LAPF, PSPF, PPF, GEPF, NSSF ipi ni bora katika kuwa mwanachama

LAPF, PSPF, PPF, GEPF, NSSF ipi ni bora katika kuwa mwanachama

Habari za jioni wana if, Naombeni msaada nataka kujua upi ni mfuko bora kati ya NSSF,PPF,PSPF na LAPF kwa anayejua ,Natanguliza shukrani zangu za dhati!

Pspf ndo mpango mzima
 
LAPF ni nzuri sanaa kwa wafanyakazi wapya wanaonza kazi kwani mkokotowo na mchanganuo wanaotumia ni nzuri sanaa hivyo ushauri Wangu kwako chagua LAPF kind regards
 
Jiunge na LAPF. Hakuna Mfuko wa Jamii bora kama LAPF. Utakuja kukubaliana na mimi.
 
PSPF ni best ikifuatiwa na LAPF, NSSF ni majanga utajuta, kama unabisha jiunge utanipa majibu


Kiukweli,nataka nikwambie tuache unafiki NSSF weka pembei wala usijaribu kujiunga kabisa ni shida tena shida wakati unataka kuchukua mafao yako na yanakuwa kidogo sana ila nakuomba ingia LAPF hutajuta na wana formula nzuri ya ukokotoaji mafao inapishana kidogo na PSPF.Muhimu LAPF mkuu na usumbufu no wala huwafuatillii wakati wa kuchukua mpunga wako,Hela yako
 
Nami nimejifunza mengi na ninashukuru sana kwa kupitia kuanza mwanzo mpaka mwisho.
Jibu nimepata
Nami ninaangaikia ajira na mfuko mimeona ni bora ni LAPF na ukifiatiwa na PSPF asanteni sana
 
Nianze kwa kuweka wazi kuwa mimi si mwajiriwa wa mfuko wowote, wala si mwajiriwa wa mamlaka ya uthibiti wa mifuko ya pension(ssra). Maoni yangu ni ya mwananchi wa kawaida na mwenye uelewa wa kiasi katika tasinia ya hifadhi ya jamii. Mfuko bora wa hifadhi ya jamii ni ule
1. unaotoa mafao yote 9 kwa mujibu wa ILO au unaokaribia idadi hiyo.
2. Uwe ni endelevu yaani unaweza kuendelea kutoa mafao kwa wastaafu wake kwa muda mrefu hata bila ya kukusanya michango.
3. Utoe mafao yanayoendana na uchangiaji wa mwanachama i.e unacholipwa mwanachama unapostaafu kikaribiana na ulichochangia, ukilipwa too high jua mfuko huo ni kama ponzi scheme tuu.

Hmna cha mafao 9.mifuko kama nssf na pspf inakufa ndani yamiaka si zaidi ya mitano
 
NSSF wanakata 10% na mwajiri 10% wakati LAPF wanakukata 5% na mwajiri 15% hiyo pekeyake tu ilinifanya nikimbie NSSF na kujiunga na LAPF kwa kuwa kila mwezi na save 5%
Hukupata ushauri vizur wa kihasibu hakuna seving yeyote hapo mkuu! kwa ufupi ni hv hizo asilimia za mifuko hukatwa kabla ya kodi kwhy unapokatwa asilimia ndogo kiwango cha kodi kinakuwa kikubwa na unapokatw asilimia kubwa kiwango cha kodi hupungua kwhy hiyo amount unafikiria kuwa unaisave inaishia tra tu
 
Mifuko bora ni miwili tu PSPF na LAPF(wanatumia the same formula katika ukokotoaji mafao)ila kati ya hii miwili PSPF ndio mfuko mzuri sababu;
1/Wana experience ya muda mrefu ktk ku operate as a pension fund(1999) compared to LAPF ambao wame transform from PROVIDENT to PENSION FUND mwaka 2008.

2/PSPF wana ofisi kila mkoa wakati LAPF wana ofisi kati ya 6 tu Tanzania nzima

3/Mikopo ya nyumba PSPF ni baada ya miaka 5 tu wakati LAPF ni baada ya miaka 15

4/PSPF wanatoa mafao ya aina 12 wakati LAPF wanatoa mafao ya aina 6 tu

5/PSPF wana wanachama karibu 400,000 kwa mujibu wa takwimu za mwaka jana wakati LAPF ndo wanaitafuta 100,000
Hayo ndo majibu ya kumsaidia mtu sio bla bla big up mkuu
 
sasa we jamaa unakuwa kama ujasoma ratio pr school ukiangalia ratio ya muda wa kuanza operation na no of customers bado lapf ni iko juu maana imechelewa kuanza lakini speed yake ni kubwa ktk ukuaji hivyo tumia statistic vizuri kuargue.
Hata china uchumi wake unakua kwa kasi kuliko USA lakini hailingani kiuchumi na USA
 
Unaposema PSPF na LAPF ndiyo the best una maana gani? Je wajua kuwa PSPF na LAPF wanapewa ruzuku Tsh 1bil na serikali kila mwaka ili iweze kulipa wastaafu wake? Je unajua siri ya PSPF kuwa na ukokotozi unaompa mstaafu mafao makubwa? Nikupe tuu kwa kifupi:
PSPF ulikuwa mfuko wa akiba kwa wafanyakazi wa serikali kuu (makatibu wakuu, wakuu wa idara). Wakati wa kuibadilisha PSPF kuwa mfuko wa pension(from a provident fund to a pension fund) makatibu wakuu wakijua huu ni mfuko wao, walijiwekea formula iliyowapendelea wao watakapo staafu.
Kwa upande wao NSSF na PPF, hawapati ruzuku kutoka serikalini, na ukifuatilia ni mifuko sustainable. PSPF na LAPF ina hatari ya kucollapse muda wowote.

Acha masihara bana ujue nina tumillion twangu lapf....usinipe pressure buree jaman
 
Unaposema PSPF na LAPF ndiyo the best una maana gani? Je wajua kuwa PSPF na LAPF wanapewa ruzuku Tsh 1bil na serikali kila mwaka ili iweze kulipa wastaafu wake? Je unajua siri ya PSPF kuwa na ukokotozi unaompa mstaafu mafao makubwa? Nikupe tuu kwa kifupi:
PSPF ulikuwa mfuko wa akiba kwa wafanyakazi wa serikali kuu (makatibu wakuu, wakuu wa idara). Wakati wa kuibadilisha PSPF kuwa mfuko wa pension(from a provident fund to a pension fund) makatibu wakuu wakijua huu ni mfuko wao, walijiwekea formula iliyowapendelea wao watakapo staafu.
Kwa upande wao NSSF na PPF, hawapati ruzuku kutoka serikalini, na ukifuatilia ni mifuko sustainable. PSPF na LAPF ina hatari ya kucollapse muda wowote.
Hakuna cha kukolapse hapo mkuu hy mifuko unayoisifu yenyewe ina maden kibao ya wastaafu na mahela yao mengi yamekopwa na serikali na ripoti ya mwisho ya CAG ilionyesha hy mifuko iko taaban
 
Nami nimejifunza mengi na ninashukuru sana kwa kupitia kuanza mwanzo mpaka mwisho.
Jibu nimepata
Nami ninaangaikia ajira na mfuko mimeona ni bora ni LAPF na ukifiatiwa na PSPF asanteni sana
Huo ndo ukweli mkuu
 
Haya hadi kufika sasa hali ipoje huko mifukoni?
 
Back
Top Bottom