Laiti marais wote wa nchi za afrika mashariki wangeshikamana wakawa kitu kimoja huenda wazungu wakatapa shida sana

wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
24,688
26,796
Kama wangekaa wakawa wamoja kama mh rais magufuli alivyosema wakashikamana ushirikiano wa kupiga vita wazungu watapata shida sana maana ukiangalia hawa wazungu wana maslahi makubwa sana kwenye hizi nchi za afrika mashariki.

Nimejaribu kuangalia msaada wanaotoa kwa mfano wa kulnda amani kule drc kongo nikagundua hakuna mzungu hata mmoja mweńe jehi lake kule zaidi jeshi la nje ya afrika ni india tuu.

Wao wakileta vitu wanashuka na chopa yao au ndege tena porini na kuchota kinachowafaa na kupaa kwa mgongo wa walinda amani kumbe kuna manufaa wanafaidi.

Kitu kingine imejiuliza kwa mfano imetomea labda adui( muasi)akishambilia wanaokufa ni askari wa nchi zetu tuu mbona wao hawalengwi?wanapasuka wa kwetu tu? Nimegundua hawa kuta kitu wanakuja kuchota (madini) na kuondoka nayo wanaacha watu wanazidi kuuwana wao wanatumia hiyo fursa.

Inabidi hizi nchi Marais wakae wafikirie hili jambo kama wakikubaliana kuunda jeshi moja la umoja wa nchi za afrika huenda hawa mabeberu tukawatesa sana maana kuna kitu watakosa kwetu ambacho wanakuja kuchukua kwa gia msaada wa vifaa vya kijeshi kulinda amani alafu wakipaa wanapaa na mzigo
 
Mh Rais Jpm kiongozi wa mfano kuna dalili naziona Afrika ya mwaka 2025 itakuwa sio hii tunayo Ishi.
 
Back
Top Bottom