Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,640
- 729,670
Mapupu ni mojawapo ya viungo vya mwili vya mnyama, mapupu yanapatikana tumboni maeneo yaliyopo maini figo bandama nk.... nyama ya mapupu ni laini sana kushinda nyama nyingine yoyote ile ila kwa bahati mbaya sana ni nyama iliyokosa thamani kuliko nyingine zote...huwezi ikuta buchani wala imepikwa kama mboga...mapupu ni maalum kwa ajili ya supu tena kwa watu wenye kipato cha chini.
Tuliowahi kuishi vijijiji tunafamu kuna maeneo ya mabwawa na mito kuna vyura wana kelele hasa, lakini ukikaribia tu wananyamaa kimya tuli kabisa, lakini wanakuona wewe huwaoni.
Madawa ya kulevya ni janga la dunia, ni adui anayeteketeza mabilioni ya dola kila mwaka kwa ajili ya kupambana naye! Licha ya hayo mabilioni ya dola lakini ni adui aliyetekekeza roho nyingi na kuharibu mali pia...ni vita ngumu hasa pengine ngumu kuliko ugaidi.
Tunatambua juhudi za serikali yetu kama taifa kwenye hii vita ngumu dhidi ya madawa, tunatambua pia juhudi za vikundi na hata mtu mmojammoja katika mapambano haya....tuzidi kutiana moyo bila kukatishana tamaa
Hii ni vita inayohitaji maandalizi thabiti, ina mtandao mkubwa wenye kuhusisha watu wazito hasa. ..!
Mikurupuko ya kisiasa ya kuwakamata vijana wachache mapusha hakutatuongoza popote kwenye kuuvunja huo mtandao uliojipanga vema...ni sawa na kutaka kutibu malaria kwa panadol
Tanzania inasemwa kama mojawapo ya njia kuu za kusafirisha midharati...je kuna lolote limefanyika hapa? !
Kuna list ndefu yenye majina zaidi ya 500 yakitajwa kama ndio mtandao wa madawa ya kulevya Tanzania...! Je yameshughulikiwa kwa kiasi gani?
Kauli kali kali za kisiasa hazitatau hili tatizo! Kamatakamata hii inayoendelea ni ujinga kiwango cha lami kwakuwa hakuna kesi itakayopelekwa mahakamani!ukosefu wa Ushahidi thabiti utawafanya wengi waachiwe huru kama ilivyotokea huko nyuma.
Drama za kibongo zimetubeba juu kwa juu kuhusu mapambano ya madawa ya kulevya kwa kukamata wasanii na wale wanaoitwa watu(vijana)maarufu bongo. ..episode hii imepakwa rangi za kung'aa na kuvutia hasa ni mijadala kila mahali.
Hili likiendelea hivi ni sawa na kukaribia lile ziwa lenye vyura wengi wanaopiga kelele zinazosikika toka mbali, lakini wakishahisi uwepo wako wanatoweka pamoja na sauti zao lakini wanakuona live.
Tusijifanye tunakula supu ya nyama ya minofu wakati kiuhalisia ni supu ya mapupu ambayo ni laini sana.
Ukitaka kuifahamu vema hii vita waulize wabrazil na wa Mexico kwa kuwataja hawa kwanza