Lazima mke ashuke tu kwa mumewe vinginevyo hakuna ndoa

Kwahiyo una maana kuwa huo utandawazi mbovu umewakumba watoto wa kike tu? Si wapo na wa kiume ambao umewakumba au kwa watoto wa kiume ukiwakumba ni sawa?

Halafu unaposema eti ni lazima mwanamke ukitaka kumuoa umkuta anajua kufanya kazi za nyumbani zote unamaanisha nini? Unamaanisha kwamba hauwezi kumvumilia mwanamke ambaye hatatimiza majukumu yake si ndiyo?

Kwahiyo unataka kusema kwamba na sisi wanawake tusiolewe na wanaume ambao hawajui kutafuta pesa tusubiri wakishatafuta wakapata ndo tukaolewe nao si ndiyo? Maana hata sisi hatuwezi kuwavumilia wanaume ambao hawataweza kutimiza majukumu yao

Kwa mitazamo hii acha tu na sisi wanawake tuendelee kutafuta wanaume wenye pesa tu kwa kweli haiwezekani wanaume mshindwe kutimiza majukumu yenu kwa kisingizio cha kuwa hamna uwezo halafu mnataka wake zenu watimize majukumu yao yote tena wawasaidie na ya kwenu kabisa halafu nyie kuwasaidia ya kwao hamtaki mnaita umume bwege
 
Waache waendelee na mashindano si wanadhani kuna tuzo

Watu wenyew wako kibao afu waendelee kutuumiza kichwa ni kuwatumia na kuwatupa huko
Yaani mnavyoongeaga hizo kauli mnajikutaga miungu wenyewe mnadhani mnamkomoa nani sasa? Kwa Mungu mwanaume malaya na mwanamke malaya wote wana dhambi

Na kama ni kwenye jamii sidhani kama siku hizi wanawake tunajali tena jinsi tutakavyoonekana kwenye jamii yaani wanawake wa hivyo wamebaki wachache mno na ndo hao ambao wako tayari kuwa hata watumwa kwa wanaume ili tu waolewe lakini wengine tushashituka siku hizi

Ndoa anapanga Mungu na siyo binadamu na Mungu hakumleta mwanamke duniani aje ateseke wala kuwa mtumwa wa mwanaume na wala Mungu hakutaka ndoa zile za mwanamke kujifanya mjinga hata kama mumewe kakosea vipi

Dunia imeshabadilika siku hizi wanaume kubalianeni tu na hali halisi na kama mnaona kuwa hao wanawake mnawatumia endeleeni kujidanganya maana sidhani kama unaweza kusema eti unamtumia mtu ambaye anafanya kitu kwa raha zake
 
1. Rejea kichwa cha habari ujue kinataka nini.

2. Fungua uzi kuhusu Marioo ili ujenge hoja yako vizuri.

3. Pole kwa kuolewa na Mwanaume kilema wa akili/asiyetambua wajibu wake ktk ndoa.

4.Karibu tena.
 
Wanawake pitieni huku kuna tiba yenu huku, wasipokuelewa basi aliyewaroga atakuwa kafa.
 
1.Rejea kichwa cha habari ujue kinataka nini.

2.Fungua uzi kuhusu Marioo ili ujenge hoja yako vizuri.

3.Pole kwa kuolewa na Mwanaume kilema wa akili/asiyetambua wajibu wake ktk ndoa.

4.Karibu tena.
Mkuu siyo kila anayetetea vichaa basi na yeye ni kichaa hivyo basi siyo kwa sababu nimewatetea wanawake walioolewa na marioo basi na mimi nimeolewa na marioo kwanza kabisa mimi sijaolewa na mpenzi wangu naweza kusema anajitahidi sana katika kusimamia nafasi yake na kutimiza wajibu wake kwangu lakini nimeamua niwaseme wale wanaume ambao siku hizi nao wanatafuta wanawake ambao wana akili ya maisha au ambao wanajua kutafuta pesa

Ili wawasaidie hao wanaume kutafuta pesa na kuhudumia familia kumbe mnajua kuwa wanaume wa design hiyo wapo na ndo hao marioo sasa mbona hamuwasemi kutwa kutusema wanawake tu niamini mimi mwanamke akishaanza kuingilia majukumu ya mume wake lazima tu atakuwa na dharau huyo mume atake asitake na kama hataki basi ndo atimize majukumu yake yote kama mwanaume bila kusubiri mke amsaidie
 
Sisi tunatambua tangu muda mrefu,yaani mkituheshimu na kututii,hapo hakuna uchawi wala ndumba,sisi tutawapenda na kuwajali mpaka mjishangae
Tatizo kuheshimu na kutii mnakotaka nyie ni ile mkifanya makosa tukae kimya tusiongee chochote na mkiamua jambo basi ndo mmeamua hamtaki kukosolewa hamtaki kurekebishwa hamtaki kushauriwa wala hamtaki kuambiwa ukweli

Ndo heshima mnayoitaka hiyo si ndiyo? Halafu kwanini mwanamke ndo aanze kutii halafu mwanaume ndo afuate kupenda? Kwanini mwanaume ndo asianze kupenda halafu mwanamke akaanza kutii?

Biblia haijasema nani aanze ila kumbuka wanaume ndo mlianza kuumbwa na nyie ndo mnaotongoza sasa kama ambavyo mnataka muwe viongozi kwenye kila kitu tunaomba pia muwe viongozi hata kwenye mapenzi ninyi ndo muanze kuonyesha huo upendo halafu muone kama wake zenu hawatawaonyesha utii

Na tunaposema kupenda tunamaanisha ni pamoja na kutokusaliti wake zenu achaneni na huo utafiti uchwara kuwa eti mwanaume anaweza akamsaliti mume na bado akawa anampenda hakuna kitu ambacho kama hicho hivyo basi mwanaume anayemsaliti mkewe hatakiwi kupewa utii na mkewe sasa kwa sababu dunia ya sasa wanaume hamuwapendi wake zenu mnawasiliti basi ndo maana hata wanawake hawawatii waume zao wanawadharau
 
Umeongea meengi sana katika comment yako,ila kwa uvivu wangu wa kuandika naomba nikuambie machache.

Angalia namna unavyoongea na mmeo,sio unaongea kama uko saloon alafu unasema unashauri ,

Maandiko kamwe hayajipingi kasome tena,ilivyoandikwa katika Bible basi wewe yakupasa utekekeze ,na hapo utajua nani anapaswa kuanza kutekeleza hayo

Kuchepuka ile tafiti iko real, wanaume tunachepuka kwa kukata tamaa tu,ila mwanamke akichepuka kapenda kweli,na siri zote za ndani atatoa.

Hivyo mkitutii na kutuheshimu amini nakwambia hata bar nyingi zitakosa wateja. ,
 
Asante Chief
 
Kwahiyo ninyi hamuwezi kuanza kuwapenda wake zenu halafu wao ndo wakafuata kuwatii?
 
Kwahiyo ninyi hamuwezi kuanza kuwapenda wake zenu halafu wao ndo wakafuata kuwatii?
Toka tunapowatongoza automatically huwa sisi ndio tumeeaza kuwapenda, kinachosalia huwa ni wajibu wenu kutuheshim na kututii,na ukipunguza kimoja wapo basi lazima uhisi upendo unaanza kupungua.
 
Kama mume ananipenda basi hakika na mimi namtii hakuna hilo halina ubishi hapo
Upendo bila utii utoke wapi? Naweza kukupenda kama mke wangu ila huna utii hakiamungu usione huo upendo unaohitaji.
 
Haaa jamani siyo nyie mnaosemaga kwamba mkiwa mnatongoza ile mara ya kwanza mnakuwa hamjatupenda bali mnakuwa mmetutamani tu halafu upendo wenu utategemea na tabia za hao wanawake mliowatongoza?
Toka tunapowatongoza automatically huwa sisi ndio tumeeaza kuwapenda,kinachosalia huwa ni wajibu wenu kutuheshim na kututii,na ukipunguza kimoja wapo basi lazima uhisi upendo unaanza kupungua
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…