.

Lecturer huyo baada yakuwekwa kiktimoto na mkurugenz wa mafunzo,usiku wa siku hiyo hiyo nilipokea ujumbe uliotumwa na namba ngeni nao unasema hivi "Acha mchezo mchafu binti utaharibika kwa uzembe wako,hayo ni mambo yakupita binti yangu acha masihara utajuta.Yangu macho,usiku mwema."

Nilitafakari huo ujumbe sana,lakini nilijitia moyo.....Nilitolea taarifa kesho yake asubuhi kwa Mkurugenzi wa mafunzo.
Bado sijaitwa kwenye hiyo bodi ingawa kuna tetesi kuwa huyu mtu amekwisha andikiwa barua yakutaka kusimamishwa.

Tuombeane sana maana ni vita kubwa,nasubiri kuitwa tu.Nimesukumwa kuandika hili na moyo wangu ili muweze kufahamu nilipofika na pia hata kama lolote linatokea bas mtasikia tu, hata kama sintakuwepo katika dunia ila mtakuwa mmepata angalau kitu fulani.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI.
 
Usife moyo,pigana mpaka mwisho ili iwe fundisho kwa wengine.Nikutakie kila la kheri.
 
pole sana dada yangu.!?
japokuwa sikusoma part I & II but i can imagine uko katika situation gani.!
naamini mungu ni wa haki na sikuzote anasimama upande wa wenye haki.!
pole sana..
 
Anakutisha ili ufute kesi.Usijibu hizo meseji, ila zitunze.Vita ndiyo kwanza imeanza.hata yeye ana wasiwasi ndiyo maana anaendelea kukutisha.
 
tunasubiri hukumu.aliajiriwa kufundisha na sio kubaka.
mi natoa pongezi kwa uongozi wa chuo sana.naona wapo makini
 
Pole sana. Wala usihofu. Huyo lecturer alifikiri kila msichana ni wa kumchezea.....not you this time.
Inaonyesha wazi ni mwanaume asiyeheshimu wanawake. Kwake mwanamke hana thamani na ni sawa na kitu anamiliki. Namuonea huruma mkewe au mwanamke atakayemuoa. Huyo mwanamke atapata taabu sana.

Umempa fundisho ajue kwa kila atakalofanya kuna consequences. Na kama anasoma uzi huu inabidi aende akae chini na kujifikiria je alikuwa anategemea nini kwa kutaka kukubaka. Kwanzq yeye mwenyewe hakuheshimu ajira yake. Kitu kinachomuweka mjini na kumfanya aonekana mtu mtaani. Kama ni kijana basi ajirudi na aanze kufikiri upya.
 
Poleni wana JF na majukumu ya kila siku.

Nimerudi tena kwa muendelezo wa ile kesi,nisiwachoshe sana lakin hali iliyofikia ni kutishiwa aman kabisa kwa ujumbe mfupi wa maaandishi kupitia simu yangu ya mkononi.
Kama nilivyotoa maelezo katika thread ile ya pili juu ya hatua zangu nilizochukua .........hatimaye ss uongozi katika ngazi ya mkurugenzi wa mafunzo alimuandikia barua huyo lecturer juu ya mimi kutojaziwa course work na kumuamuru nijaziwe course work yangu ndani ya masaa 12.
Lecturer huyo alifanya hivyo lakin hakuipeleka kwa mkuu huyo na badala yake akaipeleka kwa mkuu wa idara yangu........!

Kilichotokea sasa ametoa excuse kuwa alikuwa anaona majina mawili kwahyo ndo yalimchanganya.......mfano;TINA JOEL NA TINA KIMARO(majina haya si rasmi) wakati ukweli mtu huyo anatumia TINA JOEL KIMARO,hiyo ni sababu iliyomfanya acheleweshwe course work yangu.
Tukumbuke mtu huyo alishawahi niifundisha semister iliyokwisha somo jingine na haijawahi tokea tatizo hilo.Lakini leo hii anatoa hiyo sababu.

Lecturer huyo baada yakuwekwa kiktimoto na mkurugenz wa mafunzo,usiku wa siku hiyo hiyo nilipokea ujumbe uliotumwa na namba ngeni nao unasema hivi "Acha mchezo mchafu binti utaharibika kwa uzembe wako,hayo ni mambo yakupita binti yangu acha masihara utajuta.Yangu macho,usiku mwema."

Nilitafakari huo ujumbe sana,lakini nilijitia moyo.....Nilitolea taarifa kesho yake asubuhi kwa Mkurugenzi wa mafunzo.
Bado sijaitwa kwenye hiyo bodi ingawa kuna tetesi kuwa huyu mtu amekwisha andikiwa barua yakutaka kusimamishwa.

Tuombeane sana maana ni vita kubwa,nasubiri kuitwa tu.Nimesukumwa kuandika hili na moyo wangu ili muweze kufahamu nilipofika na pia hata kama lolote linatokea bas mtasikia tu, hata kama sintakuwepo katika dunia ila mtakuwa mmepata angalau kitu fulani.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI.
Miss Strong are you born AGAIN??
 
Good girl, worry not huo ni mkwala tu na sasa upo kwenye mazingira salama zaidi. kwa kua umeshaliweka hapa mjanvini hata ukijikwa mahali ukaumia tutaju ni yeye tu and anything bad to happen to you he will be number one suspect. We are so close on this matter and we want to see how university can provide justice to u, and ready prepared to take your case to further stage
enjoy life and let wait to here from administration
 
If you refuse to take the shit in a back seat hakuna anaekuweza. Ina gharama lakini itakuwa ukombozi wako huo.
Kila la kheri. Usisikilize sana tetesi watakuharibia manake utaongea na watamrudishia maneno. Kuwa business like. Ukikutana nae muamkie shkamoo kubwa ukimtolea jicho. Unanikumbusha babangu wakati ananifundisha a firm handshake and eye contact. It gives the other person a clue of what you want. It has taken me miles i tell you.
 
Nimekuelewa King'asti ila c tetes za watu ila ni kutoka sehemu fulan hiv...nadhan umeelewa.Tuombe mungu
 
Part I niliisoma ila part II sikuisoma but nakupongeza sana kwa hatua uliyoifikia nadhani ni fundisho kwa watu wajinga kama huyu bwana!!!!!
 
Mungu muumba akutie nguvu, akupiganie na akushindie katika vita hii....
 
Be strong like ya name!

Mungu ndiye mweza wa yote na hashindwi na kitu, pigana best inakugharimu but utaokoa na wengine wengi ambao wangetumbukia ktk mikono ya huyo mzinzi!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
u need to be strong kama jina lako najua wengi wanapitia magumu kama hayo vyuoni mungu atakuongoza
 
Back
Top Bottom