Ghost Worker
JF-Expert Member
- Apr 20, 2016
- 1,412
- 1,864
Kumekuwapo na tuhuma za muda mrefu pale law school kuhusu uchakachuaji wa matokeo japo hazina uthibitisho lakini lisemwalo lipo. Miongoni mwa tuhuma hizi ni uuzwaji wa matokeo ya watu kunakofanywa hasa na wataalamu wa IT wa taasisi hii.
Kuna vitu vinavyoweza kutiliwa mashaka na kuongeza wasiwasi kuwa haya mambo yapo na mojawapo ni utangazwaji wa matokeo ya kila cohort. Hakuna siku ambayo taasisi iliwahi kutaja tarehe sahihi ya utangazwaji wa matokeo. Tarehe inaweza kuahirishwa hata mara tatu. Sasa kama tatizo linafahamika kwanini lijirudie kwa matokeo ya kila cohort? Nini kinakuwa kinafanyika ndani ya muda huo matokeo yanapoahirishwa kutolewa?
Taasisi iliwahi kutoa ufafanuzi wa mchakato mzima wa jinsi mitihani inavyosahihishwa hadi majibu kutolewa. Tunaomba itoe ufafanuzi zaidi ni kipi hufanyika baada ya matokeo kuruhusiwa kutangazwa kuhakikisha kila mmoja anatangaziwa kile alichokipata na anachostahili.