Laweza kuwa kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laweza kuwa kweli?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mzee Mwanakijiji, Sep 30, 2008.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Sep 30, 2008
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,071
  Likes Received: 5,209
  Trophy Points: 280
  Mwandishi Maalumu, New York
  Daily News; Tuesday,September 30, 2008 @00:02
  Habari nyingine

  Tanzania itatokomeza kabisa ugonjwa wa malaria katika miaka saba ijayo, yaani ifikapo mwaka 2015, kwa kutumia njia tatu zilizothibitishwa kimataifa kuwa zinamaliza ugonjwa huo, Rais Jakaya Kikwete alisema hayo juzi mjini hapa.

  Vile vile, amesema kuwa ziara yake kwenye Umoja wa Mataifa (UN) mjini New York imekuwa ya manufaa makubwa kwa sababu Afrika imefanikiwa kuwasilisha sauti yake katika masuala muhimu yanayohusu Bara hili. Rais Kikwete aliondoka hapa jana kurejea nyumbani.

  Akizungumza na waandishi wa habari wa Tanzania walioandamana naye katika ziara hiyo kuhusu mafanikio ya ziara hiyo, Rais Kikwete alisema moja ya mafanikio ya ziara yake ni kwamba Tanzania imepata uhakikisho kuwa itatokomeza malaria ifikapo mwaka 2015.

  Alisema ahadi mpya za kupambana na matatizo ya Afrika, ukiwamo mwelekeo mpya wa kupambana na magonjwa na hasa malaria, inayoua watu wengi zaidi Afrika, ni moja ya mafanikio ya ziara yake UN.

  “Katika Tanzania, tunapambana na malaria kwa njia tatu zinazokubalika duniani, kuhakikisha kuwa wananchi wetu wanatumia vyandarua vyenye dawa, tunanyunyizia dawa za kuua mbu katika madimbwi ya maji, na pia kuhakikisha kuwa wagonjwa wanapata dawa,” alisema Raia Kikwete katika mahojiano hayo kwenye Hoteli ya Intercontinental jijini New York.

  Alisema njia zote tatu tayari zimeleta mafanikio makubwa Zanzibar ambako vifo kutokana na malaria vimeteremka mno, kutoka vifo 120,000 hadi 60,000 tu kwa mwaka. “Na mafanikio hayo yanatokana na matumizi ya asilimia 40 tu ya vyandarua Tanzania Visiwani, lakini Zanzibar haiwezi kutokomeza malaria bila kuhakikisha kuwa Bara nayo inakuwa salama.

  Hii ni mara ya tatu, tunafikia hatua ya kutokomeza malaria Tanzania Visiwani na bado ugonjwa huo umerejea kwa sababu Bara haitiliwa maanani,” alisema Rais Kikwete. Alisema Tanzania inahitaji kiasi cha vyandarua milioni 15 vyenye dawa, kwa kila Mtanzania kulala bila bughudha ya mbu, na kuwa vyanzo mbalimbali vya misaada vimekwishahakikisha kuwa vyandarua hivyo vitapatikana baada ya awamu ya kwanza ya vyandarua milioni 5.2 kuwa vimepatikana.
  “Kama mlivyosikia, Waziri Mkuu wa Uingereza, Gordon Brown, pekee yake ameahidi kutoa kiasi cha vyandarua milioni 100 katika miaka michache ijayo. Tanzania itanufaika na sehemu na vyandarua hivyo. Pili, tunao msaada wa sekta binafsi ambayo pia itatoa vyandarua.

  Mpango ni kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2015 ni dhahiri utafanikiwa,” alisisitiza Rais. Rais Kikwete aliyewasili New York, Septemba 21, mwaka huu, ameliwakilisha Bara la Afrika kwa maana ya kushiriki katika mikutano kadhaa muhimu, ikiwa ni sehemu ya mikutano ya mwaka huu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
   
 2. M

  Mbalamwezi JF-Expert Member

  #2
  Sep 30, 2008
  Joined: Sep 30, 2007
  Messages: 802
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 45
  Inawezekana, maana Pemba sasa iko kwenye kiwango cha kuweza kutangazwa na WHO kuwa hakuna malaria. Hayo ni mafanikio ya Presidential Malaria Initiative (PMI), mpango wa GW Bush ulioanza 2002 kama sikosei.
   
 3. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #3
  Sep 30, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,466
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 0
  Hakuna jipya!
  Ule mradi wa wajapani wa kutokomeza malaria in the mid 1980s uliishia wapi?- sana sana ni magari mengi,, mbwembwe za kuvaa migwanda na paraphenelia nyingine..dawa ziliishia kumwagilia michicha.....
  labda kama approach ni tofauti.
   
 4. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #4
  Sep 30, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,742
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu mi napinga hili la kuletewa vyandarua ili kutokomeza malaria,kwa maana hiyo itabidi watoe tena vingine baada ya miaka 2 kwakua hivi vitakua vimetoboka?Hivi bei ya vyandarua ni shilingi ngapi? 5000?, 7000? Hivi hatuwezi kila mwaka kwa hela yetu wenyewe kuwapa idadi flani ya raia wetu vyandarua na pia kuteketeza mazalia ya mbu?
   
 5. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #5
  Sep 30, 2008
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hebu tuache kushabikia porojo hao watu 120,000 Zenj ni almost 1/3 ya wazanzibari wote that translate into total vanishing of Island dwellers in just three to four years. Well na hiyo mpya yenye nafuu na ujiko i.e 60,000 deaths per yr ina maana watu wataisha zenj kwa malaria hata kabla ya 2015 au ndio muungwana anamaanisha utokomezaji. Na hii ya vyandarua milioni 100 du?????? Kama kweli kaka yetu aliyasema haya kazi ipo?????????? Huyu kweli ni mkulu?

  I am proud I didn't give him my vote anyways.....................
   
 6. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #6
  Sep 30, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hizi porojo za tutafikia kitu fulani mwaka fulani kwa kweli kidogo ni chafua roho maana hazina ukweli wala la maana ndani yake zaidi ya kutupotezea muda na kuwapa maskini hohehahe false hopes!
  They have feiled and are failing everyday!
   
 7. Triplets

  Triplets JF-Expert Member

  #7
  Oct 2, 2008
  Joined: Sep 27, 2007
  Messages: 1,094
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 145
  Umetoa point ya maana sana mkuu, halafu mi huwa najiuliza hivi wale wa vijijini (ambao ndio wengi) wanaolala kwenye virago na mikeka hivyo vyandarua huwa wanavitumia vipi?

  pia kwa upande mwingine hivi vyandarua vimaweza hugeuka kuwa hazards kiafya yaani unakwepa malaria na kuibuka na gonjwa jingine kwa mfano kuna wale wanaolala kwenye nyumba za udongo, vumbi kibao na sabuni ya kufulia vyandarua hawana,
   
 8. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #8
  Oct 2, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,466
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 0
  vyandarua bila kuondoa mbu......
  watu wanashinda kwenye vyandarua muda wote?
   
 9. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #9
  Oct 2, 2008
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Ahsante sana Nyambala kwa hili. Wanasiasa mara zote wanapenda kutoa takwimu za kuwafurahisha wananchi waonekane kuwa wanafanya kazi. Miradi mingi inafanyika kama zimamoto ili kujipatia popularity ya haraka itakayo wawezesha kuwadanganya wananchi baada ya miaka 5.

  Takwimu za umoja wa mataifa zinaonyesha duniani, watu 250,000,000 huugua malaria kila mwaka. Na kati ya hawa vifo vinafikia 1,000,000. Kawa numba ya mkuu hapa ya Zanzibar kuwa 60,000 ya vifo zanzibar, ina maana kwa afrika pekee yenye watu takribani 922,000,000 basi vifo ambavyo vingetegemewa baada ya haya mafanikio ya zanzibar ni 55,322,000. Hizi sijui ni takwimu za wapi huyu muungwana anataka kuwa danganya wananchi.

  Halafu jamaa anatudanganya kuwa Zanzibar malaria haijaisha kwa kuwa eti Bara haikushirikishwa. Mbu hawewezi kuvuka bahari kwa kuruka, na idadi ya mbu wanaobebwa na vyombo vya usafiri haiwezi kuwa tishio kubwa kiasi hicho. Tatizo angesema ni kwa nchi za mailand kama Kenya, Uganda Msumbiji n.k

  Pili, misaada mingi haina mafanikio yadumuyo (not sustainable), kwa kuwa tatizo sio leo tuna njaa kwa hiyo tunahitaji chakula. Ila tufanye nini ili tuweze kujitafutia chakula. Ni aibu kuwa kila rais ajae atakuwa kazi yake ni kuzurura tu kuomba misaada, haitakuwepo siku zote. Sisi kama taifa tunatakiwa tujipange, ili tuone vyandarua na dawa za mbu pamoja na hospitali zinapatikana je. Wananchi wanahusishwa vipi kujiwezesha kumiliki vyandarua na kupulizia dawa bila kusubiri msaada wa Bush (huyu Nov ndio mwisho).

  Tatu, Propaganda za siasa ziachwe katika mambo ya msingi. Kuwe na mkakati wa kuwaelimisha wananchi juu ya umaskini unaowakabili na wanatakiwa kushiriki vipi kupambana nao. Na serikali iwe tayari kuwapa watanzania furusa ya kujiletea maendeleo yao badala ya kuwa na mtizamo kuwa wazungu na wahindi ndio watakaoibadilisha nchi hii.

  Kutokomeza Malaria inawezekana tu, pale tutakapotokomeza umaskini.
   
 10. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #10
  Oct 2, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,299
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Never ever, mazingira yetu mabovu, elimu duni,uchumi duni, parasite mutation +etc ni bora tuwazie zaidi eradication, angalia yellow fever imetokomezwa duniani?
   
 11. Songambele

  Songambele JF-Expert Member

  #11
  Oct 3, 2008
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 3,101
  Likes Received: 741
  Trophy Points: 280
  Sidhani kama misaada bila kujenga uwezo na kubadili fikra itamaliza tatizo moja kwa moja manake matatizo mengine nasi tunatakiwa tuchukue hatua. Ni sawa na kugawa condom bure na watu hawazivai na ukimwi unaendelea kutesa. watu wapewe vyandarua na wajengewe uwezo na fikra za kununua kikiisha au kukitunza kiendelee kudumu.

  Ilishawahi kulipotiwa watu wanavulia samaki vyandarua na wanasiasa wanageuza msaada kuwa mtaji wa siasa kuendelea kutoa discipline kwa waTz. Pia Jk atoe feedback mara kwa mara manake unaweza usisikie tena.
   
Loading...