Lakini la pili...

Huu m'banango wa lugha uko mwingi mkuu, iko nyingine unamuuliza mtu "ee bwana umeshakula ? " anakujibu
"hamna"
(hapo ndy ana maana hajala) au "hizi Ng'ombe" badala ya hawa Ng'ombe.
"Hii Mbuzi siichinji" instead of huyu Mbuzi simchinji etc

Muda si mrefu chit chat watasema tumewavamia. Kuna taarifa kuwa wanafunzii wanafeli sana kiswahili siku hizi. Kiinglish hatupo, kiswahili hatupo... Halafu pia kuna wanaosema, (mfano) 'nyimbo ambayo iliyoimbwa'. Kwanza 'nyimbo' kosa, 'ambayo iliyoimbwa kosa.

Sahihi: wimbo ulioimbwa
Wimbo ambao umeimbwa
 
Chitcht ni changanya marumba !
Ushamsikia mtu anasema "hii pilipili uliyonipa siyo chungu, nitafutie chungu" (kwa maana hiyo siyo kali haimuwashi)
 
Mimi kama mimi napenda sana ile nyimbo ya Barnaba-Magubegube. Ni nyimbo ambayo iliyoimbwa kwa ukweli sana. Lakini pili, video yake nayo imekaa vizuri...
 
Wala si pinda pekee bali karibu watu wote ambao kwa namna moja ama nyingine wana nyadhifa nchini hapa
 
Back
Top Bottom