Lazaro Mambosasa aondolewe Dar es Salaam

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,626
Reaction score
272,402
Huu ni wito ambao naupeleka kwa IGP Sirro .

Anayotenda RPC Mambosasa DSM hayana tofauti na aliyotenda Aliyekuwa RPC wa Iringa aliyeitwa Michael Kamuhanda , huyu alisimamia kikamilifu mauaji ya mwandishi wa Channel 10 marehemu Mwangosi , Na kwa kutumia busara ya hali ya juu IGP wa wakati ule bila ya kuchelewa alimng'oa Kamuhanda na kumpeleka Makao Makuu.

Kila mwenye macho amejionea mwenyewe kauli ya jeshi la polisi kukiri kuhusika na mauaji ya mwanafunzi wa NIT , haya ni miongoni mwa mauaji ya kishamba sana kuwahi kufanywa na jeshi la polisi , yaliojaa uzembe wa kiwango kisichopimika , ni mauaji ambayo hata jambazi bwege hawezi kuyafanya .

Ni wakati sasa wa IGP kumpeleka Mambosasa Makao Makuu ili kurudisha amani jijini DSM , ambayo imetoweka moja kwa moja tangu kuingia kwa Mambosasa.

Angalizo - Si kila polisi anaweza kuwa IGP wa DSM .

- KumbukiziMTAFUTANO.jpg
 
Wewe unasema aondolewe ukamanda wa Jijini Dar??

Usije shangaa akaukwaa u-IGP!

Umesahau yaliyotokea kule Arumeru?

Ambako mkuu wa wilaya ile Alexander Mnyeti alipandishwa cheo na kuwa RC wa Manyara, licha ya clip za kina Nassari zilizomuonyesha mkuu huyo wa wilaya "akiwahonga" madiwani wa Chadema!

Hii ndiyo staili mpya ya Utendaji kazi ya wateule wa Rais, mfurahishe Bosi upande cheo!
 
Kwani mkuu wa Nchi ametoa tamko gani kuhusu watu kutekwa, matukio ni mengi, hadi jana dada yetu mwanachuo ametutoka, kura zinabadirishwa, mabox mengine yanaibiwa,. Ngoja tuanze na hapo kwanza
 
Kuondolewa itabadilisha nini? Ndo maana huwa haya maabano yenu yanaishia hewani tu. Mnaji distract halafu kuelekeza energy pasipo. Sad

Tunatakiwa tuzungumzie uwajibishwaji na watu wafunguliwe mashtaka nk. Sasa kuanza kutoa ushauri kwa watu wanaowauwa?
 
Maadui wa Taifa Wapo busy kuhakikisha kuwa wanavuruga amani ya nchi yetu; kiluchotokea Jana kinondoni ni matunda ya kazi zao.
 
Uyo muda si mrefu anapandishwa kua Kamishna kumbuka Mkuu aa Kanda Maalum mara nyingi anakuaga Kamishna....so hapo uyo SACP Mambosasa anasubiria kupandishwa kua CP
 
Huu ni wito ambao naupeleka kwa IGP Sirro .

Anayotenda RPC Mambosasa DSM hayana tofauti na aliyotenda Aliyekuwa RPC wa Iringa aliyeitwa Michael Kamuhanda , huyu alisimamia kikamilifu mauaji ya mwandishi wa Channel 10 marehemu Mwangosi , Na kwa kutumia busara ya hali ya juu IGP wa wakati ule bila ya kuchelewa alimng'oa Kamuhanda na kumpeleka Makao Makuu.

Kila mwenye macho amejionea mwenyewe kauli ya jeshi la polisi kukiri kuhusika na mauaji ya mwanafunzi wa NIT , haya ni miongoni mwa mauaji ya kishamba sana kuwahi kufanywa na jeshi la polisi , yaliojaa uzembe wa kiwango kisichopimika , ni mauaji ambayo hata jambazi bwege hawezi kuyafanya .

Ni wakati sasa wa IGP kumpeleka Mambosasa Makao Makuu ili kurudisha amani jijini DSM , ambayo imetoweka moja kwa moja tangu kuingia kwa Mambosasa.

Angalizo - Si kila polisi anaweza kuwa IGP wa DSM .
Kumuondoa tuu haitoshi anatakiwa ashtakiwe kwa mauaji.
 
Kuondolewa itabadilisha nini? Ndo maana huwa haya maabano yenu yanaishia hewani tu. Mnaji distract halafu kuelekeza energy pasipo. Sad

Tunatakiwa tuzungumzie uwajibishwaji na watu wafunguliwe mashtaka nk. Sasa kuanza kutoa ushauri kwa watu wanaowauwa?
Hii ni hatua ya kwanza mjomba , kuna kitakachofuatia .
 
mlisema uchaguzi huu hamtakubali kuibiwa kura, imekuwaje tena?
 
nimemsikia anasema jeshi la polis ndio linalosimamia uchaguzi jamani mi napenda kuuliza hivi siku hizi kumbe uchaguzi unasimamiwa na jesh la policy na sio tena tume ya uchaguzi..
 
Back
Top Bottom