Lazima mke ashuke tu kwa mumewe vinginevyo hakuna ndoa

Ndiyo kanuni ya msingi.

Sema wanawake wengi wanasumbuliwa na mapokeo na ujinga ( kutokujua namna nzuri ya kuhusiana na Mwanaume).

Kuna ombwe kubwa kutokuwa na psychology ya mahusiano ya kimapenzi
 
Katika miaka ya karibuni kumekuwa na upungufu mkubwa wa wanawake wazuri. Kwa sura, shape au mwonekano hasa mijini.

Pengine hii inatokana na mabadiliko ya tabia ya nchi na ukweli kwamba watu siku hizi hawapati lishe bora kama walivyopata wazee wetu.

Kupungua kwa idadi ya wanawake wazuri hasa katika jiji la Dar Es Salaam' Mbeya nk kumeendana pia na ongezeko la wanawake wenye viburi, lugha mbaya, wabishi, wagomvi na kwa ujumla washamba wa mahaba.

Lugha mbaya inamfukuza mume nyumbani. Kiburi kinamkosesha mke zawadi. Gubu linamfanya mume ajifunze kwenda baa hata kama hiyo sio style yake.

Tabia ya kumchunga sana mumeo na kushindana nae kila mara huichimbia ndoa kaburini kama unaitaka ndoa yako basi usimjibu vibaya mumeo hasa mbele za watu na hasa rafiki zake.

Mpokee mumeo akirudi kazini hata kama umetingwa kiasi gani. Usimtume house girl kumpokea mzigo mumeo. Ni kosa la kiufundi.

Mwite mumeo kwa jina lake la kwanza. Usimwite 'wee' au 'huyu'. Siyo sahihi. Na mume vilevile usimwite mkeo wewe au huyu!!

Ndoa inastawi au kubomoka kwa vitu vidogo sana. Yanasema maandiko kwa mujibu wa Paulo: "Enyi wake watiini waume zenu. Nanyi wanaume wapendeni wake zenu"

Kuna amri kuu mbili za kuzingatia ili ndoa idumu.

Kwanza, ni lazima mke amheshimu na kumtii mumewe.

Pili ni wajibu wa mume kumtunza na kumthamini mkewe kwa kila hali. NB: Kulingana na uwezo wa mwanaume husika ni busara pia kwa mwanamke kuridhika na hali ya kiuchumi ya mumewe.

Mke akiwa na tamaa ni chanzo cha mifarakano katika ndoa. Kama huwezi kuvumilia hali yake ni bora muachane kuliko kumpa stress kila siku kaka wa watu.

Najua siku hizi wanawake wengi wana vipato vikubwa na wengine hiyo huwa sababu ya kuwadharau au kutaka kushindana na waume zao ukweli mchungu ni kwamba kama unataka ndoa lazima uwe submissive kwa mumeo.

Kama kipato kinawazuzua na mnaona hamuwezi kumtii mume ni bora akina dada wa aina hii waishi peke yao.
anashukaje kwa mfano, kwani ulimwoa akiwa juu? nijuavyo mimi, tangu akiwa mchumba tu sio mke anatakiwa kushuka awe chini, kwenye ndoa anaingia akiwa chini, akijaribu kuinua mabeta au kibichwa hakuna ndoa hapo.
 
Back
Top Bottom