Amini msiamini, naona mchuano mkali kati ya Lameck Airo na Bwna mdogo John MAshaka 2015. Lameck aligusa nyoyo za watu na hata kumshinda mpinzani wake mkubwa Prof. Monyo. Lameck alitoa kituko cha mwaka, kwa kusema kwamba, Darasa la saba mpo??? basi umati mkubwa ukaitika tupo... Basi hiyo ndio ikawa signature yake kwenye kampeni.......Darasa la saba ukawa ndio wimbo wake. .... Ila kwenye uchaguzi wa 2015, kuna tetesi za uhakika kwamba atapambana na mwanaharakati John Mashaka ambaye anaheshimika na kukubalika siyo kawaida kwenye jimbo la Rorya. Vile vile kuna tetesi kwamba mashaka ambaye amekulia Ukonga, anaweza kugombea Segerea. Tunasubiri tuone ni wapi, ila Lameck atakuwa na wakati mgumu sana 2015