Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 18,670
- 22,260
Mfumo wa ukatishaji tikiti kwa njia ya mtandao ni nzuri, pamoja na hilo kikwazo ni lazima uwe na bando ndipo utaweza kukata tikiti, hapa ndipo unapojikuta unatumia pesa nyingine huenda kuliko mfumo wa zamani, mfano mtu anayetoka Dar kwenda Chalinze ambapo angelipa shs. Elfu tano hivi, sasa analazimika Kununua bando kwanza labda shs. Elfu mbili au zaidi ili aweze kupakua aplikesheni ya LATRA na kununua tikiti, kwa hiyo gharama tayari inakaribia nauli!
Tatizo jingine ni ununuaji wa vocha hasa wakati wa usiku au baadhi ya maeneo hata wakati wa mchana. Ukitumia mfumo wa DATA BILA MALIPO matatizo yote haya hayatakuwepo, hivyo LATRA kama mna nia ya kutusaidia wananchi bila kujali kukosa kipato toka kwetu, tumieni mfumo huu.