Laiti wananchi wangeisoma ripoti ya CAG mapema

Laiti wananchi wangeisoma ripoti ya CAG mapema

Huu mjadala mwingine umeanza, hakuna hata mmoja hapa atakayefafanua wizi huo ila ni mhemuko wa kufutata mkombo kwamba pesa ni zawili. Fafanueni wizi ulitokeaje tuwaunge mkono, lakini kuhemuka kwa kufuata mkumbo siko tayari.

Mko wengi sana
 
Kudhihirisha kwamba Zito ni mchochezi, kwenye Ripoti yake ya PAC iliyopo kwenye tovuti ya Bunge la Tanzania, ukurasa wa 21 inakiri kwamba fedha waliyolipwa PAP ni Sh. 203.1billioni na kwamba fedha iliyotakiwa kuwa kwenye Escrow Account ni Sh. 306,675,081,939/=

Kumbe inaelekea hiki ndicho Zito na wapinzani hata waliomo ndani ya CCM walichokuwa wakiogopa kisijulikane pale Rais alipoagiza Ripoti ya CAG iwekwe wazi wananchi tuisome. Pamoja na Rais kutolea ufafanuzi suala hilo bado Zito anaendelea na upotoshaji! Maadili tu ya kawaida ya ki-Afrika hayaruhusu hili kutokea. Hii inatia mashaka hata malezi na makuzi ya Zito.

Lakini kwa makusudi kabisa na kwa kuongozwa na nia ya uchochezi ukurasa wa 47 Maoni na Mapendekezo ya Kamati, Ripoti ya PAC umetumia maneno makali ya uchochezi tofauti na ukweli waliouandika wenyewe ukurasa wa 21, ninanukuu "Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi au uliganzishwa ili kuwezesha zaidi ya shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini"

Kwa mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tu, atagundua kwamba kubadilisha matumizi ya neno "iliyolipwa" ukurasa wa 21 kuwa "kuporwa" ukurasa wa 47 na kuamua kutumia kiasi cha fedha ambazo hazikuwemo kwenye Escrow Account, ni mbinu ya kufanya propaganda ya uchochezi.

Zito, alitumia wadhifa wake kama M/Kiti wa PAC vibaya na labda kwa kuhongwa au kuingia kwenye dili chafu ya Standard Chartered Bank iliyotaka kinyemela kuiba fedha za IPTL kwenye Escrow Account kwa kutumiwa na Mkono, Mengi na wanasiasa wanaotafuta u-Rais 2015.

PAC kutolea maamuzi ya uhalali wa SCB wakati kesi ziko mahakamani na kumuandama Mh. Masele, Naibu Waziri wa Nishati na Nadini kwa kumkemea Balozi wa Uingereza kutojiingiza kwenye mambo ya Wizara yake, ni ushahidi tosha kwamba Zito, alikuwa anaongozwa na dhamira ovu na maslahi binafsi, hakutumia hata chembe ya busara. PAC lini imekuwa juu ya Mahakama? Na je, Mh. Masele ni kosa lipi alilokuwa amelifanya kwa kumkumbusha Balozi wa Uingereza kuheshimu mipaka yake ya kazi?

Hapa ndipo Zito anadhihirisha kutumikia maslahi ya SCB. Yeye mwenyewe alikiri kuwa mwaka 2009 alifuatwa na Balozi wa Uingereza na ujumbe wa SCB akawakatalia. Lakini Zito anataka kutuaminisha kuwa miaka mitano baadaye alikuwa bado na msimamo uleule na kujinasibu kuwa ni mzalendo. Maazimio ya PAC kubeba azimio la kuitaifisha IPTL ambyo ni mbinu chafu ya SCB tangu mwaka 2009 waliyotaka kuifanya kupitia Bungeni kwa kukwepa njia ya Mahakama na jitihada ambazo PAC ilionekana kulinda maslahi ya SCB inadhihirisha kuwa Zito na kundi zima la PAC walitumiwa kwa maslahi yao. Kwa hiyo Zito hana hata chembe ya uzalendo.

Ni vyema kabisa Serikali ikamuangalia vizuri Zito na kudhibiti hila zake chafu ambazo ziko dhahiri kabisa. Bunge linapaswa kuiangalia kwa makini Kamati ya PAC kwa ilichokifanya kuleta taharuki isiyokuwa na sababu ambazo madhara yake ni makubwa kwa wananchi kuondoa Imani kwa Serikali yao, wahisani wakasitisha fedha za misaada ya bajeti na maendeleo hayo yote kutokana na uzushi wa Zito. Huyu ni mtu hatari kama Hitla. Asipodhibitiwa anaweza kuliangamiza taifa.

Tufikirie kwa makini na tuache mzaha, Zito na Kafulila hawafai katika jamii ya watu Wastaarabu ni wazushi, wachochezi na wasaliti wakubwa. Ni hatari sana kuamini kila wakisemacho katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Inaelekea wanahofu kwa hatma na maisha yao ya kisiasa, kwa hiyo muda huu ni wajasiliamali wa kisiasa na hilo ndilo lililoko mbele yao bila kujali madhara yake.

Too late to kamataling a train. Stanbic kulikua nini?
 
Iwapo wananchi wangepata fursa ya kuisoma ripoti ya CAG kuhusu uchunguzi wa Akaunti ya Escrow ya Tegeta kabla ya kumsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) alipowasilisha taarifa yake bungeni bila shaka wangegundua uongo wa wazi uliotolewa na kamati hiyo. Rais Kikwete alitambua udhaifu wa taarifa ya PAC ndio maana aliagiza ripoti ya CAG isambazwe na kusomwa, kabla hata yeye hajafikia maamuzi. Na kwa hakika maamuzi na ufafanuzi wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwamba fedha iliyokuwa kwenye Akaunti ya Escrow ya Tegeta ni ya IPTL yamezingatia ripoti ya CAG.

Ni lini Wananchi waliisoma ripoti ya CAG? Kwa nini iwe hii tu? Huruma hiyo kwa Wananchi imeanza lini? Acha kuwafanya Watanzania mazombie!

Mbona mikataba ya madini na gesi hao leo unaowaita Wananchi hawapewi!? Kuna ajenda gani leo hadi mwananchi anaonekana wa maana apewe ripoti. Mbona ripoti ya PCCB hapewi!
 
Kumbe ulisikia vizuri kwamba pesa zile hazikuwa za umma! Sasa tatizo liko wapi? Hiyo ndio hoja ya msingi. Na kama ni hivyo, kwa nini Zitto na malimbukeni wenzake wanaendelea kudai kuwa zilikuwa za umma? Hayo ndio maswali ya kujiuliza.

Umeamua kujitoa ufaham kwa makusud huku nafsi yako inakusuta. Ni fisadi pekee ataamini umma hauna hela zake kwenye account ya escrow. Ni mtu anaefuata mkumbo pekee ndo ataamini kuwa umma haukuwa na hela zake.
Iko very clear kwamba pesa zile IPTL anazo za kwake, Tanesco nae alipaswa awe na za kwake baada ya kupiga hesabu ya bei halali ya umeme. Serikali nayo ilitakiwa ilipwe kodi yake. Hizo zote ni hela za mimi wewe na mtanzania mwingine ambazo kama serikali ingepata stahiki zake basi huduma za kijamii zingeboreka.

Hata namna wa mgao ukiangalia trend ziligawiwa kwa uwiano au percentage kutegemea na mchango wa kila mmoja alivyofanikisha pesa kutoka. Hebu angalia:-
Tsh Million:40.4-80.8-404-1600 nk! Hivyo utaona ni 40.4, 40.4*2,40.4*10 nk! Kuna mchezo mchafu hapo!
 
Pengine jana haukusoma magazeti lakini habari hizo hata hapa JF ziliwekwa tangu jana zikimnukuu Mh. Mwigulu Mchemba.

Mkuu wanatupa matumainim tu, ila tujipe mda tutajioonea wenyewe tu. Je wakandarasi watarudi maeneo yao ya kazi/site? Na si kusikiliza maneno ya mtabiri na kuja kutuambioa tu kuwa wafadhili wameanza kuachia fedha zao.
 
Watu msifikie hatua ya kufikiria kwa ajili ya mtu mwingne, pesa ile ilikuwa na mgogoro ,ilikuwaje kabla ya kumaliza mgogoro pesa iwe ya iptl? tatizo wachangiaji wengi wapo kimaslahi, nchi haitaendelea kwa kuwa na watu wanaotazama matumbo yao.over
 
Umeamua kujitoa ufaham kwa makusud huku nafsi yako inakusuta. Ni fisadi pekee ataamini umma hauna hela zake kwenye account ya escrow. Ni mtu anaefuata mkumbo pekee ndo ataamini kuwa umma haukuwa na hela zake.
Iko very clear kwamba pesa zile IPTL anazo za kwake, Tanesco nae alipaswa awe na za kwake baada ya kupiga hesabu ya bei halali ya umeme. Serikali nayo ilitakiwa ilipwe kodi yake. Hizo zote ni hela za mimi wewe na mtanzania mwingine ambazo kama serikali ingepata stahiki zake basi huduma za kijamii zingeboreka.

Hata namna wa mgao ukiangalia trend ziligawiwa kwa uwiano au percentage kutegemea na mchango wa kila mmoja alivyofanikisha pesa kutoka. Hebu angalia:-
Tsh Million:40.4-80.8-404-1600 nk! Hivyo utaona ni 40.4, 40.4*2,40.4*10 nk! Kuna mchezo mchafu hapo!

1. Ni vyema ukajenga hoja ya kutuaminisha kuwa kweli ulisoma Ripoti zote mbili na kutuaminisha kwa rejea ya vifungu, vinginevyo ni wale wale mnaopenda kusikiliza na kuamini bila ya kufanya tafakari kutokana na kujiridhisha na ukweli ulio wazi.

2. Formula ya mgao ni dhana unayoijenga kichwani kwako kutokana na kukosa hoja ya ki mantiki hapo juu. Unapojenga hoja kwa kutumia hisia, unajinyima haki ya hoja yako kupewa uzito. Inakuwa ni hoja isiyokuwa na mashiko. Hizo ni sawa na ndoto ambazo kila mmoja anayo haki ya kuota lakini je, ndoto si zinabaki kuwa ndoto tu?
 
wewe usiye kuwa na akili timamu subiri kesi ya kudai hela zaondiyo utaelewa. pesa zimeibwa kwa nini huelewi?? wahisani wamegoma kutoa misaada kwa sababu hiyo wewe unaleta pumba zako hapa.

Msipende kutukana watu mnaopishana hoja.Ni jambo la kawaida kupishana, la msingi ni kujibu hoja kwa hoja na watu wataona wenyewe kilaza na mwenye akili.
 
Wanajukwaa pse!
Mwenye namba ya Ruge, nshafungua account bank!
 
tatizo mlilo nalo wengi wenu ni uvivu wa kusoma. Lakini pia inasikitisha kushindwa hata kusikiliza mkaelewa! Kuwepo kwa kodi ni jambo tofauti ambalo halileti maana ya fedha kuibiwa. Utaratibu wa kulipa kodi ni jambo tofauti kabisa na ni jambo endelevu. Tra wanapaswa kudai hiyo kodi. Tatizo la uongo na uzushi wa pac lipo wazi kwani wao walidai pesa iliyoibiwa ni ile ambayo haikuwemo kwenye escrow account lakini wameliaminisha taifa kwa kutumia tarakimu kubwa za uongo. Iptl/pap hawawezi kuiba fedha zao. Licha ya hivyo, tofauti kati ya fedha ya kodi na ile pesa waliyoisamehe tanesco ni kubwa mno. Inaelekea wengi mlioaminishwa uzushi wa pac hata hesabu ya kujumlisha na kutoa, hamuijui.


kweli, watu wanashabikia tu haya mambo lakini hawana uelewa au hawataki kusikia kitu tofauti na walichoaminishwa.
 
kwa akili hizi kweli kupata maendeleo halisi ni ndoto,yaani kuna watu tena mbaya zaidi ni vijana wanatetea maovu yanayofanyika hapoa nchini kwetu kisa tu kuipenda ccm au?
 
kwa akili hizi kweli kupata maendeleo halisi ni ndoto,yaani kuna watu tena mbaya zaidi ni vijana wanatetea maovu yanayofanyika hapoa nchini kwetu kisa tu kuipenda ccm au?

Mkuu, hili sio swala la CCM au Ukawa; tunajadili facts. Haiwezekani tuachie watu wakurupuke na kuwapakazia wengine kuwa ni wezi. Wamemuibia nani?
 
PAC ni mtambo wa kufua uongo

Naona yule madame Speaker nae ame surrender kiti siku hizi amekuwa kama JOB NDUGAI.

Huyu bwana Zungu anafaa sana kukaa pale juu.
 
Sidhani kama wewe umewahi hata kuiona hiyo ripoti ya CAG. Pia sidhani kama unaelewa maana ya Escrow Account. Wewe ni miongoni mwa walioingizwa choo cha kike na Zitto na timu yake. Kutafuta umaarufu sasa kunawatokea puani wahuni hawa.

Ujinga utaacha lini wewe, kama umepata mgao si utulie unataka kutusumbua akili, si yema kubisha vitu vikowazi, kamuulize prof mwandosya alichosema bungeni kuhusu ESCROW A/C
 
Mko wengi sana

Tupo wengi na bado wengi wanafunguka zaidi tunaotaka ufafanuzi na vielelezo vya wizi huo, hatuhitaji mihemuko tu bila ufafanuzi. Je umeelewa ufafanuzi wangu ninapojenga hoja kwamba hakuna wizi wa pesa ya malipo ya wabia wa kuiuzia Tanesco umeme bali ni halali yao kadiri ya mkataba na kwamba kama ni pesa ya umma basi ni kukata kodi tokana na pesa hiyo jambo ambalo Bank ya mkombozi katika taarifa yake kwa umma ilieleza kuwa lilikuwa sharti ya kutekelezwa kwanza kabla ya pesa kuchukulia?
 
Ujinga utaacha lini wewe, kama umepata mgao si utulie unataka kutusumbua akili, si yema kubisha vitu vikowazi, kamuulize prof mwandosya alichosema bungeni kuhusu ESCROW A/C


Hv kweli ulikubaliana na Mwandosya aliposema kuwa ni pesa za serikali kwa vile zilikuwa zinaonekana kwenye vita vya mahesabu ya TANESCO na BOT?Hii ilikuwa arguement weak mno.Kwani watu waliotunza hela zao BANK zinakuwa sio zao tena?AYA KANDA!
 
Wewe Kweli mata.ko, akili zako zipo mkund.uni, aliyeongea pumba jk, eti mtu anamakosa kimaadili alafu unamuomba akupishe badala ya kumshtaki,

"kazi kucheka cheka tuu"

Hivi kweli ripoti ya CAG kweli umeisoma vizuri au unazungumza usilolijua , kama ungelisoma ripoti hiyo sidhani hata ungekuwa unaandika habari hizi hapa. Kwa kifupi PAC ilihongwa kuwapotosha watanzania na haikufanya kazi kwa maslahi ya watanzania kila mtu analitambua.
 
Wakandarisi mbona wapo site jamani mbona hii nchi watu wambea sana hau amtembei mikoani
 
Hivi kweli ripoti ya CAG kweli umeisoma vizuri au unazungumza usilolijua , kama ungelisoma ripoti hiyo sidhani hata ungekuwa unaandika habari hizi hapa. Kwa kifupi PAC ilihongwa kuwapotosha watanzania na haikufanya kazi kwa maslahi ya watanzania kila mtu analitambua.

Endelea kuweweseka tu! Hivyo Wabunge wote wale hawana akili, ila mwenye akili ni wewe pekee. Wabunge wote wale hasa wa kamati ya PAC wengi wakiwa kutoka CCM wamekula rushwa ili kuwaonea wenzao? Hivi ni kweli kichwa chako kipo sawa? Hivi tu kwa kuikosesha tu serikali pesa yake ya kodi, hiyo tu pekee haitoshi mtu kuwajibika, achilia makandokando mengine? Pamoja na ushabiki, uwe na huruma na Watanzania wenzako.

Hata mh Rais wakati anahutubia wazee wa Dar, alikemea wabunge wa chama chake ambao walitetea kishabiki kuwa hakukua na ubadhirifu katika sakata la Escrow! Au hukumsikiliza? Kama alikemea, alikemea kitu gani kama siyo pasi na shaka kulikuwa na hila katika utoaji wa fedha husika.
Tukubaliane mambo fulani ya msingi:-
1. IPTL ina fedha zake tena nyingi katika ile Account
2. Tanesco nayo ina pesa zake baada ya ukokotoz upya wa bei
3. Serikali ina hela zake za kodi mabalimbali stahiki kulipwa. Na kitendo tu cha kukwepa kodi ile ilitakiwa mtu awe mahabusu.
4. PAC kama binadamu lazima kwenye ripoti yao itakuwa ina mapungufu kwa kiasi fulani. Lakini hiyo haiwez kuondoa ukweli wa taarifa yao. Kumbuka CAG alihojiwa kwa kiapo na PCCB walitoa taarifa yao pia. Tukumbuke pia Ripoti iliwasilishwa Bungeni watu wakaisoma na kuchangia. Hata maazimio ni ya Bunge zima siyo PAC tena!
 
Huu mjadala mwingine umeanza, hakuna hata mmoja hapa atakayefafanua wizi huo ila ni mhemuko wa kufutata mkombo kwamba pesa ni zawili. Fafanueni wizi ulitokeaje tuwaunge mkono, lakini kuhemuka kwa kufuata mkumbo siko tayari.

Ukimsoma vyema CAG utaielewa vyema ripoti nzima,hasa kwa wale wenye TAALUMA yao kwa maana ya WAKAGUZI na WAHASIBU.

Pesa ni ya wizi sababu zangu kuu zaweza kuwa tatu au nne.:

1.Pesa ile ilikuwa bado iko kwenye mgogoro wa pande mbili na ulikuwa unasubiri suluhisho toka MAHAKAMA ya kimataifa kuhusu uchakachuaji wa bei ya umeme iliyokuwa inalipwa na TANESCO kwa IPTL,kwa kuwa walalamikaji waliona wanalipa toza kubwa kuliko ilivyotakiwa,hivyo walifungua kesi na bahati nzuri walishinda,lakini hakuna mchanganuo uliokwihsa fanyika wakuweza kujua pesa za IPTL ni ngapi na za TANESCO ni ngapi,hivyo kwa mantiki hii pesa za UMMA hapa zimepigwa na wajanja.

2.Hakimu hakutoa maamuzi pesa hizi zilipwe kwa PAP kwa maana bado kesi ilikuwa ipo mahakamani kuhusu TOZO na mchanganuo wa pesa hizi haujafanywa hivyo kusema MAHAKAMA imeamua hata zile pesa zilizokuwepo kwenye account yenye pesa za wahusika wengi ni za PAP siyo sahihi,basi hapa wale wachache wanaojua kutumia ELIMU yao waliyoipata kwa KODI ya mtanzania vibaya wakaamua kuchota kisichohalali kutumia ELIMU yao hii kwa maana ya AG wetu,hakuwa na sababu ya kutoa idhini pesa zilipwe wakati anajua wazi si sahihi,lakini kwa sababu zake mwenyewe na wahusika aliamua kupindisha HUKUMU kwa maslahi yao wachache.

3.Kuna kodi hapo haikulipwa na ilitakiwa kulipwa kabla malipo hayajafanyika,hivyo basi hata hili nalo halikuonekana kuwa ni baya kwa viongozi wetu wakatumia vibaya mwanya wa elimu na nafasi waliyonayo kufanya maamuzi mabaya na kuhujumu mali ya umma.

4.Pesa ni ya IPTL si ya PAP kwa nini walipwe PAP na si IPTL?Na hapa hata leo JR akienda mahakamani kuishtaki serikali kuhusiana na pesa yake iliyokuwemo kwenye hii account anashinda tena kwa kishindo,sababu ana haki juu ya FAIDA iliyotokana na mauzo ya umeme baada ya kukokotoa TOZO halali,na kila muhusika kuchukua cha kwake kulingana na mahesabu.

5.Hivi serikali ilishindwa nini kufuatilia uhalali wa huyu singasinga kununua hisa za MERCHMAR?Na siyo kweli kwamba walikuwa hawamjui huyu kuwa ni TAPELI la kutupwa,amefilisika wanajua vyema sana kila kitu,lakini waliamua kufanya sababu walikuwa wanajinufaisha wao na familia zao!

Leo tuna mtu aliyepewa ZABUNI ya kuendeleza reli ya kati,na wanajua mtu huyu amefilisika na sheria za kufilisiwa wenzetu wanasheria wanazijua na hasa Mwakyembe iweje leo tumkumbatie mtu aliyefilisika,tunatafuta nini kwake zaidi ya kuliumiza TAIFA kiuchumi?

6.Jiulize ni kwa nini MASWI mpaka dakika za mwisho alikataa kuidhinisha pesa hizi kutoka,ila ni baada tu ya WAKUU wa nchi kuidhinisha pesa zitoke ndipo alipokubali kutoa,hebu tufikirie alilipwa ngapi?Je alitishwa ili akubali?Alifanywa nini huyu mtu,mpaka alidiriki kusema wakimwaga MBOGA atamwaga UGALI

Haya ndiyo mambo makuu ambayo ukiyaangalia vyema si MUHONGO,WEREMA,MASWI wala RAIS angediriki kuuchekea wizi huu.Ila sababu wote hawa wamekosa uhalali wa kuwa viongozi,wamelewa madaraka,si wazalendo hata kidogo,ni sawa na mwizi aliyeshindwa kumuibia jirani akaamua kujiibia mwenyewe.

Tujitahidi kuwa WAZALENDO tuwe tayari kulinda maslahi ya TAIFA letu,tuwe wamoja,tuwe TAIFA kwanza VYAMA baadaye.Tuchague viongozi wenye WELEDI,WAOGA wa MUNGU,WANYENYEKEVU,WAZALENDO,WATAKAO KUWA TAYARI KULIFIA TAIFA LAO.

Haya ndiyo maoni yangu,kwa TAALUMA yangu hizi pesa zipo za TANESCO,za TRA na za IPTL,hivyo kilichofanywa na viongozi wetu ni kuliibia TAIFA lao mchana kweupe,wakishirikiana na wanaowaita wawekezaji,ambao ni MATAPELI.

Na leo Sethi kanunua visima vya mafuta,hakuja na pesa zaidi ya ile $300,000,tumempa mamilioni ya dollar,hivi kweli VIONGOZI wetu wanafikiri kutumia nini?Hivi kwenye vichwa vyao kuna maji au ubongo?Hivi ni kweli walipoenda shule wameelimika au wameenda kuja kusoma na kuandika tu?

Candid Scope haya ni mawazo yangu kulingana na TAALUMA yangu,sijahongwa wala sitegemei kuhongwa sababu UTU wangu hauna bei.
 
Back
Top Bottom