Laki Moja yako itakupa milioni 3 kwa miezi 3 tu

Kukopa ndio tatizo pia, mimi napenda kuwashauri watu mkopo ni kuajiri ya kuendeleza au kukuza biashara ila sio wa kuanzishia biashara, sababu hujakumbana na changamoto yoyote ya biashara wala hujui mwelekeo ukoje wa soko sasa ukikopa litakuwa ni tatizo
Naam ushauri mzuri
 
Habari za wakati huu ndugu zangu humu !!

Siku nyingine tena tumshukuru Mungu tumeamka wazima, tukiendelea na harakati za utafutaji ridhiki za halali. Leo nina habari njema kwa wale wenzangu ambao hawana kazi ila wana pa kuanzia. Nazungumza na yule mtu ambaye anasema hana mtaji wakati mkononi ana iPhone 11, 12 au 14 na mwingine ana Samsung ya 400k.

Mtaji unao, uza hiyo simu yako ya milioni moja au ya laki 5 au 6 kisha nunua kitochi au nunua smartphone ya bei rahisi tu 150k ili usipitwe na mtandao halafu inayobaki nifuatilie hapa nakupa mchongo unaohitaji mtaji wa Tsh 100k tu na hiyo nyingine iweke akiba kwa ajili ya emergency.

Biashara ya laki moja fanya hivi. Chukua 50k tafuta brenda ya kusagia juice ya matunda, 10k tafuta dumu la lita 5 na 20k tafuta cup ndogo za kuwekea juice za take away za buku na jero jero na hiyo 20k inayobaki tafuta matunda mbalimbali saga juice dumu moja weka juice ya aina moja ambayo inapendwa sana na dumu lingine weka juice ya mchanganyiko kisha mtafute dogo yoyote unayemuamini kama huwezi kutembeza mwenyewe, mkubalianae utampa Tsh ngapi kwa siku.

View attachment 2945744

Au kama huwezi kabisa basi saga juice mpelekee mamalishe mmoja akuuzie wakati wa chakula. Hakikisha unapata mamalishe mwaminifu na ambaye hana tamaa, maana wengine wakiona unauza na yeye anatengeneza yakwake anauza.

Mfano ukiamua kutengeneza juice nzito ya kuuza Tsh 1000 kwa glass moja maana yake kwenye lita tano utapata Tsh 20000 na ukitengeneza juice nyepesi ya kuuza Tsh 500 kwa glass ina maana kwa ile lita 5 itakuwa lita 10 ambayo ukiuza zote lita 10 kwa Tsh 500 kwa glass moja utapata jumla Tsh 10000.

Matunda ya Tsh 5000 sokoni yanatosha kutengeneza juice ya lita 5 kwahiyo ukipata matunda ya Tsh 20000 utapata lita 20, sasa utapiga mchanganuo wako hapo namna utakavyofanya. Keep in mind kwamba mahesabu haya siyo halisia kwa asilimia 100 kulingana na utofauti wa mazingira, kupanda na kushuka kwa bidhaa sokoni na hali ya uchumi wa walaji.

All the best wewe ambaye utaamua kuchukua ushauri huu.

Kwa ushauri mbalimbali wa ujasiriamali hata kama huna mtaji. Napatikana WhatsApp +255 683 535 699
HIZI IDEA ZA KWENYE MAKARATASI HUWAGA ZINALIPA SANA

Jichaanganye
 
Vipi nikitengeneza nisiuze hata moja au nikauza nusu nyingine ikachacha ? Au hakuna Kuchacha ?

Na kwanini milioni tatu tu kwanini nisi-dublicate / replicate hii idea na kutengeneza Trillion kadhaa ? Huyo mama Lishe ninayempelekea ili aniuzie na bado tukapata faida kwenye margin ya sijui ngapi (tunauza 500) kwanini asitengeneze mwenyewe na kuuza kama anao wateja wa kutosha ?

In short Bongo Biashara pasua kichwa (Soko bado ni tatizo Kubwa..., watoa Hudumu ni wengi kuliko Wahitaji)
 
Nilipo hakuna umeme, je Nita saga hAyo matunda kwa meno🤓😂
Utatwanga
255755959096_status_f3500fc1ecd4407a9037267f7b564584.jpg
 
Back
Top Bottom