Endelea kuweweseka tu! Hivyo Wabunge wote wale hawana akili, ila mwenye akili ni wewe pekee. Wabunge wote wale hasa wa kamati ya PAC wengi wakiwa kutoka CCM wamekula rushwa ili kuwaonea wenzao? Hivi ni kweli kichwa chako kipo sawa? Hivi tu kwa kuikosesha tu serikali pesa yake ya kodi, hiyo tu pekee haitoshi mtu kuwajibika, achilia makandokando mengine? Pamoja na ushabiki, uwe na huruma na Watanzania wenzako.
Hata mh Rais wakati anahutubia wazee wa Dar, alikemea wabunge wa chama chake ambao walitetea kishabiki kuwa hakukua na ubadhirifu katika sakata la Escrow! Au hukumsikiliza? Kama alikemea, alikemea kitu gani kama siyo pasi na shaka kulikuwa na hila katika utoaji wa fedha husika.
Tukubaliane mambo fulani ya msingi:-
1. IPTL ina fedha zake tena nyingi katika ile Account
2. Tanesco nayo ina pesa zake baada ya ukokotoz upya wa bei
3. Serikali ina hela zake za kodi mabalimbali stahiki kulipwa. Na kitendo tu cha kukwepa kodi ile ilitakiwa mtu awe mahabusu.
4. PAC kama binadamu lazima kwenye ripoti yao itakuwa ina mapungufu kwa kiasi fulani. Lakini hiyo haiwez kuondoa ukweli wa taarifa yao. Kumbuka CAG alihojiwa kwa kiapo na PCCB walitoa taarifa yao pia. Tukumbuke pia Ripoti iliwasilishwa Bungeni watu wakaisoma na kuchangia. Hata maazimio ni ya Bunge zima siyo PAC tena!
1. Taarifa ya PAC ilichanwa chanwa na Prof. Muhongo alipotoa msimamo wa Serikali Bungeni.
2. Kwani wabunge wa CCM hawawezi kuwa wajasiliamali wa kisiasa, kama wengi wa waliochangia walivyoonyesha?
3. Suala la ukokotoaji halina mantiki hasa pale linapojengwa kwenye ushauri wa Mkono Advocates & Co aliyeipotosha TANESCO kugomea utekelezaji wa maamuzi ya ICSID 1 ya Mwaka 2001, yaliyoipatia ushindi TANESCO na kushusha gharama kutoka US$ 3.6 hadi US$ 2.6 kwa kuzingatia gharama za mtaji wa wawekezaji. Badala yake Mkono akashauri wagomee hata maamuzi hayo kwa madai ya kwamba mtaji wa IPTL ni Sh. 50,000/= tu.
4. Hivi kweli inakuingia akilini kwamba huo ulikuwa ni ushauri mzuri wenye kutumia hata chembe ya akili kwa TANESCO? Ndiyo maana hata TANESCO yenyewe baadaye waliutilia mashaka wakaomba ushauri wa ziada kutoka kwa kampuni ya uwakili ya Hunton and Williams ya Marekani, ambayo iliuona ushauri huo kuwa ulikuwa ni dhaifu na haukuwa na mantiki.
5. Zito bado anarudi na hoja za ukokotoaji wa capacity charges kwa kutumia mtaji wa Sh. 50,000/= na kwa ujanja anaingiza ICSID 2 ambayo inawahusu SCB na bado watanzania hamuoni kwamba huyu mtu alikuwa anatumiwa? Tukubaliane, kama alivyosema Rais mwenyewe na ukweli ulivyo hili jambo lina historia ndefu na masuala mengi ya kisheria. Kwa hiyo ni vigumu kwa wengi kulielewa na kuweza kuchangia kwa mantiki na hoja. Umejaribu lakini bado hujaelewa vizuri.