Laughter series: Making phone call in hell....!

Kwetunikwetu

JF-Expert Member
Dec 23, 2007
1,535
408
Kuna watu watatu (mmoja toka marekani, mwingine toka Ulaya mashariki na mmoja toka Africa) walikuwa kuzimu. Sasa siku moja shetani akawaita wale watu watatu na kuwataka wapige simu makwao kuwasabahi ndugu na marafiki.

Yule mmarekani akawa wa kwanza. Aliongea kwa muda wa dakika moja. Alipouliza bili yake shetani akamwambia ni dola 5,000.

Jamaa wa Ulaya mashariki nae akapiga simu kwa nusu dakika kisha akaikata. Shetani alipomuuliza kulikoni, yule jamaa akasema hangeweza kumudu bili kubwa hivyo inatosha. Hata hivyo shetani akambembeleza jamaa apige simu tena. Hivyo jamaa akapiga simu kwa dakika moja ingine. Alipouliza bili akaambiwa ni 500 USD.

Mwisho jamaa toka Africa (Sierra Leone) akapewa nafasi nae aweze kupiga. Yeye akagoma kabisa kupiga akiogopa bili. Hata hivyo shetani akamsihi apige simu asijali sana. Basi jamaa akaongea kwa sekunde kumi kisha akakata simu. Shetani akamsihi jamaa aongee mpaka achoke asiogope. Baada ya ushawishi mwingi jamaa akapiga simu kwa dakika tatu zaidi. Alipouliza bili akaambiwa alipe dola moja.

Sasa yule mmarekani na yule mwenzake toka Ulaya wakalalamika kwanini jamaa wa Sierra Leone kapendelewa analipa pesa kidogo almost bure. Then shetani akawajibu 'for him this was just a local call as opposed to yours which is almost international call'
 
Kwe kwe kwe!!!! Yaani Afrika ni Motoni? This is rediculous, paradox and funny, nimeipenda
 
Back
Top Bottom