Ladha yangu, undani wangu, uhalisia wangu

Ladha yangu, undani wangu, uhalisia wangu

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,661
Reaction score
870,345
Hatufanani kwenye maisha
Kila mtu ana ladha yake (taste)
Kila mtu ana shauku yake (passion)
Kila mtu ana hisia zake (feelings)
Kila mtu ana utamaduni wake (culture)

Mambo hayo manne hututambulisha kwa wengine kwa chochote na kwenye lolote. Ni rahisi sana watu wakikiona kitu na kusema..'mambo ya fulani hayo, hapo tafsiri yake ni moja tuu kwamba hadhira/jamii imeshakufahamu na kukujua vema kuwa wewe ni mtu wa namna gani na unataka nini.

Hivi vitu hivi. Haya mambo haya yana faida na hasara zake.
Faida ni pale linapotokea jambo la kheri, na hasara ni pale linapotokea jambo la shari.

Niliwahi kuvunjiwa nyumbani miaka hiyooo.. Wevi waliiba vya ndani na vya kwenye gari.. Kwenda kutoa ripoti polisi mahojiano tu ya awali yaliwapa polisi picha kamili ya wezi ni akina nani...!

Kuna wezi kwa kutumia madawa
Kuna wevi wa kutumia nondo, mapanga na silaha nginyinezo
Kuna wevi wa vikundi
Kuna wevi jeshi la mtu mmoja
Kuna wevi wa tv tuu nknk
Polisi wanawafahamu wote hao

Hata kwenye mavazi, starehe na vyakula kuna hizo aina kwa kila mmoja bila kusahau kwenye mahusiano wazee wa tandam na wale wa tumishkaki twa mia kama nyama ya sambusa

Yote hayo yalikuwa story tuu za kuzunguka mbuyu..kwenye migulu mine ladha zangu hizi hapa.. Nitazunguka kote lakini hapa home is best .. Iwe mvua liwe jua.. Hapa ndio tulizo la moyo wangu [emoji7]
Screenshot_20220905-222850.jpg
FB_IMG_1662406344945.jpg
Screenshot_20220905-223153.jpg
 
Bugatti... Hazijawahi kunishawishi
Screenshot_20220905-230458.jpg
 
Pambana one day yes! Dreams do sometimes come reality.
 
Back
Top Bottom