Tunaweza kufanya biashara gani? na huo mtaji kidogo unaweza kuwa kiasi gani?
Nadhani itakuwa vema kama tukianza kuangalia soko kwanza..., alafu tukarudi nyuma ni nini cha kufanya kuweza kukidhi hilo soko..,
Ulisema kuhusu Bar lakini binafsi ninavyojua ni kwamba hii biashara uangalizi mzuri ili watu waweze kuja na kurudi kila siku lakini kama wadau kama tayari huwa mnaenda kwenye Bar za jamaa wengine kila siku (basi inaonyesha kwamba soko lipo).
Pia kuna issue kama ufugaji tofauti tofauti (hili soko lipo ingawa kuweza ku-compete vizuri inabidi kuwe na constant supply ya kuweza kuongea na mahoteli makubwa..) na kwa hili tunaweza tukapata waangalizi as well as a vet wa kushauri na kuangalia mifugo..
Raw materials ni nyingi sana bongo (ila zinahitaji kuongezewa value..) yaani packaging nzuri hapo unaweza kupeleka hata nchi za nje (mfano niliona kuna soko zuri sana la miguu ya kuku china) ukiangalia hapa bongo watu wengine wanatupa hii miguu
Kwahiyo mkuu the list is endless cha maana ni kuanza na kitu kimoja cha kuongeza mtaji baada ya hapo hatukatazwi kuingia kwenye biashara nyingi as possible so long as kuna profit..., lakini nadhani nzuri ya kuanzia ni zile zenye risk ndogo na haziitaji learning curve kubwa baada ya hapo hata zile ngumu na zenye learning curve hakuna neno (sababu tunaweza hata kuajiri expert kusimamia)
Na kumbuka ugumu wa kufanya kazi fulani inamaanisha kwamba hata competition itakuwa ndogo (ni jinsi tu ya kuweza kuifanya hio kazi kwa urahisi) na advantage tutakayokuwa nayo hapa ni wingi wetu; hivyo basi kuliko kuangalia tu soko la bongo ni bora kuangalia masoko ya nje ya nchi na kuangalia hata vitu kama viungo ambavyo mfano kwenye ulimaji ndio vina profit zaidi.., kama tunaweza kuvipata na kusupply nje.
Mfano kuna siku nilikuwa ninafanya research kuhusu ni nini ni very profitable kuweza kulima na kuuza nikaona list kama hii hapa chini..., hivyo basi kama tunaweza tukapa hivi vitu na kuweza kuvipack vizuri na kuvituma nje ni soko zuri ambalo tutakuwa tumepata
http://ezinearticles.com/?Ten-Most-Profitable-Herbs-to-Grow&id=3438303
Kwahiyo mkuu hakuna kinachoshindikana chochote ambacho tunaweza kuweka nguvu zetu na kukifanya mwisho wa siku kina faida its just doing it well enough (ila ni bora tuangalie soko mpaka la nje..)
Kuanza tunaweza kuanzia popote ila tuangalie soko kwanza ili tuweze kufanya Opportunity Cost