Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lazima Lowassa ashitakiwe kwa Ufisadi!!

Lowassa lazima aende mahakamani
Hakuna ubishi
Huyu ni fisadi tena awamu hii lazima ashitakiwe
 
Basi,kumbe hata muheshimiwa spika alipewa huo ushahidi,yaani anaujua,sasa na yeye mbona kanyamaza nao sana?
 
Ni kweli lazima ashitakiwe kama mshtakiwa wa Kwanza. Hata Mimi pamoja na UKADA wangu naona dhahiri Richmond ilikuwa galasa la kisiasa kwa EL. Mwakyembe alifanya siasa na kamati yake ili kuweza kumwepusha MTU mwingine na kikombe kile. Basi apelekwe Mahakama ya Mafisadi akahukumiwe baada ya kuhukumiwa na Mwakyembe the lawyer..
Sasa mbona mwakyembe ndio ndio stering wa mahakama ya mafisadi?
 
Ni kweli lazima ashitakiwe kama mshtakiwa wa Kwanza. Hata Mimi pamoja na UKADA wangu naona dhahiri Richmond ilikuwa galasa la kisiasa kwa EL. Mwakyembe alifanya siasa na kamati yake ili kuweza kumwepusha MTU mwingine na kikombe kile. Basi apelekwe Mahakama ya Mafisadi akahukumiwe baada ya kuhukumiwa na Mwakyembe the lawyer..

Mkuu wangu huyo mwakyembe the laywer unayemsema hata ikitokea kesi ikafunguliwa (kitu ambacho hakiwezekani nadhani) na yeye akatakiwa kufika mahakamani kutoa ushahidi wake kama mwenyekiti wa kamati iliyochunguza sakata la Richmond....usitegemee kama ataonekana mahakamani..
 
Kiashiria cha udhaifu kwa binadamu wakati mwingine ni pale anaposhindwa kulifikisha mwisho jambo la muhimu analotakiwa kulikamilisha. Sisi kama taifa tumekuwa tunatangatanga na Jambo lililosababishwa na mtu mmoja tu na sisi kama taifa tumeshindwa kufikia mwisho wake.

Tarehe 7/2/2008 aliyekuwa Waziri wa Mkuu wa Tanganyika wakati ule, Edward Ngoyai Lowassa alijiuzulu wadhifa wake baada ya kutuhumiwa kuingilia mchakato wa Zabuni ya Ufuaji Umeme iliyosababisha kuletwa kwa Kampuni ya Ufuaji Umeme ya Richmond nchini. Tangu kujiuzulu kwa Lowassa mpaka sasa imeshapita miaka zaidi ya 8 na miezi kadhaa, lakini bado suala la sakata la Richmond halijaisha

Mitambo iliyoletwa na Kampuni ya Richmond ambayo bado ipo Pale Pale ilipofungwa na Kampuni ya Richmond, imeshabadilishwa umiliki wake mara mbili. Imetoka kwa Richmond ikanunuliwa na Dowans na sasa inamilikiwa na Kampuni ya Symbion ya Marekani. Lakini sisi kama taifa tumeachwa pale pale tulipokuwa Mwaka 2008.

Kwa kuwa kuna Mahakama ya Mafisadi inaundwa na sisi kama taifa tunayumbishwa na suala la mtu mmoja tu, ambaye si kiongozi wa serikali kwa sasa, nashauri Kesi ya Kwanza kwenye Mahakama ya Mafisadi iwe ni hii ya "Ufisadi" wa Edward Ngoyai Lowassa kuhusu Ufisadi wa zabuni ya ufuaji umeme iliyosababisha Sakata la richmond.

Ni lazima Lowassa ashitakiwe ili kama yeye anao ushahidi tofauti na ule ambao wapinzani wake wanao aje nao mahakamani ili upimwe kwenye mizani ya kisheria tujue nani mkweli kati yake yeye na wapinzani wake.

Haiwezekani mitambo ile iliyoletwa na Kampuni (Feki?) ya Richmond bado ipo nchini mwetu, inafua umeme, Tannesco wanalipa Capacity charges tanesco wanauziwa umeme kutokana na mitambo ile ile iliyokuwa ya Richmond, mkataba ule ule wa kati ya Richmond na Tannesco ndiyo umekuwa ukihuhishwa na Dowans na sasa Symbion, lakini sisi kama taifa bado tunakumbushana mambo ya mwaka 2008.

Kuukata Mzizi wa fitina ni lazima Lowassa na kama wapo na wengine waliohusika na sakata la Richmond wafikishwe kwenye Mahakama ya mafisadi mara tu Mahakama hiyo itakapoanza kazi. Tunataka Kesi ya kwanza kwenye mahakama hiyo iwe dhidi ya Lowassa na wenzake waliohusika na suala la Richmond.

KESI YA LOWASSA ISIPOKUWA YA KWANZA KWENYE MAHAKAMA YA MAFISADI NITASHANGAA KWELI KWELI!!

Kuna watu walijenga political career yao kwa kumnanga Lowassa na ufisadi. Leo hii wako juu na wanaimba nyimbo tofauti. Pengine bila kelele zao leo hii Lowasa angekuwa kiongozi wa nchi hii. Hao watu ndo inatakiwa watumie kila linalowezekana kumsafisha. Najua kama ni msamaha walishamuomba. Lakini tuamini nini juu ya wale wanaoendelea kuwananga leo kuwa ni "madikteta uchwara". Waangalieni kwanza hao, kabla ya kushauri ashitakiwe. Hapo mnataka wegine ndo wafanye kazi ya kumsafisha, wakati waliomchafua leo wamepumzika chini ya mwavuli wake; tena wanaendelea kuchafua wengine! Siasa za kuchafuana zimewajenga; kwa kuwabomoa wengine! Mliowabomoa leo mnataka wengine wawasaidie kuwajenga.
 
Basi,kumbe hata muheshimiwa spika alipewa huo ushahidi,yaani anaujua,sasa na yeye mbona kanyamaza nao sana?
Yule naye alinyamaza kwa maslahi yake ya baadaye. Na kumbuka wakati ule wa "wanamtandao" naye alikuwemo na kama vile alikuwa amejitayarisha kupata wala nafasi ya kumrithi Jakaya. alikosea step hapo katikati!!
 
Nasikia serikali ilivunja mkataba na Dowans, nao Dowans hawakukubali wakaenda mahakamani ambako Tanzania iliamriwa kulipa mapesa kibao kwa Dowans na hakuna mtu anyehoji hilo hapo, tuna akili au tumerogwa?
Dowans alipolipwa akamuuzia Symbion mitambo hiyo ambayo, hadi kesho inadunda bila wasiwasi.

Hii inanikumbusha kesi ya minofu ya samaki na meli ya wachina. Tanzania ilipona na hapo au iliamriwa kuwalipa fidia wachina! Nani alikuwa front kwenye sakata hilo?? Mijitu haihoji vitu vya msingi inakalia ushabiki wa kisiasa tu.

Nasikia kiu ngoja niende Kebby's Hotel nipate moja baridi.
 
Kuna watu walijenga political career yao kwa kumnanga Lowassa na ufisadi... Waangalieni kwanza hao, kabla ya kushauri ashitakiwe.
Usisiasishe hoja bwana, hao wanaochafuana kwenye siasa labda ndiyo mchezo wao unavyochezwa. Sisi hapa tunataka sheria ifuate mkondo wake. Lowassa ashitakiwe, Full stop!!
 
Yule naye alinyamaza kwa maslahi yake ya baadaye. Na kumbuka wakati ule wa "wanamtandao" naye alikuwemo na kama vile alikuwa amejitayarisha kupata wala nafasi ya kumrithi Jakaya. alikosea step hapo katikati!!
Hii thamthilia ni kali kinomanoma
 
Hayo ndiyo maneno!!

Ngoja tujikumbushe hii


OKW BOBAN SUNZU - Nov 26, 2011


CHADEMA Okoa Tanzania Dhidi ya Janga Lowassa Richmond

OKW BOBAN SUNZU Anasema

""CHADEMA kama chama cha wananchi wanyonge, mmetumia mda mwingi kupambanua majanga makuu ya watu wanaoangamiza taifa letu ikiwepo Lowassa na wananchi wamesikia sauti zenu, hivyo tunawaomba kwa nguvu ile ile muitaadharishe jamii juu ya Janga Lowassa kwani kuna kila dalili za kufanya ikulu iendelee kuwa pango la wanyanganyi. Shame on him and his followers""



WAFUASI WA CDM WACHENI UNAFIKI
 
Back
Top Bottom