Lakini la pili...

Raia Fulani

JF-Expert Member
Mar 12, 2009
10,876
2,739
(mfano)'...katika hilo tukaona kuwa tuboreshe sera ya kilimo ili iendane na wakati uliopo, sambamba na soko huria. Lakini la pili...' Kiukweli hapo wanasiasa, wasomi, na wataalam wetu huwa wananiacha hoi sana. Hii imekuwa wimbo wao. Wabadilishe sasa. Lakini la pili, sidhani kama ni matumizi sahihi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
 
mbona rahisi? Kwani hamjawahi kuwasikia viongozi wetu wakitumia haya maneno?
 
(mfano)'...katika hilo tukaona kuwa tuboreshe sera ya kilimo ili iendane na wakati uliopo, sambamba na soko huria. Lakini la pili...' Kiukweli hapo wanasiasa, wasomi, na wataalam wetu huwa wananiacha hoi sana. Hii imekuwa wimbo wao. Wabadilishe sasa. Lakini la pili, sidhani kama ni matumizi sahihi ya lugha yetu adhimu ya Kiswahili.

Bora leo nimepata mwenzangu wa kuliona hilo neno kama halijakaa vizuri, awali nikijidhani ni mie tu.
Ni misemo ambayo haikuwepo zamani, imezuka hii miaka ya karibuni.
Mf. Mwingine wa maneno haya ni "Mimi kama mimi....... " nalo kimaono yangu pia halijakaa njema pia.
Nilipoona tu headin' yako kabla sijaifungua Thrade nikaelewa ulichokilenga.
 
Hili limekuwa ni tatizo pana sana hasa kwa viongozi. Sijajua sababu hasa ni nini. Na hilo la mimi kaka mimi ni ishu pia. Ila nashangaa wadau humu hawakunielewa nazungumzia nini.
 
Sijalewa post ina maanisha nini?

Hivi kutumia lakini la pili ni tatizo, tuweke wazi. Mie ni mdau wa hili neno, lol.

Naona pana tatizo. Wengi wa watumiaji huwa hawaanzi na 'mosi'. Utasikia tu 'lakini pili'. Hatusikii tatu wala nne. Atasema tena kisha utasikia, 'lakini pili'. Halafu kwa nini waweke 'lakini?' ukishaweka 'lakini' ni wazi kuwa ulichoongea mwanzo kinapingana na cha pili. Upo?
 
Thanks, learned!
 
Huu m'banango wa lugha uko mwingi mkuu, iko nyingine unamuuliza mtu "ee bwana umeshakula ? " anakujibu
"hamna"
(hapo ndy ana maana hajala) au "hizi Ng'ombe" badala ya hawa Ng'ombe.
"Hii Mbuzi siichinji" instead of huyu Mbuzi simchinji etc
 
Back
Top Bottom