Akili ya kijinga ni kupinga ukweli pole sana
Kudhihirisha kwamba Zito ni mchochezi, kwenye Ripoti yake ya PAC iliyopo kwenye tovuti ya Bunge la Tanzania, ukurasa wa 21 inakiri kwamba fedha waliyolipwa PAP ni Sh. 203.1billioni na kwamba fedha iliyotakiwa kuwa kwenye Escrow Account ni Sh. 306,675,081,939/=
Kumbe inaelekea hiki ndicho Zito na wapinzani hata waliomo ndani ya CCM walichokuwa wakiogopa kisijulikane pale Rais alipoagiza Ripoti ya CAG iwekwe wazi wananchi tuisome. Pamoja na Rais kutolea ufafanuzi suala hilo bado Zito anaendelea na upotoshaji! Maadili tu ya kawaida ya ki-Afrika hayaruhusu hili kutokea. Hii inatia mashaka hata malezi na makuzi ya Zito.
Lakini kwa makusudi kabisa na kwa kuongozwa na nia ya uchochezi ukurasa wa 47 Maoni na Mapendekezo ya Kamati, Ripoti ya PAC umetumia maneno makali ya uchochezi tofauti na ukweli waliouandika wenyewe ukurasa wa 21, ninanukuu "Mfumo mzima wa Serikali ulipata ganzi au uliganzishwa ili kuwezesha zaidi ya shilingi bilioni 306 kuporwa kutoka Benki Kuu ya Tanzania na kutakatishwa kupitia benki mbili hapa nchini"
Kwa mtu yeyote mwenye akili ya kawaida tu, atagundua kwamba kubadilisha matumizi ya neno "iliyolipwa" ukurasa wa 21 kuwa "kuporwa" ukurasa wa 47 na kuamua kutumia kiasi cha fedha ambazo hazikuwemo kwenye Escrow Account, ni mbinu ya kufanya propaganda ya uchochezi.
Zito, alitumia wadhifa wake kama M/Kiti wa PAC vibaya na labda kwa kuhongwa au kuingia kwenye dili chafu ya Standard Chartered Bank iliyotaka kinyemela kuiba fedha za IPTL kwenye Escrow Account kwa kutumiwa na Mkono, Mengi na wanasiasa wanaotafuta u-Rais 2015.
PAC kutolea maamuzi ya uhalali wa SCB wakati kesi ziko mahakamani na kumuandama Mh. Masele, Naibu Waziri wa Nishati na Nadini kwa kumkemea Balozi wa Uingereza kutojiingiza kwenye mambo ya Wizara yake, ni ushahidi tosha kwamba Zito, alikuwa anaongozwa na dhamira ovu na maslahi binafsi, hakutumia hata chembe ya busara. PAC lini imekuwa juu ya Mahakama? Na je, Mh. Masele ni kosa lipi alilokuwa amelifanya kwa kumkumbusha Balozi wa Uingereza kuheshimu mipaka yake ya kazi?
Hapa ndipo Zito anadhihirisha kutumikia maslahi ya SCB. Yeye mwenyewe alikiri kuwa mwaka 2009 alifuatwa na Balozi wa Uingereza na ujumbe wa SCB akawakatalia. Lakini Zito anataka kutuaminisha kuwa miaka mitano baadaye alikuwa bado na msimamo uleule na kujinasibu kuwa ni mzalendo. Maazimio ya PAC kubeba azimio la kuitaifisha IPTL ambyo ni mbinu chafu ya SCB tangu mwaka 2009 waliyotaka kuifanya kupitia Bungeni kwa kukwepa njia ya Mahakama na jitihada ambazo PAC ilionekana kulinda maslahi ya SCB inadhihirisha kuwa Zito na kundi zima la PAC walitumiwa kwa maslahi yao. Kwa hiyo Zito hana hata chembe ya uzalendo.
Ni vyema kabisa Serikali ikamuangalia vizuri Zito na kudhibiti hila zake chafu ambazo ziko dhahiri kabisa. Bunge linapaswa kuiangalia kwa makini Kamati ya PAC kwa ilichokifanya kuleta taharuki isiyokuwa na sababu ambazo madhara yake ni makubwa kwa wananchi kuondoa Imani kwa Serikali yao, wahisani wakasitisha fedha za misaada ya bajeti na maendeleo hayo yote kutokana na uzushi wa Zito. Huyu ni mtu hatari kama Hitla. Asipodhibitiwa anaweza kuliangamiza taifa.
Tufikirie kwa makini na tuache mzaha, Zito na Kafulila hawafai katika jamii ya watu Wastaarabu ni wazushi, wachochezi na wasaliti wakubwa. Ni hatari sana kuamini kila wakisemacho katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi mkuu. Inaelekea wanahofu kwa hatma na maisha yao ya kisiasa, kwa hiyo muda huu ni wajasiliamali wa kisiasa na hilo ndilo lililoko mbele yao bila kujali madhara yake.