Lazima ujifunze haya

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,339
51,879
LAZIMA UJIFUNZE MAMBO HAYA.

Anaandika Robert HERIEL
Yule Mtibeli.

Lazima ujifunze kuona pasipo kutumia macho.
Tena ujifunze kusikia pasipo kutumia masikio.
Kama haitoshi ujifunze kusema pasipo kutumia mdomo,
Kwa maana Maisha ni vita isiyohitaji hayo, tena ni mbio zisizohitaji Farasi.

Niite Taikon wa Fasihi, mkimbiza WAKATI.

Naye ayategemeaye macho yake hataona, na apendaye kusikia hatosikia.

Nawe usisubiri majibu Kama hukutafuta maswali.
Napo uwapo katikati ya maswali usilete majibu, nawe uwapo katikati ya majibu usiweke Maswali.

Ujifunze kulia na kuomboleza pasipo kutoa machozi na ukelele,
Nawe ujifunze kufurahi pasipo kutoa Tabasamu.

Ujifunze ishara, Alama na kuzisoma nyakati, Kwa maana hizo hazitoi sauti lakini zinasema, nazo zipo lakini wenye macho hawazioni, ndio maana nalikuambia ujifunze kuona pasipo macho, tena kusikia pasipo masikio.
Looh! Taikon nimejihangaisha sasa!

Ujifunze kuuficha ukweli Kwa wapumbavu, tena ujifunze kuufichua ukweli Kwa wenye Hekima. Wala usijeukachanganya mambo hayo.

Jifunze kuona njaa wakati WA chakula, tena ujifunze kuwa na chakula wakati wa njaa, Kama utaweza kujizuia nafsi yako utakuwa umeyaweza maisha, tena Kama utaweza kuyazuia matamanio yako, utakuwa umejiepusha na maanguko.

Jifunze kuujua ukweli uliojificha kwenye Hila. Nao ukweli uliojificha kwenye hila na njama kamwe haionekani Kwa macho wala kusikika Kwa masikio ndio maana nalikuambia ujifunze kuona pasipo macho, na kusikia pasipo masikio. Hivyo ndivyo utakavyoishi.

Ujifunze kuona Shaka nafasi yako itakapoona upo salama kwani hiyo ndio salimini yako. Kwa maana waovu huweka mazingira salama kusudi kuteka Imani yako kusudi wakuangushe Kwa ghafula. Hayo nayo nilikuambia.

Ujifunze kumfurahisha Mkeo hata akiwa na huzuni, tena ujifunze kumchukiza awapo na furaha iliyopitiliza.
Ujifunze ku-balance furaha na huzuni yake. Kwa maana furaha ya mke ikizidi huweza kuangusha Nyumba, na huzuni ya Mke ikizidi huleta machafuko na mauti.

Ujifunze kumpenda Mkeo hata akiwa anakuudhi, tena ujifunze kumchukia wakati akikufurahisha. Hivyo ndivyo namna Bora ya kuishi na Mke wako.
Usiache usiku ukawa mrefu kuliko mchana, wala usiache mchana ukawa mrefu zaidi ya usiku. Hayo nayo niliyasema.

Ujifunze mbio ndefu hata Kama wewe ni wambio fupi, tena ujifunze mbio fupi hata Kama wewe ni wambio ndefu.

Jifunze kuwa Yatima hata Kama unawazazi, tena ujifunze kuwa Mjane hata Kama Una mume. Hivyo ndivyo utakavyoishi.

Jifunze kuudhiwa, kukerwa, tena ujifunze kufanya mambo yako ukiwa chini ya shinikizo, ukiwa umepaniki au kupanikishwa, tena katika Hali hiyo ujifunze kutenda Kwa usahihi pasipo kuathiri matokeo.

Ujifunze kusema Ahsante haraka Kama haujaridhika, na ujifunze kutoshukuru hata Kama umeridhika.
Niseme nini tena???

Sasa Taikon ataenda kupumzika, Kwa leo hayo yakutoshe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
Unatupiga kamba mzee,hapa unapotosha umma wa watu kwenye ndoa.

Unatakiwa uweke reasons ama ushahidi wako kutilia nguvu jambo lako,hivi unasema tu kama nabii kana kwamba umepokea wahyi unatupiga kamba.
 
Mkuu ndivyo ilivyo
Wewe sio nabii,unapotoa hoja itetee unaposema ndivyo ilivyo bainisha kwamba ndivyo ilivyo kwako wewe na mkeo na sio kwa watu wote kaka.

Hii sio hoja ya kuiweka kutetea ishu yako,bado inaonekana unaandika kujifurahisha tu kaka,ni wazi huna uhakika na unachokisema
 
Mkuu Mimi ni mwanafasihi na mwanafalsafa huwaga hatutetei hoja, Bali tunatoa hoja ambazo wafuasi na wasio wafuasi ndio huzijadili.

Hakuna mwanafasihi au mwanafalsafa anayetoa hoja alafu aanze kuanzisha mijadala ya ubishani kuitetea.

Wasomaji na wasikilizaji watapaswa kuelewa Kwa kadiri ya Uelewa wao ulivyo.

Ukiona nimekosea ni Sawa, na ukiona sijakosea pia ni Sawa.

Ndivyo Fasihi ilivyo MKUU
 
Sawa mkuu.

Nimekusoma kwa ufafanuzi huu sikujua mwanzo
 
Mkuu ndivyo ilivyo habari za FASIHI.

Ndio maana huwezi mkuta mwanafasihi mahakamani akishtakiwa, maana ukisema umeelewa hivi yeye atakuambia alimaanisha vile hata Kama alimaanisha hivyo ulivyomaanisha wewe.

Fasihi na Falsafa.
Sawa kaka
 
Kwa wenzetu maelezo yote hayo wanatumia neno moja tu” SELF CONTROL = KIASI. neno hilo moja linatosha kwa maelezo hayo wenzetu wameendelea sana.. daah sisi sijui tutapata lini uelewa wa juu zaidi ya hapa.. ila Shukrani MZEE ila uzi mzuri sana UBARIKIWE
 
Uzi huu unaijaza na kuishibisha nafsi. Ni mzito mno kwa wenye macho na hisia za ndani. Mna jicho la tatu kwa ndani.
 
LAZIMA UJIFUNZE MAMBO HAYA.

Anaandika Robert HERIEL
Yule Mtibeli.

Lazima ujifunze kuona pasipo kutumia macho.
Tena ujifunze kusikia pasipo kutumia masikio.
Kama haitoshi ujifunze kusema pasipo kutumia mdomo,
Kwa maana Maisha ni vita isiyohitaji hayo, tena ni mbio zisizohitaji Farasi.

Niite Taikon wa Fasihi, mkimbiza WAKATI.

Naye ayategemeaye macho yake hataona, na apendaye kusikia hatosikia.

Nawe usisubiri majibu Kama hukutafuta maswali.
Napo uwapo katikati ya maswali usilete majibu, nawe uwapo katikati ya majibu usiweke Maswali.

Ujifunze kulia na kuomboleza pasipo kutoa machozi na ukelele,
Nawe ujifunze kufurahi pasipo kutoa Tabasamu.

Ujifunze ishara, Alama na kuzisoma nyakati, Kwa maana hizo hazitoi sauti lakini zinasema, nazo zipo lakini wenye macho hawazioni, ndio maana nalikuambia ujifunze kuona pasipo macho, tena kusikia pasipo masikio.
Looh! Taikon nimejihangaisha sasa!

Ujifunze kuuficha ukweli Kwa wapumbavu, tena ujifunze kuufichua ukweli Kwa wenye Hekima. Wala usijeukachanganya mambo hayo.

Jifunze kuona njaa wakati WA chakula, tena ujifunze kuwa na chakula wakati wa njaa, Kama utaweza kujizuia nafsi yako utakuwa umeyaweza maisha, tena Kama utaweza kuyazuia matamanio yako, utakuwa umejiepusha na maanguko.

Jifunze kuujua ukweli uliojificha kwenye Hila. Nao ukweli uliojificha kwenye hila na njama kamwe haionekani Kwa macho wala kusikika Kwa masikio ndio maana nalikuambia ujifunze kuona pasipo macho, na kusikia pasipo masikio. Hivyo ndivyo utakavyoishi.

Ujifunze kuona Shaka nafasi yako itakapoona upo salama kwani hiyo ndio salimini yako. Kwa maana waovu huweka mazingira salama kusudi kuteka Imani yako kusudi wakuangushe Kwa ghafula. Hayo nayo nilikuambia.

Ujifunze kumfurahisha Mkeo hata akiwa na huzuni, tena ujifunze kumchukiza awapo na furaha iliyopitiliza.
Ujifunze ku-balance furaha na huzuni yake. Kwa maana furaha ya mke ikizidi huweza kuangusha Nyumba, na huzuni ya Mke ikizidi huleta machafuko na mauti.

Ujifunze kumpenda Mkeo hata akiwa anakuudhi, tena ujifunze kumchukia wakati akikufurahisha. Hivyo ndivyo namna Bora ya kuishi na Mke wako.
Usiache usiku ukawa mrefu kuliko mchana, wala usiache mchana ukawa mrefu zaidi ya usiku. Hayo nayo niliyasema.

Ujifunze mbio ndefu hata Kama wewe ni wambio fupi, tena ujifunze mbio fupi hata Kama wewe ni wambio ndefu.

Jifunze kuwa Yatima hata Kama unawazazi, tena ujifunze kuwa Mjane hata Kama Una mume. Hivyo ndivyo utakavyoishi.

Jifunze kuudhiwa, kukerwa, tena ujifunze kufanya mambo yako ukiwa chini ya shinikizo, ukiwa umepaniki au kupanikishwa, tena katika Hali hiyo ujifunze kutenda Kwa usahihi pasipo kuathiri matokeo.

Ujifunze kusema Ahsante haraka Kama haujaridhika, na ujifunze kutoshukuru hata Kama umeridhika.
Niseme nini tena???

Sasa Taikon ataenda kupumzika, Kwa leo hayo yakutoshe.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
Ahsante sana mkuu.
Ujumbe mzuri.
 
Mdogo angu nakushukuru sana.Na jumapil hii nimetoka church basi nilipokua napita na andiko lako hili nikajiona kama nasoma kitabu cha Mithali au Muhubiri.
Umenibariki..
 
Back
Top Bottom