Laana Aliyoacha Benjamin Mkapa Ni Kweli? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Laana Aliyoacha Benjamin Mkapa Ni Kweli?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ndallo, Jul 15, 2011.

 1. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Nakumbuka maraisi waliomtangulia Jakaya Kikwete waliacha wosia au ndio tuiite ni laana! Mwalimu alicha wosia mwingi sana kwa taifa hili hata kwenye Tape zinazouzwa mitaani ni tosha kabisa kuamini alichokua anakiongea na vinaonekana sasa hivi, sikumbuki raisi mwinyi aliacha wosia gani kama kuna mtu anakumbuka aliacha wosia gani kwa taifa hili baada ya kumaliza muda wake wa kuongoza taifa hili atatueleza. Lakini mimi kuhusiana na heading yangu hapo juu nakumbuka baada ya miongo miwili ya utawala wa muheshimiwa Mkapa aliwacha wosia kwakusema hivi "MTANIKUMBUKA" mwisho wa kumnukuu! Wanajanvi natafakari sana kwakina huu usemi kama ukijaribu kutafakari alipotuacha na hapa tulipo, Je wanajanvi usemi huu ndio tunachokiona sasa hivi ?? Jamani naomba kuwasilisha.
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tutamkumbuka kwa kuuza nchi, EPA, IPTL, na kutuletea timu ya RICHMOND na takataka nyingine.

  Katuachia Rais Mzuri sana ambaye kweli ukiwalinganisha, pamoja na WIZI wa Mkapa, unaona kumbe ana nafuu.

  Angelishinda Slaa, sasa hivi nina imani tungelikuwa tunaimba wimbo mwingine.
   
 3. Msema hovyo

  Msema hovyo Senior Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 195
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Vision ya Mkapa ya kumaliza umasikini wa Tanzania by 2025, naona Kikwete katia kapuni, halafu ile mikakati ya kupunguza umaskini aliyokuwa nayo Mkapa kama vile MKUKUTA, MKURABITA, PEDP, SEDP, naona yote hivi sasa inalegalega. Tumepata rais ambaye kila kuchwapo yupo angani, hana muda wa kukaa ikulu atatue matatizo ya watanzania. Binafsi sioni kama maneno ya Mkapa ni laana, bali laana yenyewe ni Kikwete. Maana Mkapa kwa nafasi yake alikuwa na uwezo wa kumpiga vita Kikwete asigombee urais.
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Ni kweli mkuu, tunamkumbuka sana,
  katuachia meremeta, mwananchi tangold, Anaben bank, EPA, kiwira, soko holela, mikataba mibovu ya madini, kuuzwa kwa shirika la ndege (ATC) likiwa na ndege zaidi ya 15 na kurudishwa likiwa na ndege 1, kuuzwa NBC kwa bei ya chee, na mengine mengi.
  Tunamkumbuka sana tu.
   
 5. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Mkuu najiuliza tu: Mkapa alipoondoka Slaa aligombea Urais?
   
Loading...