Landcruiser V8 au Hammer!!.

Chukua Landcruiser VX V8 kwa kazi zako mkuu. Hammer umnunulie Mama watoto ya kupelekea watoto shule na kuendea saluni!
 
Ipi safi hapo, anayezielewa vizuri. Nataka kununua.

Nikitumia uzoefu (naitumia katika field vijijini), nakushauri ununue Landcruiser V8. Imetengenezwa robust kwa ajili ya mazingira ya Kiafrika zaidi, hasa hizi barabara zetu mbovu. Inatumia mafuta kidogo sana, inakwenda km 11 hadi 12 kwa lita kwa spidi isiyozidi 140 KPH, lakini pia ni stable sana njiani hata ukiwa katika spidi kubwa. Ila, the car is fully electronic, uwe makini sana na mafuta ya kununua njiani, iko sensitive sana kwa mafuta yenye mushkeli.
 
Back
Top Bottom