Lazaro Nyalandu, kinyongo cha Uwaziri kitakuponza

Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida ametajwa kuwa na kinyongo cha kupitiliza Kutokana na kutoswa Kwenye Uwaziri Kwenye serikali ya awamu ya tano imebainika. Kati ya mawaziri wa Kikwete wanaoumia huyu bwana anashika nafasi ya kwanza.

Baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na Nyarandu kutoingizwa Kwenye Baraza la mawaziri lá Magufuli, huyu bwana alisuka mkakati kuwashawishi Maseneta 7 wa Marekani kuja Tanzania kuonana na Rais Magufuli kuzungumza masuala yanayotajwa ya Kimaendeleo na kumshawishi Rais amteue Nyarandu Kwenye Wizara ya Maliasili ili Marekani iendelee kushirikiana na Tanzania Kwa kutoa misaada ya vifaa vya kudhibiti ujangili nchini.

Mtakumbuka Rais Magufuli aligundua janja hiyo anakataa kuonana na hao wazungu wa Marekani badala yake alielekeza wakaonane na Spika Ndugai Waeleze mambo yao. Kitendo chá Maseneta hao waliokuja na Ndege binafsi kutomuona Rais kiliwakatisha tamaa sana Kwakuwa Ndugai hakuwa mlengwa.

Hata Wakati wa kikwete kumpandisha Nyarandu kuwa Waziri baada ya kujiuzulu Kagasheki ilikuwa ni Shinikizo la Western power, hii iliwahi kuripotiwa na Gazeti Jamhuri mara kadhaa.

Marekani wanamtaka Nyarandu Kwa sababu za maslahi ya Vitalu vya uwindaji na masuala yote yanayohusiana na bidhaa za wanyama Pori . Huyu ni mtu Pekee aliyeweza kucheza fitina zote kuwaridhisha Matajiri wa kimarekani Kwa kukana maslahi ya taifa lake.

Mdogo wake Nyarandu nimesoma Naye sheria tukiwa darasa moja na hadi leo tuko karibu sana, Pamoja na kutomkubali Kaka yake Kwa madai kwamba hana msaada kwa ndugu zake, Anaeleza jinsi Nyarandu alivyokuwa na matumaini ya kurejea Kwenye uwaziri baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiamini ana nguvu kubwa nyuma yake. Kwahiyo kitendo chá kuachwa mazima kimjengea kinyongo kupita maelezo na amenukuliwa akimnanga Rais Magufuli na Rc Makonda kwamba sio Viongozi wenye maono.

Hamad ikatokea ile Ajali ya watoto wa Lucky Visent, Wazungu waliokuwa safari Kwenda Karatu wakakutana na Ajali mbaya ya gari lá wanafunzi iliwabidi washuke na kuokoa wale Majeruhi na kuwakimbiza Hospitali Arusha, wale wazungu Kwa kushuhudia Ajali ile mbaya waliingiwa na huruma na kujitolea kuwapeleka wale watoto Marekani kutibiwa, Nyarandu alichomoka kusikojulikana akaingia kati na kujifanya Msemaji wa wa jambo lile Kwakuwa alikuwa anafahamiana na Wazungu wale. Akajipatia sifa kwamba yeye ndiyo kawapeleka Wale watoto Marekani. Mpaka wale watoto wanarudi na kupokelewa Kwa Sherehe pale KIA hakuna Pongezi toka Kwa waziri yeyote , Waziri mkuu, CCM wala Rais Magufuli Kwenda Lazaro Nyarandu. Walijua janja yake.

Ni katika mlolongo huo huo wa kinyongo cha bwana huyu, Mwezi Julay Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Alikuwa na Ziara mkoani Singida kuzindua barabara ya Itigi -Tabora, Wabunge wote wa CCM mkoani Singida walihudhuria Ziara hiyo isipokuwa Nyarandu hakwenda Kwenye Ziara ya Rais Ndani ya mkoa wake na alikuwepo Arusha amechil tu.

Hamad Tundu Lissu akapata matatizo ya kupigwa Risasi, Mbunge wa wa CCM Turky akasaidia Kwa malikauli Ndege iende Dodoma kumbeba Lissu na kumpeleka Nairobi, yule mbunge amepongezwa na Spika wa Bunge na CCM makao makuu walimpongeza Kwa maandishi Kwa kitendo chá Uungwana kusaidia Ndege ya kumbeba Tundu Lissu.

Ghafla Nyarandu akaibukia Nairobi kumtembelea Tundu Lissu na kutoa kauli tata akiwa na Wabunge wa CHADEMA. "Muelekeo ni mhimu kuliko kasi, wengi hawajui waendako lakini wana kwenda kwa kasi! Ndio maana ni bora inchi moja kwenda kwenye muelekeo sahihi kuliko maili moja kwenda kwenye muelekeo usio sahihi" alisema Nyarandu.

kabla hajaruhusiwa kuingia ndani ya Hospital kumuona Tundu Lissu Nyarandu alipiga picha Kwenye kibao chá Hospitali na kupost mitandaoni haraka hata Kabla hujamuona mgonjwa. Hii inaashiria Lengo lake ni kuonekana ameenda huko ila sio dhamira ya dhati kumuona mgonjwa, wabongo wanaita kutafuta kiki. Na ameipata kiki aliyokuwa anaitafuta. Ila maneno aliyotoa huko Nairobi na Mengine nayahifadhi ni ishara ileile ya kinyongo chake.

MUDA WA KUMJUA WAZIRI JANGILI UMEFIKA?

Gazeti Raia mwema na Jamhuri walitoa ripoti Maalum ya kurasa 7 kuelezea Ujangili unaofanywa na waziri asiyefahamika katika awamu ya nne, ujangili wa waziri huyo Ulikuwa wa waziwazi na Ushahidi uliwekwa. Waziri huyo aliyetajwa kutumia Helicopter kubeba meno ya Tembo maeneo ya Manyoni na kuyapeleka kusikojulikana. Rais Magufuli baada ya kumulika sekta ya madini hamia na Kwenye Maliasili tuwajue wanaohujumu taifa letu.

Itaendelea..............
Kanye ukalale propaganda za kitoto hizo
 
Nyalandu hakuzaliwa kuwa waziri .Hata huyo JPM hatakuwa Raisi wa maisha.kwanza kuwa waziri kwenye serikali hii ya awamu ya tano nikujidhalilisha nakuwa kama waziri kivuli maana serikali hii ni ya Raisi peke yake yeye ndiyo kila kitu.
 
Kiongozi anayesubiri sifa na kiki kupitia Majeruhi ni kimeo, sifa za huruma ni za msimu tu hizo. Leadership is all about Legacy.

Cheap popularity.
 
Tutafunua mambo mazito, Stay tuned hapa hapa. Kibaraka Huyu ni mlaini na mwepesi sana kuliko hata Basil Mramba na Yona.
 
Haya umemsema Lazaro Nyalandu kwakuwa tu hivi majuzi ameenda kumtembelea Tundu Lissu Hospitalini kuwa ana hasira ya kukosa Cheo katika Serikali ya Rais Magufuli na je vipi kwa Jaji Mstaafu Mzee Chande Othman ambaye na yeye juzi pia alimtembelea Tundu Lissu Hospitali?

Wewe ndiyo mmoja wa wale wana CCM ' Wapumbavu ' na wenye roho mbaya iliyojaa ' Ukatili ' hata wa kumzidi Muasisi wa ' Ukatili ' duniani ' Gaidi ' Osama Bin Laden. Na kama CCM yetu itaendelea kuwa na Watu ' makatili ' kama Wewe mwaka 2020 Kazi tunayo kwani nyie ndiyo mtakuwa ' alama ' Kuu ya chukizo la Wananchi Kwetu ( namaanisha CCM )

Halafu nikuonye tu kwamba wakati ' ukiwashwawashwa ' kumsema Lazaro Nyalandu kuwa ni mmoja wa ' Mafisadi ' au Watu walioiibia hii nchi jitahidi uwe na kumbukumbu nzuri kwani kuna Viongozi wako hapo tena wanatoka katika hiki hiki Chama chetu Tawala cha CCM ambao ni ' Mafisadi ' wakubwa na ndiyo hao hao wameifilisi nchi hii vibaya mno tokea miaka ya 90 hadi 2000 hapo mbona nao hujawasema? au huwajui? au unawaogopa?

Mimi ni Mwana CCM mwenzio na ' nakuchana ' mubashara / live kuwa acha kuwa na roho ya Kimasikini kama hiyo uliyonayo. Lililomtokea Tundu Lissu laweza kumtokea Mwanasiasa yoyote hata aliye Kwetu huku CCM? Pumbavu kweli Wewe tena ndiyo umenipandisha hasira na umeshaniharibia asubuhi yangu.

Mbona wanapougua Viongozi wetu wa CCM hawa hawa Watu wa CHADEMA huwa wanaenda kuwajulia hali huko Mahospitalini? Hivi leo Tanzania tumefikia hatua kwamba hadi Mtanzania mwenzetu wa Chama fulani akiugua basi Wewe wa Chama fulani hutakiwi kwenda na kama ukienda unaambiwa ' Msaliti ' au unaambiwa una ' Kisirani ' cha kukosa wadhifa / madaraka fulani?

Hakuna Member aliyenitibua ' akili ' zangu leo kama Wewe na nitaomba wana CHADEMA wasipoteze muda wao kukujibu ila waniachie Mimi mwana CCM mwenzako nikunyooshe vizuri humu ili siku zingine ujifunze kujua kwamba katika shida au tatizo lolote Watanzani huwa tunaungana na kuwa Mtu mmoja.

Najua utarudi tu sasa nakusubiri ili nikushushie rasmi ICBM langu la kisawasawa. Umenikera kunakotukuka asubuhi hii.
ww sio CCM wala nini? unatumia kama vazi la nje ila ndani ni CDM, so ntakujibu kama CDM......

ujue nn mdau, kila anaewasapoti nyie chadema mnamuona mwema, ila angalieni huu sio wakati wa kumtetea kila mtu anaeonekana yuko upande wenu, mnafuga majibwa humo, shauri yenu....kazi kutokwa na mapovu tuu mtandaoni kwa kutetea chama ambacho ukiangalia kwa undani hakina mapenzi ya dhati kwa watu

kiongozi kama kiongozi inambidi awe mzalemdo na nchi yake na asiwe biased na chama chochote, tatizo uyo nyalandu alivokosa uongozi ktk awamu hii ndo mana anaside na CDM ili kutoa duku duku lake, ila km amgekua real fighter angeyasema ayo ndani ya chama chake, ila kwasababu ya unafiki na uoga wake ndo mana ameyafanya ayo(sio kiashiria cha kiongozi mzuri, ni mtu wa kupenda vyeo na uongozi tuu)

(Hakuna Member aliyenitibua ' akili ' zangu), ukielewa maana halisi ya mtoa post huwezi kusema maneno yanaoonesha upungufu wa kuawaza kama ayo
"grow up"
 
Nyarandu Jimbo lake amewafanya wapiga kura wake Kuwa masikini wa kutupwa, Jimbo zima ni giza tupu, mavumbi matupu, miaka 20 akiwa mbunge hakuna hata jambo moja la Kujivunia alilofanya. Amejitajirisha na kuishi maisha ya anasa hapa Arusha. Chadema leo mnamshabikia huyu Jangili na mhujumu uchumi Kisa kwenda kupiga picha Nairobi? Hopeless kabisa
 
KISA CHA YOTE HAYA NI KUONESHA MSHIKAMANO NA WENYE UTU WALIOUNGANA KUMPIGANIA LISSU.!
 
Lazaro Nyarandu mbunge wa Singida ametajwa kuwa na kinyongo cha kupitiliza Kutokana na kutoswa Kwenye Uwaziri Kwenye serikali ya awamu ya tano imebainika. Kati ya mawaziri wa Kikwete wanaoumia huyu bwana anashika nafasi ya kwanza.

Baada ya serikali ya awamu ya tano kuingia madarakani na Nyarandu kutoingizwa Kwenye Baraza la mawaziri lá Magufuli, huyu bwana alisuka mkakati kuwashawishi Maseneta 7 wa Marekani kuja Tanzania kuonana na Rais Magufuli kuzungumza masuala yanayotajwa ya Kimaendeleo na kumshawishi Rais amteue Nyarandu Kwenye Wizara ya Maliasili ili Marekani iendelee kushirikiana na Tanzania Kwa kutoa misaada ya vifaa vya kudhibiti ujangili nchini.

Mtakumbuka Rais Magufuli aligundua janja hiyo anakataa kuonana na hao wazungu wa Marekani badala yake alielekeza wakaonane na Spika Ndugai Waeleze mambo yao. Kitendo chá Maseneta hao waliokuja na Ndege binafsi kutomuona Rais kiliwakatisha tamaa sana Kwakuwa Ndugai hakuwa mlengwa.

Hata Wakati wa kikwete kumpandisha Nyarandu kuwa Waziri baada ya kujiuzulu Kagasheki ilikuwa ni Shinikizo la Western power, hii iliwahi kuripotiwa na Gazeti Jamhuri mara kadhaa.

Marekani wanamtaka Nyarandu Kwa sababu za maslahi ya Vitalu vya uwindaji na masuala yote yanayohusiana na bidhaa za wanyama Pori . Huyu ni mtu Pekee aliyeweza kucheza fitina zote kuwaridhisha Matajiri wa kimarekani Kwa kukana maslahi ya taifa lake.

Mdogo wake Nyarandu nimesoma Naye sheria tukiwa darasa moja na hadi leo tuko karibu sana, Pamoja na kutomkubali Kaka yake Kwa madai kwamba hana msaada kwa ndugu zake, Anaeleza jinsi Nyarandu alivyokuwa na matumaini ya kurejea Kwenye uwaziri baada ya uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015 akiamini ana nguvu kubwa nyuma yake. Kwahiyo kitendo chá kuachwa mazima kimjengea kinyongo kupita maelezo na amenukuliwa akimnanga Rais Magufuli na Rc Makonda kwamba sio Viongozi wenye maono.

Hamad ikatokea ile Ajali ya watoto wa Lucky Visent, Wazungu waliokuwa safari Kwenda Karatu wakakutana na Ajali mbaya ya gari lá wanafunzi iliwabidi washuke na kuokoa wale Majeruhi na kuwakimbiza Hospitali Arusha, wale wazungu Kwa kushuhudia Ajali ile mbaya waliingiwa na huruma na kujitolea kuwapeleka wale watoto Marekani kutibiwa, Nyarandu alichomoka kusikojulikana akaingia kati na kujifanya Msemaji wa wa jambo lile Kwakuwa alikuwa anafahamiana na Wazungu wale. Akajipatia sifa kwamba yeye ndiyo kawapeleka Wale watoto Marekani. Mpaka wale watoto wanarudi na kupokelewa Kwa Sherehe pale KIA hakuna Pongezi toka Kwa waziri yeyote , Waziri mkuu, CCM wala Rais Magufuli Kwenda Lazaro Nyarandu. Walijua janja yake.

Ni katika mlolongo huo huo wa kinyongo cha bwana huyu, Mwezi Julay Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli Alikuwa na Ziara mkoani Singida kuzindua barabara ya Itigi -Tabora, Wabunge wote wa CCM mkoani Singida walihudhuria Ziara hiyo isipokuwa Nyarandu hakwenda Kwenye Ziara ya Rais Ndani ya mkoa wake na alikuwepo Arusha amechil tu.

Hamad Tundu Lissu akapata matatizo ya kupigwa Risasi, Mbunge wa wa CCM Turky akasaidia Kwa malikauli Ndege iende Dodoma kumbeba Lissu na kumpeleka Nairobi, yule mbunge amepongezwa na Spika wa Bunge na CCM makao makuu walimpongeza Kwa maandishi Kwa kitendo chá Uungwana kusaidia Ndege ya kumbeba Tundu Lissu.

Ghafla Nyarandu akaibukia Nairobi kumtembelea Tundu Lissu na kutoa kauli tata akiwa na Wabunge wa CHADEMA. "Muelekeo ni mhimu kuliko kasi, wengi hawajui waendako lakini wana kwenda kwa kasi! Ndio maana ni bora inchi moja kwenda kwenye muelekeo sahihi kuliko maili moja kwenda kwenye muelekeo usio sahihi" alisema Nyarandu.

kabla hajaruhusiwa kuingia ndani ya Hospital kumuona Tundu Lissu Nyarandu alipiga picha Kwenye kibao chá Hospitali na kupost mitandaoni haraka hata Kabla hujamuona mgonjwa. Hii inaashiria Lengo lake ni kuonekana ameenda huko ila sio dhamira ya dhati kumuona mgonjwa, wabongo wanaita kutafuta kiki. Na ameipata kiki aliyokuwa anaitafuta. Ila maneno aliyotoa huko Nairobi na Mengine nayahifadhi ni ishara ileile ya kinyongo chake.

MUDA WA KUMJUA WAZIRI JANGILI UMEFIKA?

Gazeti Raia mwema na Jamhuri walitoa ripoti Maalum ya kurasa 7 kuelezea Ujangili unaofanywa na waziri asiyefahamika katika awamu ya nne, ujangili wa waziri huyo Ulikuwa wa waziwazi na Ushahidi uliwekwa. Waziri huyo aliyetajwa kutumia Helicopter kubeba meno ya Tembo maeneo ya Manyoni na kuyapeleka kusikojulikana. Rais Magufuli baada ya kumulika sekta ya madini hamia na Kwenye Maliasili tuwajue wanaohujumu taifa letu.

Itaendelea..............
TABIA ZA KIKE SIO NZURI,KWENYE UKWELI TUWE WA KWELI ,KAMA TABIA YA KUPENDA WATU AU NDUGU ANAYO YEYE HUWEZI KUMZUIA ,wengine mmeshachanganyikiw na vihela vya CCM na UFISADI pia kuna watu humu wana roho za ushetani ni ndugu na wale waliompiga Lisu risasi hivyo tabia yenu haiwei kutuambukiza mtabaki wa kuwa wa shetan tu na sisi tutabaki kuwa Mungu TU,KUNA WATU wana imani na Mungu wao waache wahudumie wanapostahili na wanaona wanastahili kuhudumia,nyie wenye roho za ushetani endeleen hivyo hvy mwenzenu kuumia ni furaha kwenu,NIKUHAKIKISHIE KTK 1000000 nyie mpo 6 au 7 wenye roho za ushetani,hata mkuu JPM mwenyewe alionyeshwa kuumizwa na tukio la LISSU,hongera LAZARO Mungu atakuongezea na kukuzidishia kwan mbinguni utaenda peke yako hata ukifa utakuwa peke yako,acha hao wasiomjua Mungu wandeleze ushetani wao.Mungu mbariki Lazaro pia uwabariki watz wote wanaomuombea na kumonea huruma Lissu.
 
Lumumba uzuri wenu huwa mnaandika pumba.....kwani ni lazima kumpenda sizonje hata kama mpo chama kimoja...?
 
ww sio CCM wala nini? unatumia kama vazi la nje ila ndani ni CDM, so ntakujibu kama CDM......

ujue nn mdau, kila anaewasapoti nyie chadema mnamuona mwema, ila angalieni huu sio wakati wa kumtetea kila mtu anaeonekana yuko upande wenu, mnafuga majibwa humo, shauri yenu....kazi kutokwa na mapovu tuu mtandaoni kwa kutetea chama ambacho ukiangalia kwa undani hakina mapenzi ya dhati kwa watu

kiongozi kama kiongozi inambidi awe mzalemdo na nchi yake na asiwe biased na chama chochote, tatizo uyo nyalandu alivokosa uongozi ktk awamu hii ndo mana anaside na CDM ili kutoa duku duku lake, ila km amgekua real fighter angeyasema ayo ndani ya chama chake, ila kwasababu ya unafiki na uoga wake ndo mana ameyafanya ayo(sio kiashiria cha kiongozi mzuri, ni mtu wa kupenda vyeo na uongozi tuu)

(Hakuna Member aliyenitibua ' akili ' zangu), ukielewa maana halisi ya mtoa post huwezi kusema maneno yanaoonesha upungufu wa kuawaza kama ayo
"grow up"

Foolish.
 
Kati ya ex-mawaziri ambao siwafahamu uzuri ni Nyalandu. Ila kama ni fisadi hivyo unavyodai mtakatifu Yohana kwa jinsi apendavyo kiki angekua anamuangalia tu mpk leo??
 
Back
Top Bottom