Laiti wananchi wangeisoma ripoti ya CAG mapema

Laiti wananchi wangeisoma ripoti ya CAG mapema

1. Ungelifanya rejea kwa vifungu vya Ripoti ya CAG ungeeleweka kuwa ni mtaalamu lkn umeteremsha mambo kienyeji. Inasababisha kutilia Mashaka taaluma au hauitendei haki taaluma. Ripoti ya PAC haina mashiko kama haiendani na Ripoti ya CAG!

2. Kumbuka hukumu ya Jaji Q

Ungenisoma vyema kwenye hoja yangu ya mwanzo,ungepata mantiki ya kwanini nimesema niliyosema.

Narudia CAG amesema kunapesa ya umma na pesa ya IPTL.Pesa ya umma ipo kwenye mafungu mawili:
1.Pesa ya TANESCO ambayo walikuwa na mgogoro mkubwa na IPTL kuhusu TOZO,na wakaenda mahakamani kupata suluhu,mahakamani wameshinda ,wanalitakiwa kukokoto TOZO kulingana na na HUKUMU,na serikali haikusubiria TANESCO walifanye hili,hivyo pesa za UMMA hapa zimeibiwa upo?

2.Pesa ya TRA ambayo ilibidi ilipwe kabla ya IPTL hawajalipwa na bank kuu,hivyo hii pia ni pesa ya UMMA.upo?Sasa wewe unaniambia siitendei haki TAALUMA yangu kivipi?

3.Hakimu UTAMWA hakusema pesa ya mgogoro ilipwe,huku kulikuwa kutumia vibaya vyeo,madaraka na elimu zao walizopata kwa pesa ya mlipa kodi.Hawa wote waliohusika ni wale waliosomeshwa na serikali.
Nipo pale pale humo kuna pesa ya UMMA,tunahitaji irejeshwe.
 
mengi yamejadiliwa, ambalo halijajadiliwa ni

1. dhamira ya mgawa pesa ninini? hata kama pesa ni zake

2. anataka kupata nini katika uwekezaji alioufanya kwa watu mashuhuri/wanasiasa.

hili ni swala linalopaswa kufanyiwa kazi na vyombo vya usalama, vinginevyo kila siku kutakua na mambo mapya katika maktaba za ulinzi na usalama.
 
Tunasema pesa ni ya wizi sababu UMMA watanzania ndiyo tuliyoibiwa,kumbuka kuna pesa halali ya TANESCO na TRA na ni sababu hizi ulizozitaja za kutumia madaraka vibaya ili kupora mali za umma

Pili yake hukumu ya kuchakachua TOZO ilishakuja na TANESCO walishinda na MAHAKAMA iliwaambia TANESCO wakokotoe pesa yao ili kujua nani alipwe nini.

Sasa leo ukiniambia hakuna pesa ya UMMA nitakushangaa,na ndiyo maana nawashangaa wale tuliowapa dhamana wamekuwa MAPANYA wakitoboa magunia na hakuna kinachofanyika.PANYA ni PANYA,hakuna PAKA wakumfunga kengele PANYA maana hakuna PAKA tena huko serikalini,tuliowadhania ni PAKA ghafla wamegeuka MAPANYA na dniyo maana PANYA mkubwa anamshangaa CAG kwa nini bado yu PAKA!

Serikali imeridhia WIZI huu sababu ndiyo wanufaikaji hasa wa hizi pesa za WIZI.

Hata NCHEMBA mwenyewe anachofanya ni kujitahidi au kujaribu kuzisafisha pesa hizi ziwe SAFI,kaka haziwezi kuwa safi hata zisafishwe na JIKI bado ni CHAFU tu.

Wote wanalindana hata NCHEMBA anajitahidi kuwalinda wenzake na ndiyo maana anapiga domo zilipiwe kodi.KAka pesa za umma zimepigwa,tusiwafumie macho hawa MAJAMBAZI,tuwaambie ukweli tena kwa sauti kubwa,warudishe fedha za UMMA na sheria ichukue mkondo wake!!!!!

Swali la msingi tuelewe kulikuwa na mkataba wa mauziano ya umeme kati na mwuza umeme na mnunuzi umeme. Pande zote zilikuwa na wanasheria wao kulinda masilahi ya kila upande. Mlipaji aliridhika na huduma aliyonunua vinginevyo asingelipa kama kwa ufahamu wake na wanashiria wake kuhakiki mkataba umekiukwa. Vinginevyo kama mkataba umekukwa na mteja unaendelea kulipa ni makosa yako. Ndicho kinachotokea sasa.

Hivyo pesa si za wizi hata ukuleta hapa mahakama yakimataifa pesa zimelipwa kadiri ya makubaliano kimkataba. Tuache kuhemka tusimame kwenye misingi ya haki kisheria.
 
Hakuna haja ya kurudia porojo zako ambazo umezijenga based on Hotuba ya JK.
Looks like hata hiyo report ya CAG hujawahi kuitia hata machoni,achilia kuisoma,umekalia ushabiki wa vitu usivyovijua.
Pia unaonekana hata hukumu ya Jaji Utamwa ambao ndio Msingi wa Mgogoro huu huijui na wala hauko aware kuwa kuna kiti kama hicho.

Narudia kusema only Punguani can argue the way you do.

Tafadhali rejea kwenye ushauri wangu kwako hapo juu. Kutumia maneno ya kuudhi haikusaidii. Jenga hoja. Kama huna hoja soma hoja za wenzako uelimike. Uungwana ni vitendo.
 
Tafadhali rejea kwenye ushauri wangu kwako hapo juu. Kutumia maneno ya kuudhi haikusaidii. Jenga hoja. Kama huna hoja soma hoja za wenzako uelimike. Uungwana ni vitendo.

Haya nakuuliza.
Umeisoma hukumu ya Jaji Utamwa ?
 
Ukimsoma vyema CAG utaielewa vyema ripoti nzima,hasa kwa wale wenye TAALUMA yao kwa maana ya WAKAGUZI na WAHASIBU.

Pesa ni ya wizi sababu zangu kuu zaweza kuwa tatu au nne.:

1.Pesa ile ilikuwa bado iko kwenye mgogoro wa pande mbili na ulikuwa unasubiri suluhisho toka MAHAKAMA ya kimataifa kuhusu uchakachuaji wa bei ya umeme iliyokuwa inalipwa na TANESCO kwa IPTL,kwa kuwa walalamikaji waliona wanalipa toza kubwa kuliko ilivyotakiwa,hivyo walifungua kesi na bahati nzuri walishinda,lakini hakuna mchanganuo uliokwihsa fanyika wakuweza kujua pesa za IPTL ni ngapi na za TANESCO ni ngapi,hivyo kwa mantiki hii pesa za UMMA hapa zimepigwa na wajanja.

2.Hakimu hakutoa maamuzi pesa hizi zilipwe kwa PAP kwa maana bado kesi ilikuwa ipo mahakamani kuhusu TOZO na mchanganuo wa pesa hizi haujafanywa hivyo kusema MAHAKAMA imeamua hata zile pesa zilizokuwepo kwenye account yenye pesa za wahusika wengi ni za PAP siyo sahihi,basi hapa wale wachache wanaojua kutumia ELIMU yao waliyoipata kwa KODI ya mtanzania vibaya wakaamua kuchota kisichohalali kutumia ELIMU yao hii kwa maana ya AG wetu,hakuwa na sababu ya kutoa idhini pesa zilipwe wakati anajua wazi si sahihi,lakini kwa sababu zake mwenyewe na wahusika aliamua kupindisha HUKUMU kwa maslahi yao wachache.

3.Kuna kodi hapo haikulipwa na ilitakiwa kulipwa kabla malipo hayajafanyika,hivyo basi hata hili nalo halikuonekana kuwa ni baya kwa viongozi wetu wakatumia vibaya mwanya wa elimu na nafasi waliyonayo kufanya maamuzi mabaya na kuhujumu mali ya umma.

4.Pesa ni ya IPTL si ya PAP kwa nini walipwe PAP na si IPTL?Na hapa hata leo JR akienda mahakamani kuishtaki serikali kuhusiana na pesa yake iliyokuwemo kwenye hii account anashinda tena kwa kishindo,sababu ana haki juu ya FAIDA iliyotokana na mauzo ya umeme baada ya kukokotoa TOZO halali,na kila muhusika kuchukua cha kwake kulingana na mahesabu.

5.Hivi serikali ilishindwa nini kufuatilia uhalali wa huyu singasinga kununua hisa za MERCHMAR?Na siyo kweli kwamba walikuwa hawamjui huyu kuwa ni TAPELI la kutupwa,amefilisika wanajua vyema sana kila kitu,lakini waliamua kufanya sababu walikuwa wanajinufaisha wao na familia zao!

Leo tuna mtu aliyepewa ZABUNI ya kuendeleza reli ya kati,na wanajua mtu huyu amefilisika na sheria za kufilisiwa wenzetu wanasheria wanazijua na hasa Mwakyembe iweje leo tumkumbatie mtu aliyefilisika,tunatafuta nini kwake zaidi ya kuliumiza TAIFA kiuchumi?

6.Jiulize ni kwa nini MASWI mpaka dakika za mwisho alikataa kuidhinisha pesa hizi kutoka,ila ni baada tu ya WAKUU wa nchi kuidhinisha pesa zitoke ndipo alipokubali kutoa,hebu tufikirie alilipwa ngapi?Je alitishwa ili akubali?Alifanywa nini huyu mtu,mpaka alidiriki kusema wakimwaga MBOGA atamwaga UGALI

Haya ndiyo mambo makuu ambayo ukiyaangalia vyema si MUHONGO,WEREMA,MASWI wala RAIS angediriki kuuchekea wizi huu.Ila sababu wote hawa wamekosa uhalali wa kuwa viongozi,wamelewa madaraka,si wazalendo hata kidogo,ni sawa na mwizi aliyeshindwa kumuibia jirani akaamua kujiibia mwenyewe.

Tujitahidi kuwa WAZALENDO tuwe tayari kulinda maslahi ya TAIFA letu,tuwe wamoja,tuwe TAIFA kwanza VYAMA baadaye.Tuchague viongozi wenye WELEDI,WAOGA wa MUNGU,WANYENYEKEVU,WAZALENDO,WATAKAO KUWA TAYARI KULIFIA TAIFA LAO.

Haya ndiyo maoni yangu,kwa TAALUMA yangu hizi pesa zipo za TANESCO,za TRA na za IPTL,hivyo kilichofanywa na viongozi wetu ni kuliibia TAIFA lao mchana kweupe,wakishirikiana na wanaowaita wawekezaji,ambao ni MATAPELI.

Na leo Sethi kanunua visima vya mafuta,hakuja na pesa zaidi ya ile $300,000,tumempa mamilioni ya dollar,hivi kweli VIONGOZI wetu wanafikiri kutumia nini?Hivi kwenye vichwa vyao kuna maji au ubongo?Hivi ni kweli walipoenda shule wameelimika au wameenda kuja kusoma na kuandika tu?

Candid Scope haya ni mawazo yangu kulingana na TAALUMA yangu,sijahongwa wala sitegemei kuhongwa sababu UTU wangu hauna bei.

Huu uzi una Vifisadi na vikuwadi vingi sana na vinahoja ya mihemuko utafikiri vina hoja kumbe hamnazo!! Imeonekana pesa ya Mkombozi Bank pekee ile ya Stanbic haiko utafikiri haikuwaki kuwako!! Vifisadi vya Tanzania vinanuka ubongo!!
 
"Shida kubwa tuliyonayo hapa Tanzania ni kwamba mwizi ndo mtoa uamuzi wa wezi wenzake" hatutafika kwahili. Na mtu mzima na kiongozi mkubwa kumwambia kiongozi mwenzake mwizi ni shida hapa kwetu maana mfumo mzima ni wa wezi. Jamani watu wanazidi kutimuliwa na Rais anatoa pongezi kwa mawaziri waliochukua uamuzi huo lakini bado mtu huamini kuwa zilikuwa ni pesa za umma.
 
Swali la msingi tuelewe kulikuwa na mkataba wa mauziano ya umeme kati na mwuza umeme na mnunuzi umeme. Pande zote zilikuwa na wanasheria wao kulinda masilahi ya kila upande. Mlipaji aliridhika na huduma aliyonunua vinginevyo asingelipa kama kwa ufahamu wake na wanashiria wake kuhakiki mkataba umekiukwa. Vinginevyo kama mkataba umekukwa na mteja unaendelea kulipa ni makosa yako. Ndicho kinachotokea sasa.

Hivyo pesa si za wizi hata ukuleta hapa mahakama yakimataifa pesa zimelipwa kadiri ya makubaliano kimkataba. Tuache kuhemka tusimame kwenye misingi ya haki kisheria.

Kuhemuka hapo hakupo.Kulalamika kuhusu malipo wafanya biashara wote wanahaki ya kwenda mahakamani pale unapoona unalipa sivyo ndiyo.

Cha kujiuliza ni kwanini Maswi waridhie kulipa pesa zilizokuwa na mgogoro na wakati huo huo HUKUMU imetoka na TANESCO wameshinda?Kulikuwa na ulazima gani wakulipa hiyo pesa kwa uharaka huo?

Candid Scope hapa hakuna kuhemuka ni sheria tu,na uadilifu basi,hakuna cha zaidi.Viongozi wetu wote ni wezi na mara nyingi wanatengeneza wizi lakini hakuna wa kwafuatilia sababu ndiyo waliopo madarakani!

Hata kesho bado nitakwambia kaka yangu pesa hiyo ni ya wizi,na wizi walioufanya wameliibia TAIFA lao wenyewe,mbaya zaidi wamemlipa mpka foreigner ambaye ndiye waliyemuita ili deal lao lionekane liko sahihi.

Hivi leo huyo JK akija aambiwa na hao aliowatuma kwamba huyo Singasinga hakununua hizo hisa,atafanyaje?Atatuomba radhi au atapotezea?

Kaka nina uhakika kama tungekuwa na TISS wazalendo leo hii Singasinga asingekuwepo uraiani,lakini TISS yetu ndiyo hiyo ya kuwasaidia na kuwalinda MAPANYA BUKU
 
Huu uzi una Vifisadi na vikuwadi vingi sana na vinahoja ya mihemuko utafikiri vina hoja kumbe hamnazo!! Imeonekana pesa ya Mkombozi Bank pekee ile ya Stanbic haiko utafikiri haikuwaki kuwako!! Vifisadi vya Tanzania vinanuka ubongo!!

Kuna wengine siamini wanachokiandika ukiangalia na post zao za nyuma,sielewi kama ni wao kweli au accounts zao zimeingiliwa na virus.
 
1. Ungelifanya rejea kwa vifungu vya Ripoti ya CAG ungeeleweka kuwa ni mtaalamu lkn umeteremsha mambo kienyeji. Inasababisha kutilia Mashaka taaluma au hauitendei haki taaluma. Ripoti ya PAC haina mashiko kama haiendani na Ripoti ya CAG!

2. Kumbuka hukumu ya Jaji Utamwa, ilitolewa kubariki makubaliano ya VIP kuuza hisa zake 30% kwa PAP ambaye alikuwa tayari amenunua hisa 70% za IPTL hivyo kuwa mmiliki wa IPTL kwa 100%. Baada ya kukubali ombi la VIP la kuiondoa IPTL kwenye ufilisi.

3. Baada ya hayo hapo juu kutokea wewe ukiwa ni Mhasibu kama ulivyojinasibu, unaelewa nini kwa AMRI iliyotolewa na Jaji kwamba Liquidator akabidhi all affairs za IPTL kwa PAP? Je, kama ukweli ulivyo, zile pesa kwenye Escrow Account zilikuwa ni za IPTL, inakuingia akilini kwamba Escrow Account haikuwa moja ya affairs za IPTL, iwe kuna dispute au hakuna? Kumbuka, CAG Report ya 2012 ilikwisha shauri TANESCO wasiendelee kuzihesabu hizo fedha kama asset kwao!

Kwenye 'ALL AFAIRS'hakimu hakuwa na maana hata zile account zilizokuwa na malumbano.Na hakusema sababu alijua fika kwamba kuna kesi ipo mahakama ya kimataifa,ndiyo maana aliyetoa ufafanuzi wa hukumu ndiye naye amekatiwa noti,hivi kwa nini umkatie noti AG?

Wizi huu ulipangwa,kwenye hiyo report ya 2012 kunet off asset haina maana ya kusema pesa siyo za TANESCO,pili yake hiyo unayosema CAG alitoa elekezo itolewe au iwe netted off iliwekwa kwenye Notes za financial statements za TANESCO.

Ndugu kama huelewi kitu uliza utaambiwa maana usiumize kichwa na kutoa hoja zenye viroja ndani yake utachekwa.
 
Kama unakubali kwamba kulikua na kodi ambayo ndo pesa ya umma yenyewe na wakagawana ,bado huoni wizi uliofanyika?
 
Back
Top Bottom